Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 5
Jamani Chenge kaachia ngazi,kafuata nyayo za Lowassa,Karamagi na Msabaha.Mpooo?
Mimi bado nashindwa kuelewa hao wanaompongeza chenge kama walivyompongeza Lowassa wana maana gani?kujiuzulu kwa kuwa fisadi siyo sifa hata kidogo jamani.
Kama kweli umeiba jiuzuli halafu rudisha ulichoiba ndipo kieleweke.Ninavyoelewa mimi kujiuzulu kwa maslahi ya taifa ina maana unawajibika juu ya matendo yako.Kwa mfano kama umepora mali ya umma unatakiwa kuwajibika kwa kurejesha.
Ikumbukwe kuwa Chenge alipohojiwa siku anarejea nchini alisema hawezi kujiuzulu kwa kuwa tuhuma hizi zililenga kumchafulia jina.Sasa ilikuwaje tena akajiuzulu?.Mimi mzee wa gumzo napata shaka hapa.
Naamini kuwa kauli aliyoitoa pale airport ilikuwa ya kwake lakini hatua ya kujiuzulu haikuwa matakwa ya chenge,ni shinikizo.Nani ajuaye labda ile kamati ya uongozi ya CCM ndiyo iliyomshinikiza afanye hivyo.
Kama ndivyo basi lazima tuamini kuwa kuna jambo nyuma ya pazia,si bure.Chenge anajua na CCM wanajua ukweli wote.
La msingi kwetu ni kujua hiyo fedha itarudi lini na ni kiasi gani.Hatutwezi kushangilia kujiuzulu kwa mtu eti akapumzike na mihela yetu,thubutu.
Lakini hata tukikataa nani anatusikia?
Tusubiri kuona nani mwingine atafuata,labda mzee wa gumzo?