Marumeso
JF-Expert Member
- Oct 3, 2009
- 1,410
- 1,322
Hii ni kwa zile benki ambazo mteja analazimika kusimama/kupanga kwanza foleni kupata huduma. Unakuta wakati watu mmesimama foleni, wenzenu wengine wamekaa kwenye benchi wanapiga stori bila wasiwasi huku nao wakisubiri foleni isogee wajichomeke hapo mbele zamu zao zinapokaribia.
Binafsi nachukizwa na tabia hii kwa kuwa wengi ya watu hawa unakuta hawaonekani kuwa na shida lolote la kimwili (walau kwa kumtazama) linalofanya asisimame foleni kama wengine. Wengine ndo unakuta mtu kaingia tu anapitiliza mbele anataka ahudumiwe kabla ya aliowakuta hapo.
Hii tabia ni ya hovyo kabisa, ni ubinafsi na kukosa ustaraabu tuziache wapendwa. Kila mtu ana haraka sio wewe tu.