Kukamatwa kwa mtekaji wa dr ulimboka-Polisi Tanzania wanapomfikisha kichaa mahakamani

Bisek

Member
Apr 2, 2012
77
10
Nimeshtushwa na kushangazwa sana na taarifa kwamba yule anaedhaniwa kumteka dr.ulimboka alifikishwa mahakamani fasta.Akihojiwa polisi mbele ya walinzi wa kanisa la Gwajima mtu huyo alionekana kama kichaa hvi,sasa najiuliza ni kwann jeshi la polisi limekurupuka kumfikisha mahakamani mtu kama huyo,ni dhahiri huyo kichaas hakufanya tukio hilo peke yake,iweje wakurupuke tu kumfikisha mahakamani bila kufanya utafiti wa kina na kuwabaini wahusika wengine kwa ujumla wao?
 
Polisi walidhani watayamaliza fasta kuficha ukweli kwamba wao wamehusika na mpango huo kwa namna moja au nyingine, kutaka kuwahifadhi mabosi wao wasiaibike zaidi, kumbe ndio wanamwaga mafuta kwenye moto uwakao. Kova alijua kwamba anafanya usanii wa hatari ndio maana alikuwa anatetemeka na mwenye wasiwasi mwingi wakati anasoma karatasi zake za mchoro huo. Ona sasa Kenya nao wanasema wanachunguza ugaidi huo. Serikali nakwambia imeshikwa pabayaaaa!
 
Kama serikali ya kenya wamesema watachunguza hili tukio kwa kuhusishwa na mtu wa taifa lao natumaini kwa ukweli kubainika.
 
Wana mpango wa ''kumfunga'' huyu kichaa harakaharaka ili Dr Ulimboka asiwahi kutoa ushahidi mahakamani.........by the time amepona na kurudi jamaa atakuwa ''gerezani'' tayari na hakuna kesi tena
 
Nimeshtushwa na kushangazwa sana na taarifa kwamba yule anaedhaniwa kumteka dr.ulimboka alifikishwa mahakamani fasta.Akihojiwa polisi mbele ya walinzi wa kanisa la Gwajima mtu huyo alionekana kama kichaa hvi,sasa najiuliza ni kwann jeshi la polisi limekurupuka kumfikisha mahakamani mtu kama huyo,ni dhahiri huyo kichaas hakufanya tukio hilo peke yake,iweje wakurupuke tu kumfikisha mahakamani bila kufanya utafiti wa kina na kuwabaini wahusika wengine kwa ujumla wao?
sasa unataka kutwambia nini, kuwa waliomkamata ndio vichaa!?
 
Kama serikali ya kenya wamesema watachunguza hili tukio kwa kuhusishwa na mtu wa taifa lao natumaini kwa ukweli kubainika.

Na wakenya wasipo tafuta ukweli watatufanya tuwaogope sana maana wamezagaa sana nchini kwetu
 
Nimemsikiliza sana Dr. Ulimboka toka mkanda aliorekodiwa akiwa ICU MOI. Alieleza waziwazi watu waliomteka walifananaje. Alisema walikuwa maaskari. Huyo kijana aliyekamatwa wanaeleza kuwa katoka Murang'a nchini Kenye lakini ana pass ya Namanga. Naye anaishi Kenya siku zote na Tanzania aliingia tarehe 23 June kwa mission hiyo ya kumshughulikia Dr. Ulimboka. Ndugu zangu kama mjuavyo Kiswahili cha watu wa Kenya kinajulikana wazi bila kificho kuwa ni tofauti na Kiswahili cha Tanzania. Kama huyo kijana alihusika na sakata hilo ninaamini Dr. Ulimboka angegundua kupitia Kiswahili kuwa watekaji hao hawakuwa Watanzania. Mimi sio askari mpelelezi wa kusomea lakinini mpelelezi wa kuzaliwa ninakanusha kwa nguvu zote kuwa hawa maaskari wanawaficha wahusika wakuu katika sakata hili. LAKINI natoa tahadhari kubwa kuwa muda sii mrefu hao watajulikana waziwazi kupitia mkono mwingine usio wa serikali na ndipo aibu kubwa itawapata. Wasubiri tu na kazi inaendelea.
 
Back
Top Bottom