Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Forenaz wanazidi tu kujipenyeza at the heart of our national decision making body.
 
Mwili wako wote umejaa Pumba.
Hata huko China tunakokimbili, viwanda Kama ivi ndo wazalishaji waliowengi.
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
 
Jana iliibuka story mitandaoni ya Jeshi la Polisi kumkamata Mtanzania Halali akikamua Mafuta bila kuwa na "usajili" yaani vibali, Mafuta ya mawese. Kama kawaida Jeshi letu (ambalo kwa mujibu wa Waziri wake, wengi wao ni failures) hawakumuumiza kichwa Wala kutumia busara, wakaitisha Press na kumsulubu mwekezaji mzawa aliyekua anatafuta ada za watoto wake kwa njia Halali.

Mungu akitaka kukupa kitu sometimes anakupitisha Kwenye majaribio magumu sana, Police bila kujua kuwa kwa kuitisha Press walikua wanamsaidia kumpiga chura Teke. Leo ndugu Zitto alipost Twitter akimuonba Waziri wa Kilimo Husein Bashe kumsaidia mwekezaji mzawa huyu kujua hatua stahiki za kuboresha kazi yake na hatimae Bashe ameripoti kuwa ameshachukua hatua.

Jambo hili linastahili pongezi sana maana ni Watanzania wengi sana wanaumizwa na Hawa Watawala wadogo wanaojiita miungu Watu wakiongozwa na Jeshi la Polisi, Watendaji, na maafisa wengine wa SERIKALI.

---

Ujumbe wa Zitto Kabwe

Wananchi wanatafuta njia zao za kujipatia kipato. Bwana Halifa Issa anapaswa kusaidiwa kuonyeshwa njia za vibali na sio kukamatwa. Waziri wa Kilimo ndugu @HusseinBashe na Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni kemeeni mambo haya. Huyu anafanya value addition. Support him

Majibu ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Nashukuru kwa Taarifa hii nimewasiliana na Mh DC wa kibaha nimemuomba amtafute huyu mwananchi na kumsaidia kupitia SIDO na wizara ya kilimo tuna promote “Value addition” through backyard processing hana tofauti na wale wa alizeti wanaouza Barabarani ni Jukumu letu kuwasaidia

CHANZO CHA SAKATA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Halifa Issa (42) mkazi wa Kongowe Wilayani Kibaha kwa kosa la kumiliki na kuendesha kiwanda bubu cha kuchakata mafuta ya mawese bila ya kuwa na kibali kinyume na sheria.
View attachment 2087500View attachment 2087501View attachment 2087502

View attachment 2086623
View attachment 2086625
Nashukuru kwa Taarifa hii nimewasiliana na Mh DC wa kibaha nimemuomba amtafute huyu mwananchi na kumsaidia kupitia SIDO na wizara ya kilimo tuna promote “Value addition” through backyard processing hana tofauti na wale wa alizeti wanaouza Barabarani ni Jukumu letu kuwasaidia
 
Duh kumbe nabishana na kitufe cha Mpapure
Naomba niambie kosa la polisi hapo ni nini?

Naomba kujua ni hatua gani zilitakuwa kuchukuliwa na ni chombo gani kilikuwa na jukumu la kufichua?

Je, huyo mtu alivunja sheria au hakuvunja?
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Jukumu la polisi kulinda mali na raia wake hayo mengine ya TBS na TRA
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Mafuta ya Mawese yanayouzwa Kigoma yanakaguliwa na nani? Mafuta ya alizeti vijijini yanakaguliwa na nani? Kutetea upopoma wa Polisi unahitaji kujitoa ufahamu kama ulivyofanya wewe!
 
Viwanda vya namna hiyo mbona kule kyela viko vingi sana halafu kwani navyo vin atakuwa kusajiliwa!! vinaendeshwa locally kabisa.. ni viwanda vidogo ambavyo vinaendeshwa kifamilia kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi...
 
Kama kuna watu ambao nilikua sielewi ni kwanini hawapewi UWAZIRI ni dogo huyu wa Nzega; namkubali sana Hussein Bashe, huyu katokea familia za kibiashara au kikulima ambaye hadi ukubwani ka practice aliojifunza utotoni. Namkubali sana Bashe, wengine wamesoma biashara lakini hatuoni elimu zao wakiwa maofisini, Bashe anaonesha elimu yake. Hongera sana, huyu jamaa hata akiwa rais kwangu naona sawa tu, ni mtu na nusu
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Mafuta ya alizet yanayo kamuliwa huku mitaani yanakaguliwa na TBS ?
 
Back
Top Bottom