Kujua kama upo kwenye mahusiano mabaya (Toxic relation)

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
18,721
29,241
Topic ya leo tunaongelea kuhusu toxic people, na jinsi ya kujua kama upo katika mahusiano na mtu toxic. Nikisema mtu toxic namaanisha wale watu ambao wanakuumiza akili, moyo, confidence yako na hata mawazo yako. Hizi ni njia 5 tu ambzo zitakusaidia kujua kuwa huyo mtu ambaye upo naye katika mahusiano ni toxic ama vip.

1 - Katika malumbano kati yenu yeye huwa anataka kukuumiza wewe na sio kusuluhisha tatizo kati yenu.

Jamani ndugu zangu, manatakiwa kujua kuwa ili mahusiano yenu kuwa mazuri, kuwa perfect, wewe na mwenza wako mnatakiwa mtafute njia ya kusuluhisha matatizo kati yenu. Lakini kama kila ukigombana na mwenza wako yeye always anatafuta tu njia ya kukuumiza wewe basi that person is TOXIC. Haimaanishi kuwa hamtakiwi kugombana, kila mahusiano kuna matatizo.

2 - Wanafanya kila kitu kama ni mashambulizi.

Mfano ukienda kwa mwenza wako na maybe unataka kuongea naye kuhusu kitu ambacho hukupendezwa nacho, labda kitu alichofanya this week aua alichosema. Unaweza ukamuendea kwa upendo wote lakini yeye akachukulia vibaya.
The best way to know this ni hivi, fikiria kwa sasa katika mahusiano yenu, Je unauhuru wa kumuendea mwenza wako kuhusu jambo lolote? Huna uwoga kwamba nikimuambia kitu fulani ataishia kukasirika tu, kama huwezi basi ujue kuwa you are not in a healthy relationship and Yes, you are dating a TOXIC person.


3 - Wanakufanya wewe ndio sababu ya kila tatizo katika mahusiano yenu.

Hapa inakuwa kila tatizo, kila kitu kibaya kitakachotokea ndani ya mahusiano yenu ni your fault, wewe ndio utakuwa unalaumiwa kwa kila kitu. Utaambiwa kuwa wewe ndio tatizo na wewe ndio huelewi. Badala ya ku-admit kuwa yeye ndio amefanya kosa ni lazima tu atatafuta njia ya kugeuza mambo na kukufanya wewe ndio uonekane ndio mwenye kosa.
Toxic people huwa ni good manipulators, yaani wanajua kudanganya na kuendesha watu. Wanaweza kukufanya kuwa wewe ndio mwenye tatizo hata kama yeye ndio mwenye kosa. Ukimuachi mtu kama huyo kuendelea kukuendesha au ukiendelea kuwa katika mahusiano na mtu kama huyo ni lazima ataharibu ujasiri wako, no matter how strong and confident you are.

4 - Atakuonesha upendo mkubwa sana pindi ukiwa chini.

Tatizo kubwa la toxic people ni kuwa baada ya kukuumiza, kukusingizia vitu, kukufanya nujisikie huna maana, ( and Yes toxic people watakufanya uamini kuwa yeye tu ndio anakupenda, kuwa hakuna mtu mwingine zaidi yake yeye atayekupenda, na ukiamini hiki ndio kinampa nguvu ya kukufanyia chochote anachotaka ). So baada ya kukuumiza na wewe ndio upo at your lowest point, hapo ndio atakuonesha upendo kubwa zaidi ya siku zote, akishagundua kuwa umeumia ndio he/she will put down his/her armor.
Hii ni kwasababu katika kipindi ambacho wewe unaujsari na huumii, yeye anajiona kama hana nguvu juu yako, na hivyo always anataka yeye ndio awe mwenye nguvu.

5 - Anakuwa hana Furaha na mafanikio yako.

A toxic person atakushusha hata kama unafanya vizuri katika maisha yako, ni lazima tu atatafuta njia ya kukufanya uone kuwa mafanikio yako sio ya muhimu, like it is not a big deal. Hata kama umefanikiwa kupata kitu ulichokuwa unakifanyia kazi kwa muda mrefu, kamwe hatosherekea na wewe, atabadilisha topic, na kuanza kuelezea kitu kingine au atatafuta tatizo lolote tu.

Hii ni kwasababu toxic people wanapenda wewe uwe chini, usimpite kwenye chochote, iwe mshahara mnayopokea, mafanikio mnayopata, furaha yaani kwa kila kitu yeye ndio anataka kuwa juu yako. Yeye tu ndio anataka awe mtu anayekupa furaha ndio maana atakuweka chini kwa kila jambo zuri litakalokutokea ili ukisha-break sasa yeye ndio apate nafasi ya kuja kukunyanyua tena.

Ndugu zangu kama uko kwenye mahusiano na mtu wa aina hii.. jitafakari tena.
 
Sio wote wako ivo kuna watu wanajua kuigiza yan atakubembeleza wala usielewe nia yake tena unapewa na vijizawad bhas mtto wa watu unakubal kumbe moyon mwake wala hana hata time na ww kakueka kama part time tuu
 
Sio wote wako ivo kuna watu wanajua kuigiza yan atakubembeleza wala usielewe nia yake tena unapewa na vijizawad bhas mtto wa watu unakubal kumbe moyon mwake wala hana hata time na ww kakueka kama part time tuu
Sio wote.... ila utakubali kuwa watu w aina hii wapo. na katika kupita katika mahusiano lazima utakuwa umeshawahi kukutana na watu wa aina hii.
 
Asante Mungu uliniepusha na toxic moja hatarikila kitu wewe ni mbaya tu hadi unaambiwa shetani ana afadhali
 
Tukubaliane kuna watu kwenye mahusiano ni kama vile wanakunyima pumzi
 
Back
Top Bottom