Kujivua magamba bila sheria kuchukua mkondo wake ni usanii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujivua magamba bila sheria kuchukua mkondo wake ni usanii.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Jun 18, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katika siku za karibuni tumekua tukishuhudia kelele majukwaani ,katika vyombo vya habari na kila kona jitihada za chama tawala CCM kujivua magamba.Pomoja na kuonekana wazi ya kua jitihada hizi za chama tawala zinaonekana ni za kisanii zaidi na kwa manufaa ya watawala na zisizo na tija kwa mtanzania wa kawaida,kwa serikali ya JK na chama tawala CCM inaonekana kana kwamba agenda namba moja ya kumkomboa Mtanzania!Nguvu zote za watawala zimejikita katika swala hili kuliko katika kampeni dhidi ya ukimwi,maralia au kero nyingi za walalahoi.Hivi kweli walalahoi wanatendewa haki katika hizi propaganda za chama tawala za kuwapotezea muda na kuwajaza matumaini hewa walalahoi?

  Watanzania tulitegemea hatua za kweli kuhusu swala hili la ufisadi "Kujivua magamba"Swala la ufisadi CHADEMA waliisha liainisha na kulivalia njuga na kuyataja maeneo na wahusika wa ufisadi na hii ni wazi kila mmoja wetu.Tulichokitegemea kwa JK na chama tawala CCM ni kuchunguza maeneo yaliotajwa na wahusika na kuchukua hatua za kuwafukuza katika chama na kuwafikisha katika vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake na chama CCM kuomba msamaha kwa walalahoi na kujihukumu kwa vitendo vyao.Kwani mafisadi ni sehemu ya chama chenyewe na wamekua wanafanya ufisadi huo chini ya mwamvuli na baraka za CCM.Vitu tunavyovishuhudia hivi sasa ndani ya CCM ni marumbano ya ndani wao kwa wao,kamati juu ya kama za kuwasuruhisha mafisadi,kupeana muda wa watuhumiwa kujiengua wenyewe,kauli za viongozi wa chama tawala zinazokizana kuhusu swala na hatua za kujivua magamba.Hii inakipotezea chama muda katika swala hili badala ya kushughulikia kero nyingine za wananchi na kuwajaza walalahoi matumaini hewa.

  Hii inatufanya tuhoji ukweli na dhana ya CCM kujivua magamba.CCM DON'T BEAT AROUND THE BUSH!TUANACHOKITAKA;MAFISADI WAFUKUZWE KATIKA CHAMA MARA MOJA,WAFIKISHWE KATIKA VYOMBO VYA SHERIA,CHAMA CHA CCM KITATHIMINI GHARAMA YA UFISADI HUU UMELIGHARIMU TAIFA KIASI GANI?NA UHALALI WA KIMAADILI KUWEPO MADARAKANI.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  wataweza si maneno tu kuwakebehi wananch wa tazania wakidhani kwamba enzi hizi ni kama miaka ya sabini wakati kila ktk watu 10 saizi at least 8 wamemaliza form 4 na wanauelewa mzuri juu ya haki zao
   
 3. M

  MAURIN Senior Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawawezi hata siku moja kudhubutu kumfukuza mtu ndani ya chama,mana ndani ya CCM hakuna aliyesafi hata mmoja,ukianza Mwenyekiti wao mpaka balozi wa nyumba kumi wote wachafu,kitengo cha proganda hakina nafasi tena kwenye jamii kwa sababu ukweli has been revealed even to the KIDS.FREEDOM IS COMING.
   
 4. makwimoge

  makwimoge JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakuna jinsi ya kufanya mambo yalikwisha kuharibika, kilichobaki sasa kwa 'sisiemu' ni kuvurugana tu na wamesau kuendesha Taifa.
  yalishassemwa kuwa inchi haitatawalika
   
 5. k

  kazuramimba Senior Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  si kweli mi nadhani CCM wamefanya kazikubwa sana na siku si nyingi kazi yao itaonekana.kujivua gamba kwa CCM ileweke sio usanii ni ''mpango mkakati wa kujiponya'' ambao tukiwa wa kweli umepunguza kelele za chura(CHADEMA) kumzua TEMBO(CCM) kunywa maji.
   
 6. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umesema kweli"Mpango mkakati wa kujiponya"Ukweli unabaki uleule hapa cha muhimu kwa CCM ni masilahi ya JK,Serikali yake na chama tawala CCM kwanza na sio walalahoi.Mkuu wanajidanganya kudhani kwamba usanii wa kujivua magamba umepunguza kelele za CHADEMA na walalahoi.Wanaendelea kukimbilia ukingoni na tunawabana ukutani mpaka kieleweke,wakijivua magamba bila sheria kuchukua mkondo wake bado tutaendelea kuwabana.Kwanza kitendo cha kukubali kujivua magamba inamaana yapo na sababu za kuyavua na ushahidi wanao.hivyo tutaomba ushirikiano wa kutoa ushahidi toka CCM mahakamani.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Usanii mtupu!
   
Loading...