Kukamatwa kwa Dkt. Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA: Maoni ya Dkt. Slaa | Page 17 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukamatwa kwa Dkt. Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA: Maoni ya Dkt. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dr Willibrod Slaa, Jul 17, 2017.

 1. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #1
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Ndugu zangu Watanzania,

  Nimesoma kwa umakini "Taarifa" ya kukamatwa na kupelekwa Kituoni Katibu Mkuu wa Chadema na Viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na Kanda, kule Mbamba Bay, wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz. Mara kadhaa viongozi wa vyama mbali mbali pia wamekamatwa. Nimeshindwa kuelewa hasa tatizo la Msingi ni nini kwa kuwa Taarifa zinatolewa kwenye mitandao ya Jamii ki ushabiki zaidi. Hivyo mtu yeyote makini mwenye nia ya kulisaidia Taifa au kwa kushauri au kukemea anashindwa kwa kuwa " facts za msingi" haziwekwi wala kujadiliwa; wala na mtoa " thread/post au hata na wachangiaji. Namshukuru Mkurugenzi Kibatala, Wakili Msomi Mallya na wasaidizi wake mara kadhaa wamejaribu kutoa ufafanuzi katika hatua ya kesi lakini bila facts za matukio. Ni wazi katika hatua hiyo siyo jukumu lao kutoa facts kwa kuwa itaharibu kesi yao.

  Hata hivyo, baada ya kusoma mara kadhaa Taarifa ya matukio haya nimepaswa kurejea Political Parties Act, ( RE 2002) na Kanuni zake zote.

  1) Kimsingi, Watu wengi wanaamini kuwa Vyama vya siasa viko huru kufanya Mikutano ya ndani bila kutoa " Taarifa" ( Notice) Taarifa kwa Mamlaka husika ya Police katika eneo. Kifungu cha 11 (1-7) chahusika. Hii ni imani iliyojengwa visivyo, na utaratibu huu usipofuatwa wahusika hulalamika kuwa wanakandamizwa na kunyimwa haki za kidemokrasia na yote yanayoendana na hayo.

  Ili sisi tusioegemea upande wa Chama chochote, bali ni Wapenzi wa Taifa na kwa Taifa lolote katika ulimwengu wa leo vyama imara ni muhimu kwa maendeleo ya Kiuchumi na kisiasa. Ninaomba mwenye facts za matukio haya atuwekee ili tuweze kujadili with " objective and unbiased observations". Ebu tuachane na kauli zisizojengwa katika misingi ya kisheria kuwa " mikutano ya ndani haihitaji utoaji wa Taarifa". Ni kweli Mikutano ya Vyama vya siasa iwe ya nje au ya ndani haihitaji " Kibali cha yeyote wakiwemo Polisi ( Hukumu ya Mahakama Kuu).

  2. Pamoja na maelezo hayo kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa niliyotaja hapo Juu, mamlaka ya Polisi katika kudhibiti vyama vya siasa yapo pale pale iwapo utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na utaratibu uliowekwa na Sheria na Kanuni haukufuatwa. Utaratibu huo ni pamoja na kutoa " Notice" ( Taarifa) kwa Mamlaka husika ya Polisi katika eneo husika.

  a) Iwapo utaratibu wa kutoa Taarifa umefuatwa, Mamlaka ya Polisi hayawezi kukataza mkutano ulioombwa ( wa ndani au wa nje) isipokuwa kwa sababu zilizotajwa ndani ya Sheria.

  b) Taarifa za Ki-inteligensia au kugongana mikutano ya vyama ni sababu mojawapo ya mamlaka husika kuzuia mkutano uliotolewa Taarifa. Lakini Mamlaka hiyo inatakiwa kutoa siku/ muda mwingine au hata eneo lingine/ uwanja mwingine Mkutano huo unapotakiwa kufanyika. Hili ni hitaji la kisheria na siyo hisani ya mtu au kiongozi yeyote,

  3) Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vya Siasa vina haki ya kufanya mikutano ya kisasa, ya ndani na ya hadhara kwa lengo la kutafuta wanachama. Haina mantiki kuwa na "ndoa" ambayo wana ndoa hao wanawekewa masharti wasipate watoto kwa utaratibu ulioko ndani ya masharti ya Taratibu zilizoko katika Imani iliyowaunganisha katika ndoa hiyo. Kufanya hivyo ni kumaliza kizazi cha wana ndoa hao. Mimi siamini na sijaona mahali popote "Decree" ( Amri ya Rais) inayozuia Mikutano ya vyama ya nje wala ya ndani. Aliyeiona aniwekee humu jukwaani, Hivyo siamini kabisa kama kuna Katazo la Rais, ukiacha matamko ya kisiasa. Kauli ya Rais si sheria na haiwezi kuvunja Sheria iliyotungwa na Bunge ( Sheria na 5 ( RE 2002 ni sheria halali iliyotungwa na Bunge). Ninaamini kabisa kama kuna amri yeyote ya Rais, chama makini kingeli " challenge" amri hiyo chini ya vipengele vya sheria vya " Prerogative Orders za Certiorari, Prohibimus na Mandamus". Wanasheria wanajua vizuri matumizi ya sheria hizo katika kudhibiti matumizi mabovu ya mamlaka ya kuiongozi yeyote. Hivyo, tusitafute majibu mepesi katika " udikteta". Ni muda mwafaka sasa kutafuta majibu sahihi penginepo.

  4) Ni wazi kabisa, na nimemsikia Waziri wa Mambo ya ndani akitamka mara kadhaa kuwa mikutano ya Vyama ( ya hadhara na ya ndani ) haijapigwa marufuku alimradi utaratibu unafuatwa. Ni kwa msingi huu, ningependa sasa wapenzi wa vyama kuanza kubana viongozi wao kujua kama kweli " Taratibu" zote zilizowekwa na sheria zimefuatwa katika maandalizi ya mikutano ya vyama vya siasa. Tukumbuke Sheria yetu ya Vyama vya Siasa ni ya 1992 ( RE -as amended 2002) na Kanuni zake na tukumbuke Sheria inayoongoza Jeshi la Polisi ni za 1959 ( kama sikosei- sijacheki- na marekebisho madogo madogo kadhaa yakiwemo ya 2002). Hivyo Rais aliyeko madarakani kwa kutambua uwepo wa sheria hizo na kuzisimamia kama alivyoapa kusimamia Katiba na sheria hawezi kulaumiwa. Tangu ameingia madarakani siku takriban 600 zilizopita Rais aliyepo chini yake hapajatungwa sheria yeyote ya kudhibiti vyama na wala hakuna marekebisho yaliyofanyika, labda kama yamenipita pembeni, basi nielimishwe.. Katika hali hiyo tusipende kutafuta majibu mepesi kishabiki bila kufanya utafiti wa kina wa Tatizo linalosibu Taifa na Demokrasia yetu.

  5) Ni kweli Pia kuwa Polisi kwa kutumia Sheria za zamani zisizoendana na wakati, na bila waendesha Kesi wa Serikali ( kama ilivyo desturi katika kesi nyingi) kufanya maandalizi mazuri kesi nyingi zinazofunguliwa chini ya kinachoitwa kesi za " uchochezi" ( ambazo mimi mwenyewe kama Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama nilifunguliwa) au hasiendelei, au hatimaye hushindwa mahakamani kwa kukosa maandalizi hafifu ya Prosecutors au kwa kesi zenyewe au ukamataji kukosa misingi ya kijinai katika mazingira halisi ya leo. Ni wazi kesi hizi huchafua siyo tu jina la Serikali iliyoko madarakani bali pia sifa nzuri ya Taifa letu. Ni muhimu Maofisa Polisi kutimiza majukumu yao kwa umakini mkubwa na uangalifu mkubwa, na hasa kufuata misingi ya kisheria na kulinda Sheria za nchi bila kufanya mambo kwa kumpendeza mtu yeyote awaye. Taifa ni letu sote, mambo yakiharibika, sote tutaumia pamoja na mamlaka zenyewe za polisi, kwani leo uko kwenye madaraka kesho atakuwepo mwingine.

  6) Maelezo kuwa Chama Tawala kinafanya "Mikutano" ( ya ndani au ya nje) haiwezi kuwa hoja yenye nguvu. Kwani kama " wametimiza hitaji la " Notice" inayohitajika kisheria kama utaratibu wa kisheria unavyotaka lazima wapige "mbiu" au wawatangazie. Nani kafanya utafiti kwenye ma faili ya mamlaka husika kuwa "hawakufuata" utaratibu wa kisheria. Hii ni hoja dhaifu sana kuhalalisha "kutotafakari na kufanya utafiti" katika wa kina.

  Nimalizie tu kwa kusema kuwa, inauma kila siku kuona viongozi wa vyama wakikamatwa, na baada ya muda kuachiwa mahakamani. Ni dhahiri kuna dosari mahali. Au waliokamata hawakuwa makini, au walikuwa wakitaka kumpendeza au wanajipendekeza kwa malengo wanayojua wenyewe. Au kama nilivyoeleza Waendesha Mashtaka wa Serikali, DPP na wasaidizi wake wakiwemo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hawajiandai vizuri.

  Kwa kumalizia nirudie tena kuwa wakati ufike sasa Wapenzi wa Vyama na wapenda demokrasia kwa ujumla tusipende sana kujadili mambo kwa ushabiki bali tuanze kuwa na "Critical analysis" ya hali inayokabili demokrasia yetu na kuanza kuhoji viongozi wetu wa vyama. Viongozi wawe wazi kama wamefuata Taratibu za kisheria au wamezoea kufanya mambo kwa " mazoea tu". Hakuna mahali popote sheria inapotamka kuwa "Mikutano ya ndani ya Vyama" haihitaji " Notice". Wala Mamlaka ya Polisi hasa vifungu vya 43, 44 etc vya Police Ordinance, ( kama sijakosea) havijarekebishwa wala kuondolewa, hivyo vikitumika tusilalamike, bali tuwalalamikie viongozi wetu kwa kutokuwa " Proactive" vifungu hivyo vilivyotungwa wakati wa ukoloni vifanyiwe marekebisho ya msingi ili demokrasia ya kweli iweze kujenga msingi katika Taifa letu. Wanasheria wa vyama ningelipenda wawasaidie wapenzi wa vyama katika kutoa elimu ya msingi, lakini pia kuwashauri vizuri pia viongozi badala ya kusubiri " kesi mahakamani".

  Nawasilisha.
   
 2. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #321
  Jul 17, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,583
  Trophy Points: 280
  Mbona wameshatoka akina Masamaki wanarudi ofisini kama kawaida.Ilikuwa kiki kwa pikipiki
   
 3. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #322
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,948
  Likes Received: 8,475
  Trophy Points: 280
  Lowassa fisadi kwa miaka tisa, baada ya kununuliwa lowassa sio fisadi.
   
 4. SANCTUS ANACLETUS

  SANCTUS ANACLETUS JF-Expert Member

  #323
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 5, 2016
  Messages: 1,648
  Likes Received: 1,984
  Trophy Points: 280

  Hiki unachotaka kukisema hapa ni hulka ya kufanya hukumu bila kosa kufanyika kwanza (prejudgement).Vyombo vyote vya dola kwa asili yake havijawahi partial isipokuwa mtu mmoja mmoja kwa maslahi yake au kupotoka au vinginevyo.

  Mahakama in stricto sense, is impartial. Kunaweza kuwa na mahakimu au majaji hapa na pale ambao huamua kuchukua upande katika mashauri kadhaa na hilo haliifanyi Mahakama kuwa kama alivyowahi kusema Dokta au unavyoamini wewe. Tatizo letu tunaathiriwa na historia.

  Kila kitu mbona ....imewahi kuwa hivi....! Dunia haisimami na watu "wahuni" na wasio na mshipa wa aibu katika kuonea au kudhuru wenzao wataendelea kuwepo duniani.Na hata hivi ninapoandika wamezaliwa.Wema pia wamezaliwa. Wapo hata mwisho wa dahari.

  Sasa huwezi kuacha kutafuta haki kisa eti imewahi kuamuliwa vinginevyo na mahakama huko nyuma.Maamuzi yoyote hasi katika jambo lolote lile ni fursa.Ni nafasi nyingine ya kupata upenyo na kufikia ndoto yetu.
   
 5. SANCTUS ANACLETUS

  SANCTUS ANACLETUS JF-Expert Member

  #324
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 5, 2016
  Messages: 1,648
  Likes Received: 1,984
  Trophy Points: 280
  Hiki unachotaka kukisema hapa ni hulka ya kufanya hukumu bila kosa kufanyika kwanza (prejudgement).Vyombo vyote vya dola kwa asili yake havijawahi partial isipokuwa mtu mmoja mmoja kwa maslahi yake au kupotoka au vinginevyo.

  Mahakama in stricto sense, is impartial.Kunaweza kuwa na mahakimu au majaji hapa na pale ambao huamua kuchukua upande katika mashauri kadhaa na hilo haliifanyi Mahakama kuwa kama alivyowahi kusema Dokta au unavyoamini wewe.Tatizo letu tunaathiriwa na historia.Kila kitu mbona ....imewahi kuwa hivi....! Dunia haisimami na watu "wahuni" na wasio na mshipa wa aibu katika kuonea au kudhuru wenzao wataendelea kuwepo duniani.

  Na hata hivi ninapoandika wamezaliwa.Wema pia wamezaliwa. Wapo hata mwisho wa dahari.Sasa huwezi kuacha kutafuta haki kisa eti imewahi kuamuliwa vinginevyo na mahakama huko nyuma.Maamuzi yoyote hasi katika jambo lolote lile ni fursa.Ni nafasi nyingine ya kupata upenyo na kufikia ndoto yetu.
   
 6. c

  chihe JF-Expert Member

  #325
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 22, 2017
  Messages: 249
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 80
  Dr slaa hawezi ikwepa Laana ya kiapo cha upadre alichoapa ndio maana kila anachoanzisha huwa hakifanikiwi laana ya upadre ni mbaya Sana. Pole slaa Kwa Laana hiyo maana sasa huna tofauti na bashite.

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
 7. R

  Rutorial k JF-Expert Member

  #326
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 8, 2014
  Messages: 789
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 80
  uzuri wa dr slaa hakuwa na bei kama alivyozoea kusema...yeye alitimiza wajibu wakisheria basi...aliyemkatalia kufanya mkutano wakati ametimiza masharti slaa aliforce king na kutafuta haki yake ya msingi tena akiwa mbele....nazani ndicho anachojaribu kusisitiza

  Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
   
 8. kimsboy

  kimsboy JF-Expert Member

  #327
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 17, 2016
  Messages: 2,653
  Likes Received: 2,440
  Trophy Points: 280
  alipokua ccm mlikua mnaona makengeza kuwa hakua fisadi sio?
   
 9. H

  Hatihat Senior Member

  #328
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 29, 2012
  Messages: 133
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Ukifikiri sana, lazima utafika kwenye conclusion yako kwa jinsi Dr. Mihogo na Le profesor Lip wanavyo behave kwa sasa.
   
 10. j

  joely JF-Expert Member

  #329
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,035
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa salaam,

  unaweza kututhibitishia wakati ukiwa katibu mkuu wa Chadema kama mlikuwa mnaomba vibali kwa mikutano ya ndani?

  pia kumbuka ulituachia Chadema ya harakati sasa wanasema harakati basiii , sijui wanafanya nini ngoja tuone, itakuwaje

  Ni wazi kuwa CHADEMA ndio inakufa au inafanya timing fulani, ni mapema sana kwangu kuwalaaumu viongozi hao.
   
 11. rashidikurwa

  rashidikurwa Member

  #330
  Jul 17, 2017
  Joined: Jul 16, 2017
  Messages: 34
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 25
 12. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #331
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,362
  Likes Received: 7,093
  Trophy Points: 280
  Hivi umeelewa kwanni nmetumia historia kujenga hoja???

  nmesema dk slaa aliwahi kusema kuwa mahakama za tanzania hazina uhuru maana zinaingiliwa na ccm kwenye maamuzi yao akitolea mfano wa kesi ya lwakatare sasa ndio najiuliza ina maana kasahau yye ndio alituambia mahakama sio huru ssa iweje kma maneno yake ni ya kweli atushauri tena twende hukohuko mahakamani ambapo hukumu itatolewa kwa kuingiliwa na maamuzi ya ccm watakavyotaka????

  Hivo ndio nlichomuuliza basi ssa hayo yako ya kuniwekea lugha ya kigeni humu ili nikuone msomi hayana tija kabisa
   
 13. zitto junior

  zitto junior JF-Expert Member

  #332
  Jul 17, 2017
  Joined: Oct 7, 2013
  Messages: 8,362
  Likes Received: 7,093
  Trophy Points: 280
  kwahiyo sio tena mzee wa maandamano na matamko??? kaz kwelikweli
   
 14. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #333
  Jul 17, 2017
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,947
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Siwezi kuamini kama mwandishi wa makala haya ameshasahau aliyokuwa analalamikia alipokuwa bado ndani ya chama na yeye pia alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wanakumbwa na mikikimikiki kwa ajili ya kutetea demokrasia nchini. Hata kama anadai amestaafu siasa angekuwa katika hali nzuri zaidi ya kuwa objective na kutoa ushauri na kuonyesha njia na siyo kujifanya kama hajui katika nchi zetu hizi za Afrika bado kuna shida ya kuheshimu katiba, utawala wa sheria, haki za binadamu na demokrasia (hasa uhuru wa kutoa maoni).
   
 15. Rayban/p

  Rayban/p JF-Expert Member

  #334
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 30, 2015
  Messages: 1,111
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Anatumiaa kajinaa ganii ukoo nikaperuziiii
   
 16. R

  RUTAGAMBWA JF-Expert Member

  #335
  Jul 17, 2017
  Joined: Jun 15, 2017
  Messages: 523
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 80
  Slaa Bora upumzike utuachie inchi yetu, wewe mbona ulipigwa mabomu kule Arusha na mkeo wakamtoa midamu, inamaana na wewe hukufuata utaratibu????

  Umeshachoka wewe au umeshiba tayari, mwenye shibe huwa hakumbuki mwenye njaaa
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #336
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,498
  Likes Received: 117,186
  Trophy Points: 280
 18. yakowazi

  yakowazi JF-Expert Member

  #337
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 1,279
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Ni kweli wala hatuuhitaji yeye ashughulike na yake si alituona wpuuzi sasa nini tena ushauri awape ninyi
   
 19. J

  Jozi 1 JF-Expert Member

  #338
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 16, 2015
  Messages: 5,054
  Likes Received: 2,293
  Trophy Points: 280
  Mie naomba picha tu ndo ziongee tapatalk_1472540191576.jpeg
   
 20. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #339
  Jul 17, 2017
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 8,344
  Likes Received: 2,388
  Trophy Points: 280
  Je, kuna tofauti na jeshi la polisi la mkoloni kwa sheria hii?
   
 21. Z

  Zanzibar-ASP JF-Expert Member

  #340
  Jul 17, 2017
  Joined: Nov 28, 2013
  Messages: 4,506
  Likes Received: 7,133
  Trophy Points: 280
  Dr.Slaa Mungu anakuona...

  Malipo ni hapa hapa, ipo siku tu, Canada unapita tu, Tanzania ndio kwenu.

  Kilio chako kitakuwa kikubwa kuliko hichi tunachoumizwa sasa sisi watanzania.

  Leo hii unafurahia wanyonge kuumizwa, unajifanya huoni kinachofanyika, unajifanya hujui kinachoendelea...
   
Tags:
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...