Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam Paul Makonda ameamua kulivalia njuga suala la biashara ya mihadarati nchini.
Bwana Makonda anaamini kwamba mkoa wa Dar-es-Salaaam ndiyo unaoongoza kwa biashara hii iloshamiri kila pembe.
Itakumbukwa mwishoni mwa mwaka jana, Paul Makonda alifanya ziara ya kuutembelea mkoa wa Dar-es-Salaam kuufahamu vizuri na kutaka kuangalia namna ya kuuboresha mkoa huu ambao yeye ni mwakilishi wa raisi.
Paul Makonda alipita maeneo mengi na mojawapo ya maeneo hayo ni eneo maarufu la uwanja wa fisi.
Akiwa eneo hilo Makonda alishuhudia kwa macho yake watumiaji wa madawa ya kulevya na mateja wengi ambao hawana ajira na wengine wakiwa wamekata tamaa ya maisha kutokana na hali duni kifedha na kimaisha.
Lakini hivi karibuni mheshimiwa Makonda amaeamua kuwatangaza hadharani wale wote wanaotajwa kuhusika na biashara hii ya mihadarati huku ikisadikiwa kuwa bei ya gram 50 kwa kilo mitaani imesimama kwenye shilingi za kitanzania 140,000 taslim.
Lakini nikiwa mdau wa masuala ya teknolojia, na ujasirimali , imebidi nichangie kidogo kuhusu biashara hii ya madawa ya kulevya, matumizi ya teknolojia na ujasusi wa kutukuka.
Kisha ntaelezea namna ya kuweza kupambana na njia zinazotumika kufanikisha biashara hiyo na hatima yake kama angalau italeta ahueni kwa watumiaji au Mateja huko mitaani.
Biashara hii ya madawa ya kulevya inafanikishwa kwa kutumia njia za usafiri wa ndege, meli, binadamu, malori, mitumbwi na boti kasi, pamoja na magari yaagizwayo na kuingizwa nchini Tanzania.
Kwa kifupi mkoa wa Dar-es-Salaam ambao ni mkoa wa kibiashara wa Tanzania "Commercial City" mpaka sasa katika duru za biashara hii mkoa huu unatambulika kama ndiyo kituo kikuu ya usafirishaji wa madawa haya au "major transit route" ya madawa yanayopitishwa kwenda nchini Afrika Kusini kupitia bandari ya Mtwara.
Mpaka kufikia mwanzoni mwa mwaka 2016 biashara hii ilikuwa imeota mizizi mikubwa ilokomaa na kuthibitisha hilo mheshimiwa raisi wa JMT John Magufuli aliona jinsi machine za udukuzi "Scanners" katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na baadae pale Bandarini Dar-es-Salaam zikiwa hazifanyi kazi.
Kuharibiwa kwa makusudi kwa mashine hizo ni katika kuhakikisha mzigo unapitishwa na vijana wabebaji bila shida, huku malori yakipitisha mizigo hiyo katika bandari za Dar-es-Salaam, Mtwara, Tanga, Zanzibar na bandari za kutengezwa (boat parking berths) kama Bagamoyo na Kunduchi.
Safari ya madawa ya kulevya inaanzia nchini Afghanstan nchi ambayo haina bandari au "landlocked".
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya umoja wa mataifa kitengo kinachoshughulikia madawa au UNODC, nchi ya Afghanistan inazalisha tani 355 kila mwaka ikiwa ni asilimia 90 ya madawa yote yanayozalishwa duniani.
Pakistani na Afghanistan kwa pamoja wanatumia mpaka wao ambao una kilomita zipatazo 2500 ambao pia unawasaidia watoroshaji wa madawa hayo kupitia sehemu mbalimbali za kusini na kusini mgharibi mwa Pakistani hususani katika majimbo ya Sindh ambako kuna bandari ya Karachi na Balochistan ambako watoroshaji wanatumia njia ya ardhini.
Pamoja na madawa haya kupenyezwa na kusafirishwa kwenda barani Ulaya na Marekani lakini pia kuna njia ya kuyapitisha kuhakikisha yanafika katika pwani ya Tanzania.
Waafrika waliopo nchini Pakistani katika mji wa bandari wa Karachi huakikisha madawa hayo yanapakiwa katika mabunda madogomadogo "nylon sachets" kisha kuwekwa ndani ya madebe maalum na kuwekewa kifaa maalum ya kukifuatilia au "tracking device" kiitwacho GPRS yaani General Packet Radio Service.
GPRS ni mfumo wa mawasiliano ya simu ambao unatumia mtambo wa 2G na 3G kusafirisha kipande cha taarifa au Data kwa kasi.
Mwishoni mwa miaka ya tisini kulikuwa na mfumo wa 2G na baadae mwaka 2001 ukaja mfumo wa 3G na baadae mwaka 2012 tumeona mfumo mpya wa 4G ambao ndiyo unatumika kwa sasa kwenye simu za mikononi.
Lakini wasafirishaji wa madawa ya kulevya wao bado wanatumia mifumo ya 2G na 3G ambayo inawasadia kuhakikisha picha za mizigo, video na sehemu kidogo ya maelezo ya kuhusu mzigo kama umepakiwa salama na umeondoka bandarini Karachi kuelekea pwani ya Dar-es-Salaam.
Meli zitokeazo Karachi zikifika mbali kidogo ya pwani ya Tanzania karibu na bandari za Tanga, Zanzibar na Bagamoyo, nyakati za usiku au mchana, mizigo hiyo ya madawa hudondoshwa bandarini na hapo boti kasi huelekea katika sehemu hizo huku wasafirishaji wakitumia simu za mikononi na vifaa vya mawasiliano kukomboa mizigo hiyo na kuifikisha katika nchi kavu za miji ya Tanga, Dar-es-Salaam na Zanzibar.
Kwa kuwa biashara hiyo ni rasmi katika mji wa Dar-es-Salaam, yapo maeneo kadhaa ambayo yana bohari maalum za kuhakikisha mizigo hiyo inafunguliwa na kufungwa upya katika uzito mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko na mizigo mingine kuwa tayari kusafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini kupitia bandari ya Mtwara.
Tayari majina mbalimbali yametajwa kuhusishwa na biashara hii na majina mengine ni mazito ambayo yanahusisha watu wenye nafasi katika jamii.
Vita ya madawa ya kulenya ni kubwa na inayohitaji umakini mkubwa lakini haiwezi kushindwa.
Pia vita hii inahitaji uwezo mkubwa wa fedha ambazo zitawekezwa kwenye idara husika ya kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya.
Tumesikia raisi wa Philippines bwana Rodrigo Duterte yeye aliamua kuwa watumiaji wa madawa ya kulevya wauwawe tangu ainge madarakani mwezi Juni mwaka jana na mpaka sasa watu 7600 wakiwemo watumiaji na wasambazaji wameuawa.
Pamoja na kuwepo kwa watu wanaopinga vita hii ya madawa ya kulevya inayofanywa na raisi Duterte, idadi kubwa ya wananchi wanaunga mkono juhudi yake hii kiasi cha kumpa nguvu ya kusema kwamba kampeni yake hii itaendelea ndani ya kipindi chote cha utawala wake ambao utaishia mwaka 2022.
Hapa nchini Tanzania mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam ambao umeathirika na biashara hiyo nae ameamua kulivalia njuga suala hilo na anahitaji pongezi na msaada mkubwa.
Fedha zinazohitajika ni pamoja na zile za kujenga vituo maalum au kutenga kitengo maalum au "rehabilitation centre" ndani ya hospitali kadhaa ili kuwasaidia wale mateja wote ambao watakuwa tayari kushirikiana serikali katika mapambano dhidi ya biashara hii.
Lakini pamoja na mkuu wa mkoa bwana Paul Makonda kujitokeza kujaribu kutatua tatizo hili bado kunahitajika juhudi zaidi khasa za wizara ya mambo ya ndani na kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya.
Na kama nilivyoainisha hapo juu teknolojia inayotumika kuwezesha usafirishaji wa madawa haya, kwa Tanzania tuna budi kuwekeza katika vifaa na teknolojia katika kukabiliana na suala hili khasa kuwa hatua moja mbele au "one step forward".
Kwa kuwa wasafrishaji wanatumia vifaa vya GPRS kufanikisha biashara yao basi polisi wa kitengo cha kudhibiti madawa wanapaswa kuwa na ujuzi wa teknolojia kama hizi, kupewa vitendea kazi kama "helicopter" maalum zenye uwezo wa kupiga picha nyakati zote za mchana na usiku (ingawa shughuli hizi hufanywa usiku) na ndege zijiendeshazo zenyewe au "Drones".
"Helicopter" na "drones" zinaweza kutumika kufanya doria katika pwani za Tanga, Dar-es-Salaa, Bagamoyo, Zanzibar na Mtwara.
Lakini vita hii itafanikiwa pia kwa waziri husika wa mambo ya ndani kuja na mikakati yake ambayo anapaswa kuisoma bungeni kwa kutumia muswada wa dharura ambao utakuwa umerekebisha baadhi ya vipengele mbalimbali vya makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Mpaka sasa ni mheshimiwa raisi John Magufuli na Paul Makonda peke yao ambao wametoa kauli kuhusu biashara hii ya madawa ya kulevya hadharani.
Waziri husika Mwigulu Nchemba upo wapi?