Kukamatwa kwa Dkt. Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA: Maoni ya Dkt. Slaa | Page 19 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukamatwa kwa Dkt. Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA: Maoni ya Dkt. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dr Willibrod Slaa, Jul 17, 2017.

 1. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu Watanzania,

  Nimesoma kwa umakini "Taarifa" ya kukamatwa na kupelekwa Kituoni Katibu Mkuu wa Chadema na Viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na Kanda, kule Mbamba Bay, wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz. Mara kadhaa viongozi wa vyama mbali mbali pia wamekamatwa. Nimeshindwa kuelewa hasa tatizo la Msingi ni nini kwa kuwa Taarifa zinatolewa kwenye mitandao ya Jamii ki ushabiki zaidi. Hivyo mtu yeyote makini mwenye nia ya kulisaidia Taifa au kwa kushauri au kukemea anashindwa kwa kuwa " facts za msingi" haziwekwi wala kujadiliwa; wala na mtoa " thread/post au hata na wachangiaji. Namshukuru Mkurugenzi Kibatala, Wakili Msomi Mallya na wasaidizi wake mara kadhaa wamejaribu kutoa ufafanuzi katika hatua ya kesi lakini bila facts za matukio. Ni wazi katika hatua hiyo siyo jukumu lao kutoa facts kwa kuwa itaharibu kesi yao.

  Hata hivyo, baada ya kusoma mara kadhaa Taarifa ya matukio haya nimepaswa kurejea Political Parties Act, ( RE 2002) na Kanuni zake zote.

  1) Kimsingi, Watu wengi wanaamini kuwa Vyama vya siasa viko huru kufanya Mikutano ya ndani bila kutoa " Taarifa" ( Notice) Taarifa kwa Mamlaka husika ya Police katika eneo. Kifungu cha 11 (1-7) chahusika. Hii ni imani iliyojengwa visivyo, na utaratibu huu usipofuatwa wahusika hulalamika kuwa wanakandamizwa na kunyimwa haki za kidemokrasia na yote yanayoendana na hayo.

  Ili sisi tusioegemea upande wa Chama chochote, bali ni Wapenzi wa Taifa na kwa Taifa lolote katika ulimwengu wa leo vyama imara ni muhimu kwa maendeleo ya Kiuchumi na kisiasa. Ninaomba mwenye facts za matukio haya atuwekee ili tuweze kujadili with " objective and unbiased observations". Ebu tuachane na kauli zisizojengwa katika misingi ya kisheria kuwa " mikutano ya ndani haihitaji utoaji wa Taarifa". Ni kweli Mikutano ya Vyama vya siasa iwe ya nje au ya ndani haihitaji " Kibali cha yeyote wakiwemo Polisi ( Hukumu ya Mahakama Kuu).

  2. Pamoja na maelezo hayo kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa niliyotaja hapo Juu, mamlaka ya Polisi katika kudhibiti vyama vya siasa yapo pale pale iwapo utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na utaratibu uliowekwa na Sheria na Kanuni haukufuatwa. Utaratibu huo ni pamoja na kutoa " Notice" ( Taarifa) kwa Mamlaka husika ya Polisi katika eneo husika.

  a) Iwapo utaratibu wa kutoa Taarifa umefuatwa, Mamlaka ya Polisi hayawezi kukataza mkutano ulioombwa ( wa ndani au wa nje) isipokuwa kwa sababu zilizotajwa ndani ya Sheria.

  b) Taarifa za Ki-inteligensia au kugongana mikutano ya vyama ni sababu mojawapo ya mamlaka husika kuzuia mkutano uliotolewa Taarifa. Lakini Mamlaka hiyo inatakiwa kutoa siku/ muda mwingine au hata eneo lingine/ uwanja mwingine Mkutano huo unapotakiwa kufanyika. Hili ni hitaji la kisheria na siyo hisani ya mtu au kiongozi yeyote,

  3) Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vya Siasa vina haki ya kufanya mikutano ya kisasa, ya ndani na ya hadhara kwa lengo la kutafuta wanachama. Haina mantiki kuwa na "ndoa" ambayo wana ndoa hao wanawekewa masharti wasipate watoto kwa utaratibu ulioko ndani ya masharti ya Taratibu zilizoko katika Imani iliyowaunganisha katika ndoa hiyo. Kufanya hivyo ni kumaliza kizazi cha wana ndoa hao. Mimi siamini na sijaona mahali popote "Decree" ( Amri ya Rais) inayozuia Mikutano ya vyama ya nje wala ya ndani. Aliyeiona aniwekee humu jukwaani, Hivyo siamini kabisa kama kuna Katazo la Rais, ukiacha matamko ya kisiasa. Kauli ya Rais si sheria na haiwezi kuvunja Sheria iliyotungwa na Bunge ( Sheria na 5 ( RE 2002 ni sheria halali iliyotungwa na Bunge). Ninaamini kabisa kama kuna amri yeyote ya Rais, chama makini kingeli " challenge" amri hiyo chini ya vipengele vya sheria vya " Prerogative Orders za Certiorari, Prohibimus na Mandamus". Wanasheria wanajua vizuri matumizi ya sheria hizo katika kudhibiti matumizi mabovu ya mamlaka ya kuiongozi yeyote. Hivyo, tusitafute majibu mepesi katika " udikteta". Ni muda mwafaka sasa kutafuta majibu sahihi penginepo.

  4) Ni wazi kabisa, na nimemsikia Waziri wa Mambo ya ndani akitamka mara kadhaa kuwa mikutano ya Vyama ( ya hadhara na ya ndani ) haijapigwa marufuku alimradi utaratibu unafuatwa. Ni kwa msingi huu, ningependa sasa wapenzi wa vyama kuanza kubana viongozi wao kujua kama kweli " Taratibu" zote zilizowekwa na sheria zimefuatwa katika maandalizi ya mikutano ya vyama vya siasa. Tukumbuke Sheria yetu ya Vyama vya Siasa ni ya 1992 ( RE -as amended 2002) na Kanuni zake na tukumbuke Sheria inayoongoza Jeshi la Polisi ni za 1959 ( kama sikosei- sijacheki- na marekebisho madogo madogo kadhaa yakiwemo ya 2002). Hivyo Rais aliyeko madarakani kwa kutambua uwepo wa sheria hizo na kuzisimamia kama alivyoapa kusimamia Katiba na sheria hawezi kulaumiwa. Tangu ameingia madarakani siku takriban 600 zilizopita Rais aliyepo chini yake hapajatungwa sheria yeyote ya kudhibiti vyama na wala hakuna marekebisho yaliyofanyika, labda kama yamenipita pembeni, basi nielimishwe.. Katika hali hiyo tusipende kutafuta majibu mepesi kishabiki bila kufanya utafiti wa kina wa Tatizo linalosibu Taifa na Demokrasia yetu.

  5) Ni kweli Pia kuwa Polisi kwa kutumia Sheria za zamani zisizoendana na wakati, na bila waendesha Kesi wa Serikali ( kama ilivyo desturi katika kesi nyingi) kufanya maandalizi mazuri kesi nyingi zinazofunguliwa chini ya kinachoitwa kesi za " uchochezi" ( ambazo mimi mwenyewe kama Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama nilifunguliwa) au hasiendelei, au hatimaye hushindwa mahakamani kwa kukosa maandalizi hafifu ya Prosecutors au kwa kesi zenyewe au ukamataji kukosa misingi ya kijinai katika mazingira halisi ya leo. Ni wazi kesi hizi huchafua siyo tu jina la Serikali iliyoko madarakani bali pia sifa nzuri ya Taifa letu. Ni muhimu Maofisa Polisi kutimiza majukumu yao kwa umakini mkubwa na uangalifu mkubwa, na hasa kufuata misingi ya kisheria na kulinda Sheria za nchi bila kufanya mambo kwa kumpendeza mtu yeyote awaye. Taifa ni letu sote, mambo yakiharibika, sote tutaumia pamoja na mamlaka zenyewe za polisi, kwani leo uko kwenye madaraka kesho atakuwepo mwingine.

  6) Maelezo kuwa Chama Tawala kinafanya "Mikutano" ( ya ndani au ya nje) haiwezi kuwa hoja yenye nguvu. Kwani kama " wametimiza hitaji la " Notice" inayohitajika kisheria kama utaratibu wa kisheria unavyotaka lazima wapige "mbiu" au wawatangazie. Nani kafanya utafiti kwenye ma faili ya mamlaka husika kuwa "hawakufuata" utaratibu wa kisheria. Hii ni hoja dhaifu sana kuhalalisha "kutotafakari na kufanya utafiti" katika wa kina.

  Nimalizie tu kwa kusema kuwa, inauma kila siku kuona viongozi wa vyama wakikamatwa, na baada ya muda kuachiwa mahakamani. Ni dhahiri kuna dosari mahali. Au waliokamata hawakuwa makini, au walikuwa wakitaka kumpendeza au wanajipendekeza kwa malengo wanayojua wenyewe. Au kama nilivyoeleza Waendesha Mashtaka wa Serikali, DPP na wasaidizi wake wakiwemo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawajiandai vizuri.

  Kwa kumalizia nirudie tena kuwa wakati ufike sasa Wapenzi wa Vyama na wapenda demokrasia kwa ujumla tusipende sana kujadili mambo kwa ushabiki bali tuanze kuwa na "Critical analysis" ya hali inayokabili demokrasia yetu na kuanza kuhoji viongozi wetu wa vyama. Viongozi wawe wazi kama wamefuata Taratibu za kisheria au wamezoea kufanya mambo kwa " mazoea tu". Hakuna mahali popote sheria inapotamka kuwa "Mikutano ya ndani ya Vyama" haihitaji " Notice". Wala Mamlaka ya Polisi hasa vifungu vya 43, 44 etc vya Police Ordinance, ( kama sijakosea) havijarekebishwa wala kuondolewa, hivyo vikitumika tusilalamike, bali tuwalalamikie viongozi wetu kwa kutokuwa " Proactive" vifungu hivyo vilivyotungwa wakati wa ukoloni vifanyiwe marekebisho ya msingi ili demokrasia ya kweli iweze kujenga msingi katika Taifa letu. Wanasheria wa vyama ningelipenda wawasaidie wapenzi wa vyama katika kutoa elimu ya msingi, lakini pia kuwashauri vizuri pia viongozi badala ya kusubiri " kesi mahakamani".

  Nawasilisha.
   
 2. popbwinyo

  popbwinyo JF-Expert Member

  #361
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 3,384
  Likes Received: 2,141
  Trophy Points: 280
  Mm siyo Dr ila nimegundua kinachomsumbua Dr,hivyo kwa hili nimemzidi Dr ufahamu,
  Nlichokiona na kinachokusumbua Dr ni msukumo wa ndani wa kutaka watu wakufahamu km hauna chama,ndo mana hata fafanuzi yako hauna tofauti na refa anaeto penati kwa simba halafu anatafuta red card ili kuequalise kosa,
  Siku ukiacha kuamini kuwa ulidhurumiwa utakuwa mtu bora sana ambae kila uongeacho kitaeleweka
   
 3. popbwinyo

  popbwinyo JF-Expert Member

  #362
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 3,384
  Likes Received: 2,141
  Trophy Points: 280
  Hilo swali la mstari wa kwanza limenibariki sana,na nnatmni Dr ajirewind kifikra akumbuke hyo
   
 4. popbwinyo

  popbwinyo JF-Expert Member

  #363
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 3,384
  Likes Received: 2,141
  Trophy Points: 280
  Hata aloandika(Dr)nae anaweza kuwa kaandika kishabiki,ushabiki si wa cdm na ccm hata kushabikia kununulika nao ni ushabiki,
  Hata kushabikia ukweli ni ushabiki nk nk
   
 5. Gerasmus

  Gerasmus JF-Expert Member

  #364
  Jul 17, 2017
  Joined: May 23, 2016
  Messages: 381
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 80
  Mtu aliyeyakimbia makazi yake kwa sbb za kiusalama na kuomba ukimbizi ughaibuni hawezi kuelewa yanayoendelea huku tuliko....busara ni "kukaa kimya"
   
 6. ngolyongo

  ngolyongo Member

  #365
  Jul 17, 2017
  Joined: May 23, 2017
  Messages: 97
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 25
 7. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #366
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23,517
  Likes Received: 19,740
  Trophy Points: 280
  Mzee alipewa bank slip ya bilioni 2,alipotaka kudraw akakuta milioni 2! Akaambiwa matatizo ya mtandao,lakini atawezeshwa Canada,hana ujanja.wanaume wameumbwa kwa mateso
   
 8. Pancras Suday

  Pancras Suday Verified User

  #367
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,293
  Likes Received: 1,374
  Trophy Points: 280
  Unafikiri huko kwenye mitandao ndo wapo salama!?

  Sent from my iPhone 6s
   
 9. Nnangale

  Nnangale JF-Expert Member

  #368
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 20, 2013
  Messages: 1,448
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  hayuko peke yake waambie wainjoi maisha kwa biashara waliyofanya.
   
 10. More problems

  More problems JF-Expert Member

  #369
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 26, 2017
  Messages: 377
  Likes Received: 190
  Trophy Points: 60
  So ulistafu siasa !??
  Au umerudi kama rafiki yako!?
  Una uhakika gani kama huwa hawaombi vibali!?
  Na vip iwapo sisiemu wanaomba wanapewa ila wengine hawapewi!?
  Kwann wawaachie bila hukumu wenye makosa!??

  Mzee kaa zako ukimbizini utulie tuachie malofa na wapumbavu mateso yetu.
   
 11. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #370
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,508
  Likes Received: 6,431
  Trophy Points: 280
  Haya, sawa.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #371
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,280
  Likes Received: 7,466
  Trophy Points: 280
  Dr. Willibrod Slaa

  Ulitahadharisha kuhusu uzi kutokuwa wa 'ushabiki'. Tulikueleza uweke akiba ya maneno
  Uzi wako kwa ujumla ulilenga kueleza wananchi wanalalamikia bila kujua 'facts'.

  Kwa ufupi uzi ulilenga vitu vitatu, kwanza kulaumu vyama na viongozi bila wewe kuwa na facts, pili kulaumu wanachama wanaolalamika bila wewe kuwa na facts, na muhimu zaidi kusaidia Polisi kujenga hoja kwa vifungu ulivyosema ili hoja itumike endapo Polisi hawakujua hilo, I mean ulikuwa unawatonya!

  Kwa taarifa yako wameachiwa bila mashtaka. Hiki ndicho nilieleza bandiko la awali kabisa
  Nilikueleza tatizo si taratibu kufuatwa, ni matumizi mabaya ya nguvu na madaraka

  Nilikueleza, huwezi ukaongelea utaratibu wa kuomba vibali kana kwamba kila jambo lipo sawa
  Huwezi ukafanya tafiti katika mazingira yenye factor nyingine nje unazotafiti
  Huwezi kufuata utaratibu kukiwa na sheria kandamizi kama za 48hr

  Na nikaueleza huwezi kufuata taratibu eneo lisilo na utaratibu

  Nakuomba urudi tujadiliane bila ushabiki.
  Mada yako ni nzuri kwasababu kuna uhalisia wa tukio

  Dr Slaa rejea tafadhali, hata hivyo ni ombi tu.

  Sisi tutaendelea kujadili mada yako kikamilifu tukienda mbali baada ya kupata 'facts'
   
 13. uvugizi

  uvugizi JF-Expert Member

  #372
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 294
  Trophy Points: 180
  Maelezo mengi , hakuna cha Maana hapa Hanna cha sheria wala kipengele swala ni wasifurukute wapinzani kama Rwanda .
   
 14. young solicitor

  young solicitor JF-Expert Member

  #373
  Jul 18, 2017
  Joined: Dec 26, 2015
  Messages: 580
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  sasa unajitofautishaje na mijitu inayoamini itatawala hii.nchi milele au wale wanaodai kuongeza muda wa utawala
   
 15. MAGALEMWA

  MAGALEMWA JF-Expert Member

  #374
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 8, 2015
  Messages: 4,105
  Likes Received: 2,329
  Trophy Points: 280
  dr. slaa my friend unataka ushahidi gani wa udikteta zaidi ya kauli ya rais wako kuwa siasa hadi 2020?

  Kama huuoni udikteta na mikakati mibovu ya ukandamizaji ebu tafakari na ufafanue haya:-
  1. Kwa hoja yako hapo juu kuwa "kushindwa kwa serikalu na kesi za uchochezi kunadhalilisha taifa letu" fafanua kwa nini watawala wasiwe sehemu ya udhalilishaji wa taifa?

  2. Nakushangaa kusema chama tawala kinazingatia taratibu. Labda umesahau kauli yako "kuwa ccm bila polisi ni wepesi"

  3. Hoja yako inatiwa na mashaka ya kuhamishiwa CANADA kwa manufaa ya watawala. Unazuga na utaifa huku unajua chanzo cha gharama ya kukufikisha huko uliko si utaifa.

  4. Tuache tupambane hivyo hivyo usituongezee machungu.
   
 16. obell

  obell Member

  #375
  Jul 18, 2017
  Joined: May 31, 2016
  Messages: 48
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Running away from problems is not the best way to sort them out. Doctor you're already busted out and silence is golden. You are hypocrite and you deserve to be smashed by any elite. You accepted the leadership of your wife now reap the fruits of thy weakness!!

  Sent from my Vodafone 785 using JamiiForums mobile app
   
 17. J

  JOHNKEKE JF-Expert Member

  #376
  Jul 18, 2017
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 80
  Duh. Kweli kazi ipo. Dr Slaa kutoa hoja nzito tena za kuwasaidia upinzani, lakini hilo hawalioni wamebaki kudhiaki, kutukana na wachache kuuliza maswali ambayo yameshajibika kwenye maelezo ya Dr.
  Kweli uelewa wa watanzania huko chini sana. Ndo maana kila wimbo mnaoimbishwa mnaitikia tu bila kufikiri.
   
 18. c

  chach JF-Expert Member

  #377
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  A narudi kama lipumba kudai u katibu mkuu

  Sent using Jamii Forums mobile app
   
 19. k

  konyola JF-Expert Member

  #378
  Jul 18, 2017
  Joined: Dec 13, 2016
  Messages: 720
  Likes Received: 855
  Trophy Points: 180
  DOKITA nakuona unakula kuku kwa mrija na mama Musumbuzi anakubonyeza bonyeza kengele ya bomani ukifaidi mafao ya kazi kubwa ya chama cha makinikia wakakusahaulisha vipigo walivyowahi kukupa leo unazungumzia siasa za tz kama za SCANDINAVIAN COUNTIES haya DOKITA ukimaliza kale mzigo ulale
   
 20. i

  ibesa mau JF-Expert Member

  #379
  Jul 18, 2017
  Joined: Sep 17, 2015
  Messages: 1,543
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Naomba nikuulize swali moja tu Dr. Hivi ni sheria gani inatumika kuwakamata wapinzani na kuwaweka mahabusu pasipo kuwafikisha mahakamani.
   
 21. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #380
  Jul 18, 2017
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,916
  Likes Received: 1,189
  Trophy Points: 280
  Vyama vya siasa vina Haki ya kikatiba ya kufanya mikutano ya nje/hadhara ili kujipatia Wanachama. Haina Mantiki kuwa na Ndoa halafu mnakatazwa kuzaa Watoto. Dr Slaa bila Kijiba cha Roho ulicho nacho juu ya Wapinzani ebu fafanua hii kauli.
   
Tags:
Loading...