Kukamatwa kwa Mbowe, jaji mkuu Chande anahusika?

kila siku tunasema nchi haina kiogozi nyie mnabisha - haya sasa oneni haya mambo. miaka hii 10 tutaijutia sana, badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma.
 
KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NA NAIBU WAKE KUKAMATWA NA KUSHIKILIWA SIKU CHACHE KABLA YA KIKAO CHA BAJETI NI DALILI ZA WIZI UNAOTARAJIWA KUFANYWA NA WAKUBWA BUNGENI.
Dr. hivi unadhani mbowe atashikiliwa hadi jumatano??
 
Ni jambo la kushangaza kwa wana CDM kulalama na kuitupia lawama CCM kuwa imetia mkono kukamatwa kwa Mwenyekiti wao ambaye ni mbunge Hai, Mheshimiwa Freeman Mbowe. Haingii akilini kwa watu walio makini kutotenganisha mipaka ya kazi kati ya MAHAKAMA, POLISI na CCM. Mbowe ni mjuaji wa ufanyaji kazi na taratibu za vyombo vya sheria na dola vya nchini mwetu, tena amezungukwa na jopo la wanasheria na mawakili wanaoshinda katika viunga vya mahakama kila kukicha HIVYO ni wajuzi wa masuala ya mahakama yanavyoendeshwa.

Ni jukumu la kila mshitakiwa aliye katika dhamana kuweka kumbukumbu ya siku ya kesi, tena mheshimiwa ana kitu cha ziada kwani katika kesi yao wapo washitakiwa wengi ambao haipiti siku pasipo kuwasiliana. Pia katika kesi yao wana wakili ambaye kwa mujibu wa kazi zake ni lazima aweke kumbukumbu ya tarehe za kesi zinazohusu wateja wake. Mshitakiwa kama Mbowe ambaye ni mtunga sheria na anaetetewa na wakili, katika hali ya kawaida, hataeleweka machoni mwa jamii kuwa ameshindwa kutokea MAHAKAMANI zaidi ya mara moja pasipo kutoa sababu za maandishi kwa Mahakama husika kupitia mwakilishi wake ama WAKILI.

Moja kwa moja, ujumbe unaopatikana ni DHARAU kwa MAHAKAMA ama anataka umaarufu kupitia vyombo vya SHERIA. Hivyo Hakimu hana makosa, mkono wa sheria umechukua MKONDO wake. Watz tuchape kazi tusiingie katika mtego wa CDM na MBOWE ambao wanataka kujipatia UJIKO kupitia MAHAKAMANI na POLISI. Maandamano endelevu wamegundua hayana mvuto badala yake wanataka MISIFA kwa kuifanya MHIMILI mmojawapo wa DOLA uonekane hauna USAFI mbele ya wananchi.

KWA KUWA AMELIKOROGA, INABIDI ALINYWE SI VINGINEVYO!!!!

Kweli kabisa na kwa kuongezea tu, "ameusaga mtama aubwie mwenyewe". Wananshangaza!
 

Ntakusaidia mfano mmoja: Nchi hii kuna kundi la watu hutoa roho za wenzao kwa kuwapiga risasi lakini hawaguswi. Wanaoguswa na kutiwa misukosuko ni wengine. Rudi nyuma kuanzia 1998 (Membe Chai), 2001 (Pemba), 2011 (Arusha). Hakuna kosa kubwa la jinai kama kumuuwa mtu, lakini hapa Tanzania siyo kosa kabisa iwapo ni polisi wakifanya hivyo -- na ndiyo maana nchi hii haiwezi kutulia kamwe.

Huko Misri yule dikteta Mubarak sasa anashitakiwa kwa kuuwa waandamanaji wasio na silaha -- kama vile Pemba na Arusha. JK anaichezea sana nchi hii! I warn him.

Nawaambia Magamba: Mfungeni Mbowe, Zitto, Lissu na wengineo. Hamtakuwa wa kwanza kufanya hivyo, kwani ndo mtindo katika nchi za Afrika -- lakini ipo siku yenu, hilo mjue kabisa, unless mnabadilika.

Nauliza tu: Lipi katika vitu viwili hivi linaweza kuirudisha CCM kwenye chati mbele ya wananchi kwa haraka:

1. Kuwasakama viongozi wa CDM kwa kuwakamata, kuwafunga ets AU

2. Kuwafukuza kutoka kwenye chama Rostam na genge lake na kuwafungulia mashitaka?

Jibuni swali hilo vizuri.
 
Tuanusubiri mtujuze kinachoendelea, hakuna kulala haki hailetwi mlangoni lazima kuipigania, tunathamini mchango wenu mliopo mstari wa mbele.
 
oya tujichanganye basi fastaaaaaa oyaaaa natamani nimnyonge Mwema.grrrrrrrrrrrrrrrrr.....
 
Huu ni ushahidi mwingine wa umuhimu wa katiba mpya. Haya mambo ya muhimili wa mahakama nao kutokuwa huru kiasi hiki kama pia bunge lisivyo huru ni ugonjwa mbaya kuliko magonjwa yote ya taifa hili.
 
hizi siasa zinataka kutupeleka kwenye kupigania uhuru kama kina mandela sasa, from jail! mungu anusuru nchi hii,kama alivyosema na farao na iwe hivyo kwetu pia!
 
Leo ni siku ya kihisitoria hapa tanznia, hasa jijini dsm, wanamabadiliko wa kweli tumekusanyika hapa mTAA WA UFIPA KINONDONI dsm, tutaanza mipaparuko ya kukamatana na vibaka wa demokrasia saa tisa hii, wote wenye nia nzuri na nchi mnataarifiwa kufika hapa saa hii, mtaa wa ufipa kinondoni.

LENGO NI KUPINGA UGANDAMIZAJI WA DEMOKRASIA NA UONEVU DHIDI YA WATETEZI WA WANYONGE.

KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI NA NAIBU WAKE KUKAMATWA NA KUSHIKILIWA SIKU CHACHE KABLA YA KIKAO CHA BAJETI NI DALILI ZA WIZI UNAOTARAJIWA KUFANYWA NA WAKUBWA BUNGENI.

kama vipi leo tutwae madaraka
 
wahuni hawa wanataka kudanganya wenzao.

akili ya mbayuwayu itumbukize kwenye ya kwako.

huyu nyakarungu wala hatafika kinondoni. ffu andaa bakora nzuri kwa hawa wahuni na tandika vizuri sana
 
Nawaambia Magamba: Mfungeni Mbowe, Zitto, Lissu na wengineo. Hamtakuwa wa kwanza kufanya hivyo, kwani ndo mtindo katika nchi za Afrika -- lakini ipo siku yenu, hilo mjue kabisa, unless mnabadilika.

Nauliza tu: Lipi katika vitu viwili hivi linaweza kuirudisha CCM kwenye chati mbele ya wananchi kwa haraka:

1. Kuwasakama viongozi wa CDM kwa kuwakamata, kuwafunga ets AU

2. Kuwafukuza kutoka kwenye chama Rostam na genge lake na kuwafungulia mashitaka?

Jibuni swali hilo vizuri.


Penye red. Itakuwa vigumu kwa CCM kujibu swali hilo kwani sasa wamefika njia panda. Wangepima mood ya wananchi wangegundua kuwa wananchi wengi wangependa mapacha watatu wanachukuliwa hatua kali.

Kwa upande mwingine haidhuru CCM wangefanya vyote viwili kwa pamoja, ingewasaidia angalau.
 
wahuni hawa wanataka kudanganya wenzao.

akili ya mbayuwayu itumbukize kwenye ya kwako.

huyu nyakarungu wala hatafika kinondoni. ffu andaa bakora nzuri kwa hawa wahuni na tandika vizuri sana

pamoja na ID zako zote, ukombozi wa nchi hii lazima upatikane. haijalishi tutamwaga damu wangapi lakini lazima taifa huru lizaliwe
 
Back
Top Bottom