Kujiuzulu kwa Ngeleja ndio suluhu ya mgao wa umeme? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujiuzulu kwa Ngeleja ndio suluhu ya mgao wa umeme?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamura, Oct 18, 2011.

 1. K

  Kamura JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vichwa vya habari vya magazeti mbalimbali ya leo vinasema "Zitto, Makamba wamkalia kooni Ngeleja" kimsingi wabunge hao wanataka Waziri huyo wa Nishati na Madini ajiuzulu kwa kile wanachosema kwamba ameshindwa kutatua tatizo la mgao wa umeme. Mmoja akisema maoni yake si ya kulenga kufikiriwa kupewa Uwaziri.

  Siamini kwamba kujiuzulu kwa Ngeleja ndiko kutaleta suluhu ya tatizo hilo. Kama wabunge hao wana mbinu za kutatua tatizo hilo wameshindwa nini kukaa na kijana mwenzao na kubadilishana mbinu za kutatua tatizo hilo? Kumsakama kwamba ajiuzulu mwarobaini wa ugonjwa huo. Wangekuwa wamekaa naye wakamweleza namna ya kutatua tatizo hilo akakataa ningeona logiki ya wao kumshitaki kwa wananchi.
   
 2. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Eh...!!
   
 3. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ngeleja hajui ni nini kinahitajika kutatua tatizo la umeme, ndio maana alikuja na muswaada wa kitoto bungeni wa kuomba hela ambazo zisingetosha hata kidogo kutatua tatizo la umeme bali alitaka hela za kula yeye na Jairo tu siku ziende mpaka Wabunge walipomrudisha na Midabwada yake wakamsaidie kurekebisha. Je anaweza kututatulia tatizo mtu wa namna hii!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ndio hajui wajibu wake!mtu mzima kazi yake kutoa takwimu za uongo juu ya utatuzi wa tatizo la umeme
   
 5. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,446
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  Hivi mgao wa umeme Tanzania umeanza Ngeleja akiwa waziri,kujiuzulu sio tiba.TATIZO LIPO KWENYE VYANZO VYA ENERGY.
   
 6. K

  Kamura JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama ni hivyo, Tanesco ifumuliwe.
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Angalau itakuwa ni kuonyesha uwajibikaji. tokea ameingia hali ya mgao imekuwa ikiongezeka badala ya kuwapo dalili za kupungua, takwimu zimetawala zaidi kuliko uhalisia wa kinachotokea, bora akapisha wengine. However aliyemteua naona yuko kimya akijua yeye c Mungu kufanya mvua inyeshe mtera,wanaelewana siasa zitaendelea
   
 8. K

  Kozo Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  • Acha kutoa majibu mepesi kiasi hicho,aliyekwambia kuwa tatizo ni vyanzo vya ENERGY kakudanganya na ww umeamini,hebu kuza ufahamu wako ili usilubunike kiwepesi na mabingwa wa udanganyifu kwa sababu ya uvivu wa kulitumikia Taifa kwa maendeleo ya Taifa na kutumika kwa ajili ya matumbo yao na tamaa zao.
   
 9. K

  Kamura JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Fafanua.
   
 10. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,446
  Likes Received: 7,185
  Trophy Points: 280
  hata aje YESU AWE WAZIRI WA ENERGY.KAMA TUNATEGEMEA MABWawa yajae ndo tupate umeme.MGAWO HAUTOKWISha kamwe.ndo nasisitiza Vyanzo ndo tatizo.
   
 11. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hajui kazi yake pale ndio maana hafanyi kazi vizuri
   
 12. K

  Kamura JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo siasa zimetawala hata kwenye masuala ya msingi. Binafsi nachelea kumrushia lawama Ngeleja kwa sababu Serikali hutoa ahadi kibao za kutoa fedha kwenye makaratasi na matamshi bungeni lakini ni wazito sana kutoa fedha hizo kwa wakati na wakati mwingine huwa hazitolewi kabisa. Si sekta ya nishati tu, zipo sekta kibao zinasuasua kwa sababu fedha ya kuziendesha hazitolewi.
   
 13. r

  raffiki Senior Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wambie kaka, mie mwenyewe nimeshangaa hata hao wanaoshikikiza wenzao wajuizulu wanasema tatizo ni kua uzalishaji wa umeme ni mdogo kuliko mahitaji ya umeme.

  Mbaya zaidi nao wanakuja na solution zao ambazo pia hazitatui matatizo, mmoja amesema eti pesa zilizokusanywa kutokana na mafuta ya taa yatumikayo hasa vijijini zitumike kupeleka umeme vijijini. na mwingine anayeshinikiza anasema Tanesco ugawanywe vipande 3 ndio solution ya umeme.

  SASa jiulize ndugu yangu hizo solution zao zinaongeza uzalishaji wa umeme?????kama wao walivyotabainisha kua tatizo ni MB ndogo??? Mie nawapongeza kwa kauli yao kua tuanze kuwajibika kwamba wanaoshindwa kutoa suruhisho la matatizo kama hilo la umeme wajiudhuru.

  Hivyo basi wao waanze kujiudhuru kwamaana nao hawajaja na solution ya tatizo bado hasa ukizingatia mmoja alikua kamati ya nishati katika serikali iliyopita, baada ya kujiudhuru na wanaowashinikiza nao wajiudhuru...then waachie nafasi wengine wenye uwezo watatue matatizo ya watanzania na sio matatizo binafsi.

  I remain 2b challenged nt
   
 14. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nijuavyo mimi Tatizo la umeme limekuwepo kwa kitambo sasa, hii inatokana na ukweli kwamba ni serikali ya awamu ya 1 tu iliyoweka mipango madhubuti ya kuwekeza. Awamu zingine zote zimekuwa zikija na mipango ya dharura, kitu ambacho naamini hakiwezi tatua tatizo hili sugu. But tujiulize je kuna dhamira ya kweli ya kuondoa mgawo wa umeme, foleni za dar es salaam,etc nakumbuka Bw Magufuli aliahidi kuondoa msongamano wa dar in 3 moon nilicheka na kustaajabu na ukweli u dhahiri. Tujiulize je wizara hizi zinapewa kasma ya kutosha kuondoa matatizo haya. Kama jibu ni yes basi Ngeleja awajibike, kama No basi wa kiwajibika ni serikali na wakuwawajibisha ni sisi kwenye saduku la kula.
   
 15. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kaka leo ndiyo wajua siasa kutawala kila kona ? Waasisi waujinga huu si ni CCM? Ngeleja kuondoka ni ishara kubwa ya uwajibikaji na kila mmoja ajue akikosea anaondoka hiyo solution one .Ngeleja ni mla rushwa nina ushahidi kwamba yeye na wezake hawako tayari kuona permanent solution iko kwa kuwa CCM wanakula huko .Bila vyanzo vya maji umeme unaweza kuwepo tena mwingi tu sina wasi wasi na hili sema ushabiki umewajaa nyie mafisadi hadi wa mawazo .
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jaribu kutumia akili yako vizuri.

  Zito na January si mawaziri wa nishati sasa unataka wajiuzulu ili wawajibike kwa lipi? Kazi yao ni kushauri na wamefanya hivyo mara kadhaa.

  Ngeleja ndiye waziri, anatakiwa kuhakikisha nchi ina umeme wa kutosha lakini miaka mitatu na ushee aliyokaa hapo tumeambulia giza, lazima ajiuzulu kuonyesha kuwajibika.
   
 17. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  tunataka uwajibikaji, unaposema kitatokea hiki kisipo tokea uwajibike kwa hilo!
   
 18. K

  Kamura JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa hiyo unamaanisha kwamba Ngeleja anafanya makusudi au amehongwa suluhu ya umeme ispatikane. Kwa nini ustoe huo ushahidi tumhukumu kwa haki?
   
 19. r

  raffiki Senior Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We ndio utumie akili, tatizo haufatilii wanasema nini unasoma kwenye magazeti na mtandao tu ulikuwepo siku ya mjadala star TV, walisema wao kama viongozi wa kamati wametua ushauri na njia za kutatua tatizo la umeme..na njia walizosema kubwa ni hizo nilizozitaja hapo juu ..na kwa nukuu ya maneno yao pia tatizo wamesema kama nilivyotaja hapo juu..sasa elewa sio kukurupuka tu...je hizo njia zao zinatatua tatizo wanalolisema wao pia??hiyo inamaanisha hata wao hawana jibu sahihi la kutatua tatizo la umeme sasa kwa kufuata wanaloamini kua kama mtu ukisshindwa uachie wengine hivyo basi nao wameshindwa na waachie wengine wapo wenye uwezo wa kutatua hilo yaweza kua wewe...sio tu kukazania ngeleja ajiudhuru wkt hata wao hawajatoa solution..Kama nayo inatakiwa iwe na mbinu mbadala za kutatua tatizo sasa haina nao wajitoe na ngeleja ndio ajitoe. Period.
   
 20. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Huyuu kaka ni mbabaishaji wala hajui kitu, hana uhakika na akiongeacho, ndo maana alienda Dar kumpongeza katibu wa wizara yake huku akimwacha bosi wake pinda anahangaika na bunge!
   
Loading...