Kujivua gamba kunatosha kumaliza matatizo yetu?

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
209
CCM wametutangazia dhamila yao ya 'kujivua gamba'. Nape amekwenda mbali zaidi kwa kututajia magamba husika kwamba ni Rostam Aziz, Edward Lowasa na Andrew Chenge. Nimekuwa nikijitahidi kutokushangaa hatua hii.

Swali kubwa nililonalo, hivi kujiondoa kwenye uongozi watu hawa (kujivua gamba) ndio mwisho wa matatizo yetu? Kwa nini Nape na wanasiasa wenzie wa CCM hawataki kuwa wakweli na kutueleza kuwa kujivua gamba ni njia yao ya kuficha kichwa na kiwiliwili chote kubaki nje?

Kama wanayo dhamila ya kweli sio tu watuhumiwa hawa wajivue gamba bali pia warudishe chenji yetu!
Chenji yetu ikirudi angalau tutafanya mambo ya maendeleo k.v. kujenga zahanati na shule.

Nawasailisha.
 
Back
Top Bottom