Kujiuzulu kwa mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Watanzania tunajifunza nini?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,579
20,879
Kujiuzulu kwa hiyari kufuatia mauaji ya watu 36 kwa waziri wa Kenya na mkuu wa jeshi la police kwa hiyari, Je! watanzania tunajifunza nini na watu wafanyao makosa ya dhahiri huku wakizidi kung'ang'ania madaraka?
 
kujiuzulu kwa hiyari kufuatia mauaji ya watu 36 kwa waziri wa kenya na mkuu wa jeshi la police kwa hiyari,je watanzania tunajifunza nini na watu wafanyao makosa ya dhahiri huku wakizidi kung'ang'ania madaraka?

waziri wa ulinzi amefukuzwa na mkuu wa polisi amejiuzulu ....mkiwa mnaandika habari kama hizi muwe mnaweka source
 
Hata hivyo wamechelewa sana!! Ingekuwa kwa wenzetu siku nyingi sana wangekuwa wameshapumzika.
 
Mifano hai tunaiona kila siku lakini viongozi wetu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.

Wana uchu mno linapokuja suala la madaraka
 
kuna nchi zingine bhana watu wako serious nandhani pia kuna mwaka fulani mkuu wa polisi kenya alifukuzwa kazi na kuwa mkuu wa posta kama sijasahau vile.
 
Mabomu yalilipuka Mbagala na Gogolamboto na kuuwa watu wengi na wengi kujeruhiwa na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali, hakuna yeyote aliyewajibika. Pale Gogolamboto hakuna fidia yeyote iliyolipwa kwa waathirika hadi sasa.
 
Kujiuzulu kwa hiyari kufuatia mauaji ya watu 36 kwa waziri wa Kenya na mkuu wa jeshi la police kwa hiyari, Je! watanzania tunajifunza nini na watu wafanyao makosa ya dhahiri huku wakizidi kung'ang'ania madaraka?

Mkuu fuatilia gazeti la Nation kwenye mtandao. Rais Kenyatta kaona utaratibu kumuwajibisha kikatiba ni ngumu kamwambia ajiuzulu mwenyewe wakiwa uso kwa uso. Waziri kamtimua tu na kumtangaza mwingine hapo hapo.
Bongo utasikia haondoki mtu na rais yupo tu
 
Kenyatta hana akili kweli.anaamini akimfukuza huyo kiongoZi al shabab watapunguza mauaji.
 
Kuondoka mpaka watu wameandamana angejitoa zamani madarakani, hakuna la kujifunza hapo, ni wale wale tu
 
Mabomu yalilipuka Mbagala na Gogolamboto na kuuwa watu wengi na wengi kujeruhiwa na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali, hakuna yeyote aliyewajibika. Pale Gogolamboto hakuna fidia yeyote iliyolipwa kwa waathirika hadi sasa.

David Mwangosi alipigwa bomu wazi wazi lakini bado kuna wasengerema wanabembea kwenye viti vya ofisi. Na mbaya zaidi wanahabari wenzake wamekaa kimya.
 
Watanzania na waafrica ni wabinafsi na uongozi ni sehemu ya kutajirikia na kuwajibika kwa manufaa ya nchi. Hilo ndilo tujifunzalo
 
Watanzania na Waafrica ni wabinafsi na uongozi kwao ni sehemu ya kutajirika na tendo la kuwajibika kwa manufaa ya nchi sio sehemu yet. Hilo ndilo tujifunzalo
 
Back
Top Bottom