Kukamatwa kwa Dkt. Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA: Maoni ya Dkt. Slaa | Page 18 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukamatwa kwa Dkt. Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA: Maoni ya Dkt. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dr Willibrod Slaa, Jul 17, 2017.

 1. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu Watanzania,

  Nimesoma kwa umakini "Taarifa" ya kukamatwa na kupelekwa Kituoni Katibu Mkuu wa Chadema na Viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na Kanda, kule Mbamba Bay, wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz. Mara kadhaa viongozi wa vyama mbali mbali pia wamekamatwa. Nimeshindwa kuelewa hasa tatizo la Msingi ni nini kwa kuwa Taarifa zinatolewa kwenye mitandao ya Jamii ki ushabiki zaidi. Hivyo mtu yeyote makini mwenye nia ya kulisaidia Taifa au kwa kushauri au kukemea anashindwa kwa kuwa " facts za msingi" haziwekwi wala kujadiliwa; wala na mtoa " thread/post au hata na wachangiaji. Namshukuru Mkurugenzi Kibatala, Wakili Msomi Mallya na wasaidizi wake mara kadhaa wamejaribu kutoa ufafanuzi katika hatua ya kesi lakini bila facts za matukio. Ni wazi katika hatua hiyo siyo jukumu lao kutoa facts kwa kuwa itaharibu kesi yao.

  Hata hivyo, baada ya kusoma mara kadhaa Taarifa ya matukio haya nimepaswa kurejea Political Parties Act, ( RE 2002) na Kanuni zake zote.

  1) Kimsingi, Watu wengi wanaamini kuwa Vyama vya siasa viko huru kufanya Mikutano ya ndani bila kutoa " Taarifa" ( Notice) Taarifa kwa Mamlaka husika ya Police katika eneo. Kifungu cha 11 (1-7) chahusika. Hii ni imani iliyojengwa visivyo, na utaratibu huu usipofuatwa wahusika hulalamika kuwa wanakandamizwa na kunyimwa haki za kidemokrasia na yote yanayoendana na hayo.

  Ili sisi tusioegemea upande wa Chama chochote, bali ni Wapenzi wa Taifa na kwa Taifa lolote katika ulimwengu wa leo vyama imara ni muhimu kwa maendeleo ya Kiuchumi na kisiasa. Ninaomba mwenye facts za matukio haya atuwekee ili tuweze kujadili with " objective and unbiased observations". Ebu tuachane na kauli zisizojengwa katika misingi ya kisheria kuwa " mikutano ya ndani haihitaji utoaji wa Taarifa". Ni kweli Mikutano ya Vyama vya siasa iwe ya nje au ya ndani haihitaji " Kibali cha yeyote wakiwemo Polisi ( Hukumu ya Mahakama Kuu).

  2. Pamoja na maelezo hayo kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa niliyotaja hapo Juu, mamlaka ya Polisi katika kudhibiti vyama vya siasa yapo pale pale iwapo utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na utaratibu uliowekwa na Sheria na Kanuni haukufuatwa. Utaratibu huo ni pamoja na kutoa " Notice" ( Taarifa) kwa Mamlaka husika ya Polisi katika eneo husika.

  a) Iwapo utaratibu wa kutoa Taarifa umefuatwa, Mamlaka ya Polisi hayawezi kukataza mkutano ulioombwa ( wa ndani au wa nje) isipokuwa kwa sababu zilizotajwa ndani ya Sheria.

  b) Taarifa za Ki-inteligensia au kugongana mikutano ya vyama ni sababu mojawapo ya mamlaka husika kuzuia mkutano uliotolewa Taarifa. Lakini Mamlaka hiyo inatakiwa kutoa siku/ muda mwingine au hata eneo lingine/ uwanja mwingine Mkutano huo unapotakiwa kufanyika. Hili ni hitaji la kisheria na siyo hisani ya mtu au kiongozi yeyote,

  3) Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vya Siasa vina haki ya kufanya mikutano ya kisasa, ya ndani na ya hadhara kwa lengo la kutafuta wanachama. Haina mantiki kuwa na "ndoa" ambayo wana ndoa hao wanawekewa masharti wasipate watoto kwa utaratibu ulioko ndani ya masharti ya Taratibu zilizoko katika Imani iliyowaunganisha katika ndoa hiyo. Kufanya hivyo ni kumaliza kizazi cha wana ndoa hao. Mimi siamini na sijaona mahali popote "Decree" ( Amri ya Rais) inayozuia Mikutano ya vyama ya nje wala ya ndani. Aliyeiona aniwekee humu jukwaani, Hivyo siamini kabisa kama kuna Katazo la Rais, ukiacha matamko ya kisiasa. Kauli ya Rais si sheria na haiwezi kuvunja Sheria iliyotungwa na Bunge ( Sheria na 5 ( RE 2002 ni sheria halali iliyotungwa na Bunge). Ninaamini kabisa kama kuna amri yeyote ya Rais, chama makini kingeli " challenge" amri hiyo chini ya vipengele vya sheria vya " Prerogative Orders za Certiorari, Prohibimus na Mandamus". Wanasheria wanajua vizuri matumizi ya sheria hizo katika kudhibiti matumizi mabovu ya mamlaka ya kuiongozi yeyote. Hivyo, tusitafute majibu mepesi katika " udikteta". Ni muda mwafaka sasa kutafuta majibu sahihi penginepo.

  4) Ni wazi kabisa, na nimemsikia Waziri wa Mambo ya ndani akitamka mara kadhaa kuwa mikutano ya Vyama ( ya hadhara na ya ndani ) haijapigwa marufuku alimradi utaratibu unafuatwa. Ni kwa msingi huu, ningependa sasa wapenzi wa vyama kuanza kubana viongozi wao kujua kama kweli " Taratibu" zote zilizowekwa na sheria zimefuatwa katika maandalizi ya mikutano ya vyama vya siasa. Tukumbuke Sheria yetu ya Vyama vya Siasa ni ya 1992 ( RE -as amended 2002) na Kanuni zake na tukumbuke Sheria inayoongoza Jeshi la Polisi ni za 1959 ( kama sikosei- sijacheki- na marekebisho madogo madogo kadhaa yakiwemo ya 2002). Hivyo Rais aliyeko madarakani kwa kutambua uwepo wa sheria hizo na kuzisimamia kama alivyoapa kusimamia Katiba na sheria hawezi kulaumiwa. Tangu ameingia madarakani siku takriban 600 zilizopita Rais aliyepo chini yake hapajatungwa sheria yeyote ya kudhibiti vyama na wala hakuna marekebisho yaliyofanyika, labda kama yamenipita pembeni, basi nielimishwe.. Katika hali hiyo tusipende kutafuta majibu mepesi kishabiki bila kufanya utafiti wa kina wa Tatizo linalosibu Taifa na Demokrasia yetu.

  5) Ni kweli Pia kuwa Polisi kwa kutumia Sheria za zamani zisizoendana na wakati, na bila waendesha Kesi wa Serikali ( kama ilivyo desturi katika kesi nyingi) kufanya maandalizi mazuri kesi nyingi zinazofunguliwa chini ya kinachoitwa kesi za " uchochezi" ( ambazo mimi mwenyewe kama Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama nilifunguliwa) au hasiendelei, au hatimaye hushindwa mahakamani kwa kukosa maandalizi hafifu ya Prosecutors au kwa kesi zenyewe au ukamataji kukosa misingi ya kijinai katika mazingira halisi ya leo. Ni wazi kesi hizi huchafua siyo tu jina la Serikali iliyoko madarakani bali pia sifa nzuri ya Taifa letu. Ni muhimu Maofisa Polisi kutimiza majukumu yao kwa umakini mkubwa na uangalifu mkubwa, na hasa kufuata misingi ya kisheria na kulinda Sheria za nchi bila kufanya mambo kwa kumpendeza mtu yeyote awaye. Taifa ni letu sote, mambo yakiharibika, sote tutaumia pamoja na mamlaka zenyewe za polisi, kwani leo uko kwenye madaraka kesho atakuwepo mwingine.

  6) Maelezo kuwa Chama Tawala kinafanya "Mikutano" ( ya ndani au ya nje) haiwezi kuwa hoja yenye nguvu. Kwani kama " wametimiza hitaji la " Notice" inayohitajika kisheria kama utaratibu wa kisheria unavyotaka lazima wapige "mbiu" au wawatangazie. Nani kafanya utafiti kwenye ma faili ya mamlaka husika kuwa "hawakufuata" utaratibu wa kisheria. Hii ni hoja dhaifu sana kuhalalisha "kutotafakari na kufanya utafiti" katika wa kina.

  Nimalizie tu kwa kusema kuwa, inauma kila siku kuona viongozi wa vyama wakikamatwa, na baada ya muda kuachiwa mahakamani. Ni dhahiri kuna dosari mahali. Au waliokamata hawakuwa makini, au walikuwa wakitaka kumpendeza au wanajipendekeza kwa malengo wanayojua wenyewe. Au kama nilivyoeleza Waendesha Mashtaka wa Serikali, DPP na wasaidizi wake wakiwemo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawajiandai vizuri.

  Kwa kumalizia nirudie tena kuwa wakati ufike sasa Wapenzi wa Vyama na wapenda demokrasia kwa ujumla tusipende sana kujadili mambo kwa ushabiki bali tuanze kuwa na "Critical analysis" ya hali inayokabili demokrasia yetu na kuanza kuhoji viongozi wetu wa vyama. Viongozi wawe wazi kama wamefuata Taratibu za kisheria au wamezoea kufanya mambo kwa " mazoea tu". Hakuna mahali popote sheria inapotamka kuwa "Mikutano ya ndani ya Vyama" haihitaji " Notice". Wala Mamlaka ya Polisi hasa vifungu vya 43, 44 etc vya Police Ordinance, ( kama sijakosea) havijarekebishwa wala kuondolewa, hivyo vikitumika tusilalamike, bali tuwalalamikie viongozi wetu kwa kutokuwa " Proactive" vifungu hivyo vilivyotungwa wakati wa ukoloni vifanyiwe marekebisho ya msingi ili demokrasia ya kweli iweze kujenga msingi katika Taifa letu. Wanasheria wa vyama ningelipenda wawasaidie wapenzi wa vyama katika kutoa elimu ya msingi, lakini pia kuwashauri vizuri pia viongozi badala ya kusubiri " kesi mahakamani".

  Nawasilisha.
   
 2. rashidikurwa

  rashidikurwa Member

  #341
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 16, 2017
  Messages: 34
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
  Hakuna haki bila wajibu, wajibu wa kila chama ni kutoa notice kabla hakijaitisha mkutano ama kikao chchote, Sasa wengine wanaamua kujiitishia vikao tu bila kufuata sheria na taratibu!! Utafikiri ni kikao cha Baba na watoto wake!!!

  Ni lazima kila kiongozi wa chama cha siasa akumbuke kuwa hii ni nchi inayoongozwa na viongozi waliotokana na Umma, kwahiyo ni lazima waheshimu mamlaka, na kama hawawezi wahame nchi kwa mda hadi pale watakapoweza kutii mamlaka ndipo warudi, hatubembelezani sasa hivi hilo wakae wakilijua.
   
 3. K

  Kihava JF-Expert Member

  #342
  Jul 17, 2017
  Joined: May 23, 2016
  Messages: 2,095
  Likes Received: 1,566
  Trophy Points: 280
  Yeye kwanini ule mkutano wake wa Serena Hotel alitokea mlango wa uani?

  Kwanini alipewa ulinzi wa kufa mtu wakati anahutubia pale Serena Hotel akimpigia kampeni mgombea wake ampendaye, ambaye mwanzo alituambia ndiye dalali wa nyumba zetu za serikali?
   
 4. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #343
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,948
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
  Dr.Slaa,Kwa kumalizia nirudie tena kuwa wakati ufike sasa Wapenzi wa Vyama na wapenda demokrasia kwa ujumla tusipende sana kujadili mambo kwa ushabiki bali tuanze kuwa na "Critical analysis" ya hali inayokabili demokrasia yetu na kuanza kuhoji viongozi wetu wa vyama
   
 5. B

  Babati JF-Expert Member

  #344
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 31,836
  Likes Received: 25,112
  Trophy Points: 280
  Hatimaye Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji na viongozi hao 8 wakiwemo wabunge wawili, wameachiwa muda huu majira ya saa 5 asubuhi. Jana tulizitaka mamlaka zilizohusika kutoa amri ya kuwakamata zitoe amri ya kuwaachia huru mara moja kabla chama hakijatoa kauli nyingine kuhusu hatua zingine ambazo kingechukua kulinda sheria, uhuru na haki katika nchi

  Tutaendelea kuwajuza. Baadae saa 7 mchana Chama kitafanya press conference itakayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lisu.
   
 6. B

  Babati JF-Expert Member

  #345
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 7, 2014
  Messages: 31,836
  Likes Received: 25,112
  Trophy Points: 280
  Huyu babu anazeeka vibaya sana.
   
 7. n

  nijothemaster JF-Expert Member

  #346
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 2, 2015
  Messages: 324
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ....Haki ya kikatiba, sheria, mahakama, vibali, polisi, mamlaka, demokrasia, mikutano ya kisiasa........SIASA.....

  Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
   
 8. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #347
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 4,518
  Trophy Points: 280
  Mzee wetu ulaya kumemchosha, pensheni aliyopewa na Mwakyembe umeisha sasa amebakia nyumban anacheza na junior. Ameshasahau kuwa ameandamana sana mpaka yeye na mama mtoto wake wakala virungu na kuvuja damu. Sasa analaumu wahanga kama anavyofanya mghaibuni mwenzake mmoja.

  Nimkumbushe Mzee wetu kuwa 'it is always about the big picture'. Haya yanayotokea sasa ndo tunayopigania kila, sio ujio wa Lowassa. Kosa litakalomsuta maisha yake yote ni kuacha harakati kisa Lowassa kahamia Chadema. Akaona kuliko amuunge mkono mlutheri basi acha mbona imwagike.
   
 9. n

  nijothemaster JF-Expert Member

  #348
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 2, 2015
  Messages: 324
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Naomba kuuliza mkuu, nimikutano ya aina yoyote haihitaji ruhusa kutoka sehemu yoyote au ni ya kisiasa tu ndio haihitaji ruhusa?...

  Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
   
 10. R

  Richmak Member

  #349
  Jul 17, 2017
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Dr Slaa hakika naona umbali umeanza kuchukua nafasi yake (distance taking its toll).

  Pamoja na falsafa uliyotumia bado unaonekana uko mbali na uhalisia, makusudi au kwasababu za kutokuwepo kwa muda mrefu. Blaming the victims? Hukusikia kauli kali kutoka juu kuwa hataki kujaribiwa? We miss the true fighter in you.
   
 11. M

  Mdala Vangu Member

  #350
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 8, 2017
  Messages: 21
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 5
  Katibu Mkuu mstaafu wa CHADEMA Dr. Wilroad Slaa salaam!,

  Nimesoma thread yako nimeipenda sana hasa kwenye kukumbusha Sheria na utaratibu wa kuendesha siasa. Lakini kuhusu la kukamatwa Kwa Katibu Mkuu wa CHAD EMA Dr. Mashinji ni kwamba taarifa zilipelekwa polisi na waliridhia.

  Hadi siku ya tarehe 15.07.2017 yaani siku ambayo walikamatwa kulitokea mapokezi makubwa pale tulikuwa na magari manner na Pikipiki 10 zilizofungwa Bendera. Na tulimpokea eneo la Kilosa makao makuu ya wilaya ya Nyasa tukampeleka hotelini ili aweze kupumzika Kwa safari ndefu halafu muda wa mkutano ukifika ndipo twende kwenye ukumbi wa mkutano.

  Sasa wakati wa asubuhi tulifunga Bendera kwenye barabara inayoelekea ukumbi wa Mkutano. Lakini Mara baada ya katibu kumfikisha hotelini polisi waliaza kuja Kwa madereva wa Bodaboda ambapo hawakukuta hata mmoja mwenye Bendera ya chama kwani tulipofika tu hotelini tuliwaambia watawanyike lakini tukutane ukumbini SAA 8:00 mchana. Lakini haikutosha tutaona tena Polisi wanang'oa Bendera zote tulizokuwa tumezisimika pembeni mwa Barabara Kwa miti ya miazi.

  Tulipowauliza wakasema wamepewa agizo toka juu kwamba wazing'oe. Na baada ya hapo ndipo wakamkamata Zubeda Sakuru (Mb) na baada ya kufika ukumbini Wakati Katibu Mkuu anaongea walifika polisi na kuwakamata wengine waliokuwepo. Hii ndo picha
   
 12. M

  Mindi JF-Expert Member

  #351
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,550
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Huyu Slaa ni msaliti. Anzia pale alipojiondoa CHADEMA. kwanza ieleweke kwamba kuwa na maoni tofauti siyo tatizo. Angeweza tu kukaa pembeni na kuacha chama kiendelee kutekeleza kile ambacho yeye hakubaliani nacho. lakini angeheshimu uamuzi wa chama na kukaa kimya. lakini wapi! aligeuka kuwa chombo cha CCM, vyombo vitano vya TV vilimtangaza siku hiyo na alitumia nguvu zake zote kuiponda ponda CHADEMA. nadhani lengo lilikuwa kuimaliza kabisa, kwamba yeye ameondoka basi kusiwepo na chama tena. alishangaa na kuumia sana CHADEMA ilipoendelea kusonga mbele na pamoja na wenzake katika UKAWA, kujinyakulia ushindi wa kihistoria.

  Sasa njoo kwenye bandiko la leo. vitendo vya awamu hii kwa ujumla ni vya kuumaliza kabisa upinzani, na wala siyo kama ilivyokuwa enzi za awamu ya nne. kwa hiyo kitendo cha Slaa kuchukua vipisi vya matukio na kujenga hoja katika muktadha mzima, hiyo ni kashfa kubwa kwa msomi wa kiwango chake. Njaa mbaya sana
   
 13. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #352
  Jul 17, 2017
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,935
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  Muzee Slaa unaboa.
  Rudi basi bongo ujiunge na yule profesa wa buguruni. How wonderful: profesa na daktari combination.
   
 14. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #353
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,439
  Likes Received: 1,299
  Trophy Points: 280

  Mzee shikamoo.
  Naona Ulaya /Canada kunataka kukusahaulisha ya Bongo/Afrika. Ukafanyte utafiti kwenye makabrasha ya Vituo vya Polisi Bongo? Nadhani itapendeza ukaendelea kula bata bila kuiwazia Tanganyika.(Tanzania Bara). Huku ukimfundisha maadili ya kiafrika na Kiulaya ++ Bwana mdogo (Mrithi wako) Ni imani yangu tu.
   
 15. Mr Equalizer

  Mr Equalizer JF-Expert Member

  #354
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 14, 2013
  Messages: 544
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 180
  Mzee katika andiko lako ziko hoja kadhaa za msingi .Ila kwa upande mwingine pia umejitia upofu , umejifanya huyajui mazingira ya siasa za tanzania.
  Ni mara ngapi Police wametoa vibali vya mikutano halafu badae wanakuja kuivuruga?

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 16. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #355
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,787
  Likes Received: 6,660
  Trophy Points: 280
  Ndio huyu huyu alikuwaga rais wa mioyoni, au umesahau?
   
 17. Ilankunda1234

  Ilankunda1234 JF-Expert Member

  #356
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 28, 2015
  Messages: 3,646
  Likes Received: 2,817
  Trophy Points: 280
  Katika bandiko linalohusu siasa zabupinzani nimekuwa nikiona mtu pekee ambae unaweza ukomboa upinzani ni wewe. Sasa kwa mawazo haya' upinzani umekufa ni dhahili kabisa umeamua kuwa sisiem

  Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #357
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,943
  Likes Received: 15,476
  Trophy Points: 280
  Kazi ya moyo ni kusukuma damu.
   
 19. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #358
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,912
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Nilitaka Sana kumkumbusha hili. Iringa na kuuawa kwa Mwangosi ilikuwa katika harakati zake za kufungua matawi huko Nyololo.

  Leo anasema kitu tofauti kabisa.

  Sent from my TECNO-W5 using JamiiForums mobile app
   
 20. Ilankunda1234

  Ilankunda1234 JF-Expert Member

  #359
  Jul 17, 2017
  Joined: Dec 28, 2015
  Messages: 3,646
  Likes Received: 2,817
  Trophy Points: 280
  U zuri chadema washampata mgombea uraisi Miaka mitatu kabla ya uchaguzi inauma sanaaaaaaaaa

  Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
   
 21. s

  st44273 JF-Expert Member

  #360
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 3, 2013
  Messages: 329
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Duh! Kweli wewe ni lecturer, maswali yote uliyomwuliza ni ya msingi sana, sijui kama anaweza kuya attempt.
   
Tags:
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...