Kukamatwa kwa mwandikishaji wapiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukamatwa kwa mwandikishaji wapiga kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ngoshwe, May 25, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Taarifa Kuwa mujibu wa Clouds FM (Jahazi) leo 25.05.2010:

  Kuna mwandikishaji wapiga kura katika eneo la Baruti shule ya msingi Kimara Baruti - Dar es salaam amekamatwa na anashikiliwa na polisi kutokana na kuendelea na zoezi la uandikishaji wapiga kura licha ya ukweli kuwa zoezi hilo lilipaswa liwe limefungwa tokea siku ya jumapili (tarehe 23.05.2010).

  Mkrugenzi wa Tume ya Uchaguzi Bw. Rajab Kilavu alipohojiwa kuhusu jambo hilo amekuwa ni zaidi ya " Samwel Kivuitu", kwa jinsi alivyo na kigugumizi na anaonekana amekosa kauli nyoofu kabisa , ametoa maelezo yanaoyjikanganya kuwa wale ambao hawakuweza kuandikishwa jumapili jioni, muda wa nyongeza uliruhusiwa tena mpaka jumatatu asubuhi (sijui waliwezaji kuwabaini),.Kilavu anasema yeye si msemaji mkuu labda iwe anayepaswa kuulizwa juu ya hilo ni msimamizi/mratibu wa eneo husika, yaani wa Manispaa ya Kinondoni. au mwandikishaji husika..(sijui imekaaje hii)...


  Yaonyesha jamaa wamejipanga tena!!.
   
Loading...