Kujiuzulu kwa mawaziri bila ya anayewatua kuwajibika ni mchezo wa kuigiza

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Ifike wakati bunge liache kuzunguka katika kutoa maamuzi yake,waziri mkuu aliyeteuliwa na rais wa awamu ya nne mh. E Lowassa aliwajibishwa kutokana na sakata la ufisadi kwa kusimamia mikataba tata ya kuzalisha umeme,akamteua mh. Pinda naye amekumbwa na misukosuko mingi kutokana na matamko yake yanayoashiria uvunjifu wa amani.Miongoni mwa kauli zake ni pamoja na wanao ua ALBINO nao wauwawe,akalia machozi bunge likamsamehe,waziri mkuu huyu ana kesi ya jinai ndani ya mahakama kuu dhidi ya kauli yake ya waache wapigwe tu maana wametuchoshwa.Pamoja na hayo yote serikali hiyo hiyo ikaendelea kumtetea na kushindwa kumwajibisha. Linakuja suala la katiba ya JMT ambayo inatamka wazi kuwa waziri mkuu atatekeleza yale yote yatakayoamriwa na rais aliyemteua.Kuna vikao vya baraza la mawaziri ambalo rais wa nchi ndiye M/kiti wa baraza hilo katika kufanya maamuzi magumu ya kitaifa,ni kawaida maazimio ya serikali huanzia kwenye vikao vya baraza la mawaziri ambalo katibu mkuu kiongozi ndiye katibu wa baraza hilo,kwa mantiki hiyo basi utaona kumwajibisha waziri mkuu pekee yake na mawaziri mizigo hakutoshi kwani utendaji wao una Baraka zote toka kwa M/kiti wa baraza hilo ambaye ni rais wa nchi. Cha msingi sasa,ni wakati sasa wa bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais kutokana na kuteua aina ya watendaji ambao mwisho wake wanavurugwa na kufanya maamuzi ya kiimla,lakini pia huwezi kuwa na serikali dhaifu rais akabaki salama,rais ndiye mkuu wao,ameshindwa kuwasimamia watendaji wake akiwa kama overseer atawezaje kutuongoza ilihali serikali yake imekiuka haki za usawa wa binadamu. Wabunge waache kutafuna maneno,tunaomba hoja iwasilishwe ya kutokuwa na imani na rais mara moja vinginevyo tutaamini kinacho fanyika ni changa la macho.Tumechoshwa na siasa zile zile za ndani ya bunge,sasa tunataka vitendo.
 
CCM mpasuko na mgawanyiko mkubwa,yaelezwa ndo mwisho wao.Anguko lao latimia.CHADEMA kuchukua nchi
 
Tatizo ni JK lakini nani atamvalisha paka kengele?
 
CCM mpasuko na mgawanyiko mkubwa,yaelezwa ndo mwisho wao.Anguko lao latimia.CHADEMA kuchukua nchi

Kila mahali hivi sasa ni mipasuko tu. Umesahau CDM wamesahau CCM sasa hii wanashughulikia kujisafisha na kashfa ya kumdhulumu kamanda wao Zitto kabwe?
 
Hakuna serikali watanzania tukubali maumivu ya kupotea chini ya miaka kumi wanawake wakome na maneno cheupe na kumimina kura nadhani wameyapata sasa mlo moja kwa siku
 
Kila mahali hivi sasa ni mipasuko tu. Umesahau CDM wamesahau CCM sasa hii wanashughulikia kujisafisha na kashfa ya kumdhulumu kamanda wao Zitto kabwe?

Zitto kasha kuwa historia kwenye siasa za nchi hii alidhani anaweza kuwapanda magwiji wa siasa za nchii na wananchi mwache ale alichovuna amebaki kujitamba na nembo za chadema vichwani hana pa kwenda walimfanya aache kupalura migebuka hao
 
Pinda atalia sasa hivi yatampata ya Jairo ha ha KIkwete anavunja baraza la mawaziri mara nne katika miaka kumi inamaana sio kiongozi hajui kuongoza na ni dhaifu
 
kwa sasa nikuwajibika kwenda mbele chama sasa kimeshika hatabu waziri na watendaji wa serikali lazima wajipange kutenda kazi nzuri.
 
kwani jk ndiyo huenda wizarani kutenda kazi wewe mgonjwa kweli unawezaje kumtuhumu jk kwa wizara tatu wakati anao mawaziri wengi na wizara nyingi.

Muungwana mwa... siamini kama upeo wa akili yako umeishia hapo?

Tatizo la nchi hii ni JK akiwa ndo mwenye madaraka yote ya nchi...
 
kwani jk ndiyo huenda wizarani kutenda kazi wewe mgonjwa kweli unawezaje kumtuhumu jk kwa wizara tatu wakati anao mawaziri wengi na wizara nyingi.

the buck stops with the president, period! Hawezi kuwa anafanya maamuzi feki waliochini yake waadhibiwe yeye aendelee kutesa tena anatakiwa kuliomba taifa msamaha kwa yote haya. Wasaidizi wake wanawajibika kwa makosa ya waliochini yao na yeye lini ataanza kuiga mfano wa uwajibikaji?
 
Zitto kasha kuwa historia kwenye siasa za nchi hii alidhani anaweza kuwapanda magwiji wa siasa za nchii na wananchi mwache ale alichovuna amebaki kujitamba na nembo za chadema vichwani hana pa kwenda walimfanya aache kupalura migebuka hao

Lakini anawake pia wanaomuona ni shujaa wao............
 
Tumeona,tumesikia na tunasubiri kuona maamuzi ya ushauri wa kamati ya bunge iliyochunguza sakata Zima la Operation Tokomeza yanatekelezeka kama wabunge walivyopendekeza. Hatutegemei kuona kuwa wamefunika kombe mwanaharamu apite kwa kuwafanya kafara baadhi yao ilihali kiranja mkuu wao ni muathirika wa utendaji wake mkuu katika kusimamia utendaji wa kila siku wa serikali. Tumechoshwa na blabla zisizo na tija kwa taifa,tunataka utendaji mbovu wa serikali sikivu usichukuliwe kwa pupa kwani ni suala la mfumo mzima ambao bila maamuzi magumu kufanyika itakuwa ni sawa kunawa uso huku matongo tongo yakibaki machoni. Bunge lisiishie hapo,uwajibikaji wa pamoja ndiyo misingi ya utawala bora,bunge lihakikishe KILONGOLA Pinda naye anafuata nyayo za wenzake ili kupisha bwana mkubwa aweze kuunda serikali yenye lengo la kuwafikisha angalau hatua moja ya matumaini Watanzania. Pia ni nafasi ya bunge kutafakari kwa kina juu ya imani yao kwa rais,kwani haiwezekani akili ile ile ya mtu yule yule ndani ya serikali ile ile inayoendeshwa kwa mfumo ule ule iunde serikali inayoweza kuwajibika kwa wananchi,kama kweli bunge limeamua kuwa la kizalendo lifike mbali zaidi ya kumwajibisha waziri mkuu
 
kwani jk ndiyo huenda wizarani kutenda kazi wewe mgonjwa kweli unawezaje kumtuhumu jk kwa wizara tatu wakati anao mawaziri wengi na wizara nyingi.
wewe unaona mawaziri watatu ni wachache!!!kumbuka si hawa tu kuna wengine waliwahi kuachia ngazi huko nyuma!nadhani tuwe fair anayewachagua hawa mawaziri hayuko serious au la basi vigezo anavyotumia kuwapata si sahihi!
 
kwani jk ndiyo huenda wizarani kutenda kazi wewe mgonjwa kweli unawezaje kumtuhumu jk kwa wizara tatu wakati anao mawaziri wengi na wizara nyingi.
Tuwe wa kweli ndugu zangu wana jamvi,huwezi kuwa na familia yenye maadili ikiwa msimamia maadili una kimbia majukumu yako ya kiutendaji kwa misingi ya kumsakizia mama eti ndiye anayeshinda kutwa nzima na familia.Upo wapi umuhimu wa vikao vya semina elekezi kama sio aina nyingine ya ufisadi katika kutafuna pesa za walipa kodi.Huwezi kuwa kiongozi wa kushinikizwa kama vile huna macho ya kuona,tumeona ndani ya awamu hii ya nne bunge kwa mara ya tatu linamshinikiza rais kuwawajibisha mawaziri wake,ikiwa yeye ndiye overseer na haoni kuna haja gani ya kuwa na makengeza ya maamuzi kwa wananchi kupitia kwa wabunge wao.Ni wakati sasa wa Mr. safari kupumzika kupisha wenye commitment na matatizo ya Watanzania na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom