Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa?

Wanabodi,

Siku zote, nabii huwa hakubaliki nyumbani, lakini sote tunakubali kuwa Mungu siku zote huwa anazungumza na watu wake, kupitia manabii, na nabii anaweza kuwa mtu yoyote hata usiyemtegemea. Japo mimi sii miongoni mwa manabii hawa wa Mungu, lakini kuna vitu huwa navisema, halafu vinakuja kutokea.

Sasa kwenye hili la Spika, kuna sauti niliisikia na nikasema humu!, angalia nilisema nini, na lini?

Bandiko hili pia ni bandiko la unabii

Je, wajua kuwa kitendo cha kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika, Mhe. Job Yustino Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili taifa letu Tanzania, tuachane na "Bora Spika" na badala yake tupate "Spika Bora". Swali ni Je CCM ituteulia "Spika Bora", au itaendelea na ule utaratibu wake wa ki CCM, kutupatia "Bora Spika" kama kawaida?. Unabii ni huu.​

Kama ni kweli, kujiuzulu kwa Ndugai, ni mpango wa Mungu, ili taifa letu lipate "Spika Bora", CCM ina wajibu wa kutupatia "Spika Bora" wa ukweli, kati ya hao waliojitokeza. Ikitokea CCM kututeulia "Bora Spika" mwingine, maana yake, huku kutakuwa ni kwenda kinyume cha mpango wa Mungu, hivyo CCM isipotuteulia "Spika Bora" na badala yake, ikatuleulia "Bora Spika" mwingine, this time around "Karma Itahusu..".​

Wasalaam.

Paskali.
Dr. Tulia amethibitisha huu mpango wa Mungu kwa Bunge la Tanzania. Spika Dr. Tulia, Mungu ambariki Sana.
Sasa Bunge ni Bunge Sheria Msumeno sio Bunge lile Bunge kujipendekeza, sasa ni Bunge sheria, Bunge heshima.
Big up sana Tulia.
P
 
Dr. Tulia amethibitisha huu mpango wa Mungu kwa Bunge la Tanzania. Spika Dr. Tulia, Mungu ambariki Sana.
Sasa Bunge ni Bunge Sheria Msumeno sio Bunge lile Bunge kujipendekeza, sasa ni Bunge sheria, Bunge heshima.
Big up sana Tulia.
P

Sasa tunahitaji Bunge lililochaguliwa Na watu sio hili la mwendazake
 
Uchaguzi wa Spika mpya, utafanyika kwenye kikao kijacho cha Bunge, ambapo vyama mbalimbali vya siasa, vitateua majina ya wagombea wake, kila chama mgombea mmoja. Hivyo Mtanzania yoyote, kutoka chama chochote cha siasa, aliyekidhi sifa na vigezo, anaweza kuwa Spika wa Bunge la JMT.

Lakini kwa siasa za Tanzania, tukubali, tukatae, ile kauli ya Mwalimu Nyerere kuhusu urais wa Tanzania, kuwa “rais bora lazima atatoka CCM”, ikingali inaishi hata kwenye Uspika, kuwa Spika bora wa Bunge la JMT, lazima atatoka CCM.

Kama nilivyouanza mwaka huu, katika salamu zangu mwaka mpya, kwa kusema huu ni mwaka wa mabadiliko, na kuwaomba Watanzania tubadilike, kujizulu kwa Spika aliyepita, ni mpango wa Mungu kuleta mabadiliko katika mhimili huu pia, baada ya Mungu kuleta mabadiliko kwenye mhimili wa Serikali, sasa ni zamu ya mabadiliko katika Mhimili wa Bunge, dini zote zinatusisitiza tushukuru kwa yoye, hivyo tushukuru hata kwa mabadiliko haya ya mkuu wa mhimili wa Bunge, baada ya kutokea fursa hii, ni jukumu la Bunge letu kutupatia Spika Bora.

Paskali.
Spika Tulia kaiva sana kwenye suala kutafiri Sheria, naangalia hapa Bunge live wanapitisha muswada wa tume ya uchaguzi naona anamtoa knout mpaka AG huyu dada ni balaa wabunge wote wanampigia makofi.

Mbeya tunasema Tulia mitano tena.
Naunga mkono hoja Hongera Spika Dkt. Tulia Ackson. Kuna haja MaSpika wetu iwe lazima kuwa Wanasheria?

Tena sio Tulia mitano tena bali 2025 could be ni Dr. Tulia!.
Angalia tulikotoka nae
1. Hivyo japo ni mimi niliyemtabiria Dr. Tulia uspika, Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

2. Fursa ya Spika mpya ilipojitokeza, niliwaomba CCM Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa?

3. Hivyo Dr Tulia aliposhinda nikamshauri Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!

4. Kwa vile Rais Samia amesisitiza 2025 twende na Mwanamke Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! wengi wanadhani Mwanamke wa 2025 ni lazima awe Rais Samia, anaweza kuwa ni Dr. Tulia!.
5. Sababu ya kwanini 2025 anaweza kuwa ni Dr. Tulia ni HII

P
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom