Kujiuzulu kwa waziri zanzibar ni kwa makosa na udhaifu wa dereva kuhukumiwa kondakta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujiuzulu kwa waziri zanzibar ni kwa makosa na udhaifu wa dereva kuhukumiwa kondakta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Jul 24, 2012.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naipongeza hatua ya waziri wa mawasiliano na uchukuzi wa Zanzibar Kujiuzulu na kuwajibika kwa yaliyotokea kwa hili ni shujaa kwani kwa serikali yetu kitendo hiki ni nadra kutokea katika utawala wetu chini ya CCM.Madudu katika wizara ya nishati wakati wa Ngeleja ambayo yalikua wazi hakuwajibika mpaka kwa shinikizo la wabunge ambapoilimlazimu Rais JK kuvunja baraza la mawaziri na kulisuka upya! ili kumuondoa kiwavi huyu.Swala la madaktari na mambo mengine chungu mzima.Imefikia kuhoji tatizo liko wapi.Ni makosa kumuadhibu kondakta kwa makosa ya dereva aliesababisha ajali.TATIZO LETU SIO MAWAZIRI(MAKONDAKTA) TATIZO RETU NI RAIS JK KWANI NI YEYE ANAEWATEUA HIVYO ANAPASHWA KUWAJIBIKA,AJIPIME UALALI WAKE KUA KATIKA NAFASI HIYO JK NI JANGA LA TAIFA.MUNGU IBARIKI TANZANI
   
 2. N

  Nambombe Senior Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nampongeza huyu waziri kwa kuwajibika.Nadhani ipo siku atakuwa rais wa muungano wa Tanzania kwani mwinyi alijiuzuru
  vile vile na baadae akawa rais.
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kujiuzuru kwa waziri wa uchukuzi wa Zanzibar kama hatua ya kuwajibika baada ya kuzama meli ya SKAGIT in fundisho kwa serikali ya CCM kuwa accountability is part of a democratic process in a country that purports to practice good governance!! Wazanzibari kwa weli ni watu makini sana ukiwafananisha na wenzao wa bara ; hawa jamaa wana msimamo na mara nyingi sio wanafiki na kuwepo kwao kwenye muungano wa hivi na wenzao wa bara kumewapotezea nafasi nyingi katika maendeleo yao kama nchi!! Wazanzibari watakuwa na maendeleo ya kasi sana kama watajikomboa!!
   
 4. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  BIG up tunahitaji watz kama huyu jamaa ikiwezekana rais nae ajiuzulu tuitishe uchaguzi upya
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  ni uvivu wa kufikiri tu ndio utakuletea mawazo hayo!
   
 6. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Raisi wetu ana kasoro nyingi lakini embu kidogo tuache kila kitu kumtupia yeye au unataka kusema anaongoza hii nchi akiwa na birds eye view ya Tanzania na matatizo yake yoooote.

  Nadhani kuna vingine hata yeye mwenyewe anakuja kuvijua baada ya kuibuliwa na whistle blowers or the opposition parties ingawa response yake after receiving the facts ni dhaifu.
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama unadhani wewe una fikiri kuliko mimi nadhani unamapungufu kichwani mwako kama walivyo magamba wenzio; wazanzibari ni watu wenye msimamo kuliko wenzao wabara na hilo limejionesha hata pale bungeni Dodoma wanavyoonesha umoja wao kutetea maslahi ya nchi yao !! Kama hamuwahitaji wazanzibari kwenye muungano wenu kwanini mnawang'ang'ania waendelee kuwamo ilihali wao hawataki? Kwanini hamuitishi kura ya maoni muone umakini wao?
   
Loading...