Kujivua gamba kupo au la angalia kauli za Kikwete, Sumaye na Mukama ndiyo uamue | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujivua gamba kupo au la angalia kauli za Kikwete, Sumaye na Mukama ndiyo uamue

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Feb 6, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  “Haiwezekanitukaendelea kuwa na watu wa hovyo, lazima chama kijipange na kujiweka sawa ilikisipoteze sifa kwa jamii,” Jakaya Kikwete akiwa Mwanza jana. Anaongeza, "Hivi karibuni nikiwana NEC hapo Dodoma, nilitumia kauli ‘Nyoka Kujivua Gamba’. Usemi huo ulienezwatofauti kabisa. Kimsingi tulipitisha maazimio mengi, lakini wenzetu wameonaazimio moja tu la kujivua gamba.”
  “Hatuwezi kuwa nachama imara kama hatukuondoa magamba, mwenyekiti wetu wa chama taifa lazimatuyaondoe magamba yanayokipaka chama matope.” Fredrick Sumaye akiwa Pangani mkoani Jana.
  “Hata Waingerezawanatabia moja. Wakiona jambo linawasumbua, wanaunda Royal Commission, jambo hilolitachunguzwa kwa muda mrefu. Wakimaliza, watu wameshasahau,” Wilson Mukama katika mahojiano maalum na gazeti la Mwananchi wiki jana.
  Kwa kauli hizo hapo juu tutegemee nini?

   
 2. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kupo. Lakini kuna maana ya undani ambayo yatakiwa uitafakari. Swali ni hivi; Hivi Tanzania kuna wasomi wenye uwezo wa kuchukuwa nafasi walizo jivuwa hao wenye magamba?
   
 3. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Hii ni mpya! Ina maana kati ya watanzania milioni zaidi ya 40 hawezi kupatikana mtu wa kuchukuwa nafasi zao?
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Hiki ni kichomi!!
   
Loading...