Kujivua gamba: Vunjeni CCM yote sio kufukuza watu watatu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujivua gamba: Vunjeni CCM yote sio kufukuza watu watatu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Apr 28, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Hili swala la kijivua gamba naona kama ni mchezo wa kitoto, hii inatokana na ukweli kuwa ccm ina idadi ya viongozi wengi ambao wamekuwa kero na kikwazo kwa maendeleo ya chama hata nchi kwa ujumla. Kama kweli ccm ingekuwa na nia ya dhati nafikiri chama chote kingevunjwa na kuunda chama kipya, pengine kama wangefanya hili watanzania tungewaamini. Kusema wanaotajwa kwenye kashfa za kifisadi waondoke kwenye chama hiyo sio suluhisho la tatizo kwani kuna viongozi wengi mafisadi ambao hawajatajwa popote na wanaendelea kutafuna nchi kama mchwa, nafikiri hawa ndiyo wabaya kushinda hata hao mapacha watatu. Sitaki kuamini kuwa watu watatu tuu ndiyo Kikwazo kwa ccm naamini hawa ni kielelezo tu lakini tenga lote limechina. Kama mwalimu Nyerere alivyovunja chama alichokipenda TANU vunjeni ccm ili kizaliwe chama kitakacho rudisha heshima vinginevyo mimi naona ni kuimba shairi lisilo na ujumbe.
   
Loading...