Kujua wakati una mimba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Wanawake wengi hujua wameshika mimba aghalabu wiki 3 baada kushika mimba. Mwili wenyewe utakuonyesha/utakutabiria kama:

Hedhi yako itakoma/itakuwa nyepesi
Utasikia uchefuchefu/utatapika (ugonjwa wa asubuhi – ‘morning sickness’ – na inaweza kutokea wakati wowote wa siku pia).
Matiti yako yataanza kuwasha, kufura au yataanza kuwa makubwa.
Chuchu (ncha ya titi) na sehemu zilizokaribiana zitaanza kuwa nyeusi na zizizoweza kuvumilia.
Itakubidi kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Utasikia uchovu
Kusokotwa na tumbo

Kama umeona baadhi ya dalili hizo, unaweza kuwa na mimba. Pata jaribio/uchunguzi kipimo cha mimba ili kupata yakini! Unaweza pimwa bure katika kliniki iliyokaribu nawe au ununue kifaa vya kujipmia nyumbani kutoka duka la dawa. Daktari wako anaweza kukupima pia au atakuelekeza kwa mtaalamu kama hauna.

Umuhimu wa kunyonyeasha
Pindi tu baada ya kujifungua,kumung’unya wa kujirudia rudia wa mtoto hutoa oksitoksini kutoka kwa teziubongo wa mama.Homoni hii haiashirii tu matiti kumtolea mtoto maziwa (hii inajulikana kama tendohiari la utoaji wa maziwa ama “let-down), lakini wakati huo huo husababisha mkunyato katika mji wa mimba. Mkunyato unaotokea huzuia utokaji wa damiu uliozidi na husaidia mji wa mimba kurudia ukubwa wake wa kawaida.

Ikiwa mama atanyonyesha mtoto bila ya kutumia maziwa mbadala ama vyakula vingine kipindi chake cha kuingia mwezini kitacheleweshwa.Tofauti na akina mama ambao huwalisha watoto wao kwa kutumia chupa, ambao kwa kawaida huingia mwezini baada ya majuma sita hadi manane, akina mama wanaonyonyesha wanaweza kukaa bila ya kuingia mwezini kwa kipindi cha miezi kadhaa. Hali hii ina manufaa muhimu ya kuhifadhi chuma katika mwili wa mama na mara kwa mara hutoa nafasi asili baina ya uja uzito.

Kunyonyesha ni kuzuri kwa akina mama wapya na vile vile kwa watoto wao. Hakuna chupa za kufisha vijidudu,hakuna haja y a kununua maziwa ya mtoto,kupima na kuyachanganya.Inaweza kuwa rahisi kwa mama anayenyonyesha kupoteza uzani wa uja uzito vile vile kwani kunyonyesha kunatumia vizio vya joto. Kunyonyesha pia husisimua mji wa mimba kukunyata na kurudia ukubwa wake halisi.

Mwanamke anayenyonyesha huzalimishwa kupumzika ambako anahitaji sana.Ni lazima akae chini na kupumzika kila baada ya masaa kadhaa ili anyonyeshe.Kunyonyesha wakati wa usiku ni rahisi pia. Ikiwa amelala chini, mama anaweza kulala huku bado ananyonyesha.

Kunyonyesha pia ni njia asili ya kuzuia mimba-hata ingawaje sio ya kutegemewa.Kunyonyesha mara kwa mara huzuia uzalishaji wa mayai na hivyo kupunguza uwezekano wa mama anayenyonyesha kuingia mwezini, kutoa mayai ama kupata uja uzito. Hakuna hakikisho hata hivyo. Mama ambao hawataki watoto wengi wanapaswa kutumia mbinu za kuzuia mimba hata ikiwa bado wananyonyesha. Kujidunga homoni na vipandikizi wakati wa kunyonyesha ni salama kama zilivyo mbinu za kinga za kuthibiti uzazi.Maelezo kwenye vidonge vya kuthibiti uzazi vinasema ya kwamba ikiwezekana mbinu nyingine ya kuzuia uja uzito inafaa kutumiwa hadi mtoto achishwe ziwa.

Kunyonyesha pia hupunguza gharama.Hata ingawaje mwanamke anyenyonyesha huwa na hamu kubwa ya chakula na hula kalori zaidi, chakula chake cha ziada sio ghali ukilinganisha na kununua maziwa ya mtoto. Kunyonyesha hupunguza matumizi ya pesa ilhali hutoa chakula ambacho ni bora zaidi kwa mtoto.

Manufaa ya Kipindi Kirefu ya Kunyonyesha
Sasa imeanza kuwa bayana ya kwamba kunyonyesha humpatia mama zaidi ya manufaa ya kipindi kifupi katika kipindi cha hapo mwanzoni baada ya kujifungua.
Utafiti umeonyesha manufaa mengine ya kiafya ambayo mama anaweza kuyafurahia kwa kunyonyesha.Manufaa haya yanajumuisha afya bora, kupungua kwa hatari ya baadhi ya saratani na manufaa ya saikolojia.
Kitu kingine muhimu kinachotumiwa katika kuzalisha maziwa ni kalshiamu.Utafiiti wa hivi sasa unaonyesha ya kwamba baada ya kuachisha watoto ziwa,uzito wa mfupa wa mama anayenyonyesha hurudia ule wa kabla ya uja uzito ama huwa hata wa juu zaidi. Mwishowe,kunyonyesha kunaweza kusababisha mifupa yenye nguvu zaidi na hupunguza hatari ya ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) “mifupa iliyokonda.”Utafiti wa hivi sasa umethibitisha ya kwamba wanawake ambao hawakunyonyesha wako katika hatari kubwa ya kuvunjika kwa nyonga baada ya kukoma hedhi.
Wanawake ambao hawanyonyeshi wameonekana katika utafiti mwingi kuwa katika hatari kubwa ya kupata saratani za uzazi. Saratani ya ovari na ile ya mji wa mimba zimepatikana kuwa za kawaida katika wanawake ambao hawakunyonyesha.
Hitimisho: Kunyonyesha hupunguza hatari ya matatu kati ya magonjwa mabaya sana katika wanawake-saratani za wanawake, ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa mifupa-bila ya tishio lolote la kiafya.

Masuala ya Kisaikolojia Kwa Akina Mama Wanaonyonyesha
Kunyonyesha ni zaidi ya kutoa tu lishe na kumlinda mtoto dhidi ya magonjwa kupitia kwa maziwa ya mama.Kunyonyesha hutoa njia ya kipekee ya kuingiliana baina ya mama na mtoto, kukaribiana kwa papo hapo kwa ngozi –kwa-ngozi na malezi ambayo akina mama wanaotumia chupa wanapaswa kufanya jitihada ili wayarudufu.
Prolactin ambayo ni homoni inayotengeneza maziwa,huonekana kutoa utulivu maalumu kwa akina mama na kuwasaidia kupambana na mfadhaiko kwa njia iliyo bora.
 
Utunzi wa mama kabla ya kuzaa

Huu ni utunzi ambao hutolewa kwa mama wakati wa uja uzito ili kuhakikisha ya kwamba mama anabakia kuwa mwenye afya na anajifungua mtoto mwenye afya.Hujumuisha mambo yafuatayo:

  • Ukadiriaji wa hatari zinazoweza kumkumba
  • Ukadiriaji unaondelea wa ustawi wa kijuzi
  • Ukadiriaji unaoendelea wa utata
  • Elimu kuhusu usumbufu wa kawaida wakati wa uja uzito,hali ya hisia (ukijumuisha huzuni wa baada ya kujifungua),vikao vya darasa kuhusu kabla ya kujifungua.
  • Majadiliano kuhusu kujifungua na jinsi ya kujifungua
Kujipatia matibabu
Historia ya uvutaji sigara, unywaji wa pombe na matumizi ya madawa inafaa kutathminiwa. Pia wanawake wanashauriwa kutojitibu kabla ya kuangalia kwanza usalama wao na wa mtoto aliyetumboni. Ni bora kutaja kwamba vitamini na tiba za kutumia mitishamba zinafaa kupunguzwa wakati wa uja uzito. Kwa mfano, matumizi ya zaidi ya vidonge viwili vya Vitamini A kila siku kunaweza kusababisha dosari za kuzaliwa kwa mtoto atakayezaliwa.

Mlo
Ushauri kuhusu mlo unafaa kutilia mkazo mlo kamili na vyakula tofauti tofauti ukisisitizia kabohaidreti changamani na protini, pamoja na kiasi cha kutosha cha foliate(miligramu 0.5), chuma (miligramu 15) ,kalshiamu (miligramu 1200) na maji (lita 2-3) kila siku.

Tembelea kituo cha afya ya mama wajawazito
Tembelea ktuo cha afya ya mama wajawazito kila mwezi katika kipindi cha kwanza cha wiki 28, baadaye nenda baada ya kila wiki mbili mpaka wiki ya 36. Kutoka hapa nenda kila wiki mpaka siku ya kuzaa. Kila wakati unapotembelea kituo cha afya, hali ya afya yako na ya mtoto wako inaangaliwa.
Usumbufu wa kawaida wakati wa ujauzito

  • Ongezeko la kutaka kwenda haja ndogo ni kawaida lakini linafaa kufanyiwa uchunguzi kwani 8% ya wanawake waja wazito watakuwa na maambukizo katika eneo wanalotumia katika haja ndogo ambayo hayaonyeshi dalili.
  • Uvimbe katika kifundo cha mguu unaweza kuhusishwa na kushinikiza kwa mishipa itwayo inferior vena cava. Ikiwa kuvimba hakuambati na shinikizo la damu, tiba huwa kupumzisha miguu ikiwa imewekelewa juu kama vile ya kiti au kwa kutumia vyakula kama Celery au Vitamin B6 ambazo kwa kawaida huondoa maji mwili kupitia kukojoa mara nyingi.
  • Kufura kwa mishipa kwa sababu zizo hizo na kupata nafuu baada ya kufuungiwa kunaweza kuwa kwa kushtua. Pindi tu inapotambulika, matumizi ya mapema ya stokingi za kushikilia ni jambo la busara; ilhali matumizi ya mda mfupi ya kiinua fupanyonga na vipande vya barafu vinaweza kumaliza dalili hizi za kufura kwa mishipa katikaa tupu.
  • Kiungulia husababishwana kupwa kwa tumbo na umio pamoja na ongezeko la shinikizo la tumbo.Ushauri wa mkao na mlo pamoja na matumizi ya vimaliza asidi humaliza mengi ya haya, lakini mpinzani wa H2 (kitengo cha B katika uja uzito) anahitajika mara moja moja.
  • Uyabisi wa tumbo (kuwa na gesi kwa tumbo) unaweza kutokea mapema lakini angalau husababishwa na homoni lakini unaweza kuzidishwa na ongezeko la yaliyomo kwenye fupanyonga.Ongezeko la ukubwa wa mishipa na kushinikizwa kwa mishipa katika fupanyonga kunaweza kusababisha kufura kwa mishipa. Wanawake wanapaswa kushauriwa kuongeza matumizi yao ya uoevu na ufumwele na ikiwa dawa za kuharisha zinahitajika zinapaswa ziwe za aina ya ufumwele k.m Metamucil ama Fybogel.
  • Kuumwa na sehemu ya chini ya mgongo ni jambo la kawaida kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya mkao.
  • Kuoza kwa meno na magonjwa ya tishu zinazozunguka meno huongezeka wakati wa uja uzito na unafaa kushughulikiwa na dakitari mapema.
  • Mabadiliko katika ngozi yanajumuisha madoa ya hudhurungi kwenye ngoziambayo hutoweka baada ya ujauzito.
  • Mikwaruzo hutokea katika 17% ya wanawake waja wazito. La kuvutia ni ya kwamba 50% ya wanawake wenye ugonjwa wa ngozi huonyesha dalili za kupata afueni wakati wa uja uzito. Ikiwa hakuna kipele, zingatia ukosefu wa chuma ama hali inayoweza kuwa hatari ya kusimama ama kupunguza kasi ya mtiririko wa nyongo wakati wa uja uzito. Dawa za kuzuia mzio zinaweza kuwa za manufaa.
  • Alama zinazobakia kwenye ngozi ya tumbo, mapaja, makalio ilinyooka baada ya uja uzito ikiwa ukuaji umekuwa wa haraka. Ukavu na kujikunakuna kunaweza kutulizwa na mafuta ya mboga ama krimu ya Vitamini E na kutotumia sabuni.
 
Vipimo vya mimba

Vipimo hivi huchunguza kuwepo kwa Human Cherionic Cronadotropin (HCG) kwa mkoja au damu. HCG wakati mwingine hitwa ‘Pregnancy Hormone’ na huwa kwa mwanamke tu wakati ana mimba. Kuna aina mbili ya vipimo: kipimo cha mkojo na kipimo cha damu.

Kipimo cha Mimba cha Mkojo
Wanawake wengi hutumia kipimo hiki ambacho pia huitwa cha nyumbani (HPT-home pregnancy test) kwa sababu ni rahisi kutumia na bahasa (rahisi kibei) kuna aina nyingi za vipimo hivi. Kwa kimoja, utakwanya mkojo wajo kwa kikombe na kukitumbukiza ‘kijiti’ huko na kwakingine utaweka ‘kijiti’ hicho kwenye viungo vya mkojo. Njia iliyobora ni itakayokuonyesha kiwango cha HCG, hivyo tafuta moja katika kiwango cha hCG kutoka 15 hadi 30. Utasaidiwa na mhudumu wako dukani la dawa au kliniki.

Vifaa hivi hufaa kwa asilimia 97-99 kuyakirisha uwepo wa mimba vinapotumiwa ipasavyo. Hivyo kufuata maagizo ni muhimu. Pia angatia wakati wa kuharibika wa kifaa kwani kifaa kilichoharibika hakitakupatia matokeo unayotarajia.

Kama utapata matokeo yasiyofaa/yasiyo hakika
Kama utajipima/utapimwa bado kidogo*, unaweza kuona kwamba hauna mimba ili hali unayo. Aina nyingi ya vipimo vya nyumbani hukushauri ujipime baada ya siku kadha bila kujali matokeo uliyopata awali. Kama unaendelea kupata matokeo yasiyofaa nab ado unashuku una mimba, ongea na daktari/mkaguzi afya waka.

Kama utapata matokeo yafaayo/yahakika
Kama utapata matokeo ya hakika, fanya miadi na mkaguzi afya wako punde tu. Mkaguzi wa afya yako atayakinisha kama una mimba kupitia kipimo cha damu na ukaguzi mwingine (pelvic exam) na atakwambia chaguzi uliza nazo.

Kipimo cha Damu
Kama wataka kipimo cha damu badala ya kite cha nuymbani, fanya miadi na mkaguzi afya wako/dakatari wako.
 
thanks kwa somo zuri MziziMkavu, tuanze hapo kwenye kunyonyesha. kwa wale akina mama ambaoo ni walezi yaani baada ya kujifungua huwa hawawez kuingia hedhi hadi wameachisha kunyonyesha, basi hawa mara nyingi sana huwa hawawez kupata ujauzito lakin sasa kutokana na maazingira waweza kukuta unaconceive mara nying ikitokea haali kabla ya kuona hedhi jua yai lilipokomaa lilikutana na mbegu b4 mens. lakin pia kwa yule aliye ustudy mwili wake vizuri akajua tabia zake basi anaweza hata asitumie hizo hormones wakati ananyonyesha.

mathalani mm ni miongoni mwa wanawake wanao lea so mpaka nimwachishe mtoto ndipo ninapoanza kuona period mbali na hapo sion kabisa. kwa muda wote huu mm huwa siwez kupata ujauzito kbisa kwa kizazi kinakuwa kimesinyaa. kama nikimwachisa mtoto kumyomya akiwa na miaka 2 basi kwa muda wote huo sitapata hedhi. hii ni njia nzur sana ya kupanga uzazi but iko ltd kwa baadhi ya watu.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu asante sana hiyo njia ya kumnyonyesha kwa muda wa miaka 2 ndio njia wanayotumia wanawake wa kiislam inakuwa wewe mzazi hupati mimba mpaka baada ya miaka 2 inakuwa jambo zuri kwa faida yako wewe na mtoto wako anakuwa na afya bora unajuwa maziwa ya kopo sio mazuri kumnyonyesha mtoto anakuwa hana afya nzuri kuliko maziwa ya Mama asante sana mkuu inaonyesha wewe watoto wako uliwanyonyesha miaka 2? Kina mama siku hizi hawanyonyeshi watoto muda mrefu eti kwa kuogopa maziwa yao yatanguka au kuwa makubwa kasheshe kweli.................................... gfsonwin
 
Mi nilipata hedhi mwezi mmoja baada ya kujifungua ikabidi nitumie kalenda mpaka leo ana miaka miwili na miezi saba
 
child spacing in my family is 3 yrs. so atleast huwa napata muda wa kurudisha afya kabla sijaconceive tena. ila hii theory doesn't apply to most of women and imeshakuwa kama vile watu do not trust it any more.
 
Mi nilipata hedhi mwezi mmoja baada ya kujifungua ikabidi nitumie kalenda mpaka leo ana miaka miwili na miezi saba

safi sana, kwa hiyo ulishaujulia mwili wako. mimi huwa sipend matumiz ya madawa ya kupanga uzazi so am always against it.
 
child spacing in my family is 3 yrs. so atleast huwa napata muda wa kurudisha afya kabla sijaconceive tena. ila hii theory doesn't apply to most of women and imeshakuwa kama vile watu do not trust it any more.
Ok ni vizuri ukiwa unapanga wakati wa kupumzika sasa una watoto wangapi mwenzangu? ............. gfsonwin
 
Last edited by a moderator:
Jamani kunyonyesha miaka miwili mwenzenu naona sifikishi, hii ni kutokana na kwamba nakonda sana kila siku, baada ya uzazi nilikuwa nimenenepa ila sasa nakonda kila siku naona nitamwachisha akiwa na mwaka tu labda na miezi 2.
 
Pika

Uji, juice kwa sana! Wewe ni mvivu kula km Mimi.
 
Back
Top Bottom