sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Ifike wakati bunge liache kuzunguka katika kutoa maamuzi yake,waziri mkuu aliyeteuliwa na rais wa awamu ya nne mh. E Lowassa aliwajibishwa kutokana na sakata la ufisadi kwa kusimamia mikataba tata ya kuzalisha umeme,akamteua mh. Pinda naye amekumbwa na misukosuko mingi kutokana na matamko yake yanayoashiria uvunjifu wa amani.Miongoni mwa kauli zake ni pamoja na wanao ua ALBINO nao wauwawe,akalia machozi bunge likamsamehe,waziri mkuu huyu ana kesi ya jinai ndani ya mahakama kuu dhidi ya kauli yake ya waache wapigwe tu maana wametuchoshwa.Pamoja na hayo yote serikali hiyo hiyo ikaendelea kumtetea na kushindwa kumwajibisha. Linakuja suala la katiba ya JMT ambayo inatamka wazi kuwa waziri mkuu atatekeleza yale yote yatakayoamriwa na rais aliyemteua.Kuna vikao vya baraza la mawaziri ambalo rais wa nchi ndiye M/kiti wa baraza hilo katika kufanya maamuzi magumu ya kitaifa,ni kawaida maazimio ya serikali huanzia kwenye vikao vya baraza la mawaziri ambalo katibu mkuu kiongozi ndiye katibu wa baraza hilo,kwa mantiki hiyo basi utaona kumwajibisha waziri mkuu pekee yake na mawaziri mizigo hakutoshi kwani utendaji wao una Baraka zote toka kwa M/kiti wa baraza hilo ambaye ni rais wa nchi. Cha msingi sasa,ni wakati sasa wa bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais kutokana na kuteua aina ya watendaji ambao mwisho wake wanavurugwa na kufanya maamuzi ya kiimla,lakini pia huwezi kuwa na serikali dhaifu rais akabaki salama,rais ndiye mkuu wao,ameshindwa kuwasimamia watendaji wake akiwa kama overseer atawezaje kutuongoza ilihali serikali yake imekiuka haki za usawa wa binadamu. Wabunge waache kutafuna maneno,tunaomba hoja iwasilishwe ya kutokuwa na imani na rais mara moja vinginevyo tutaamini kinacho fanyika ni changa la macho.Tumechoshwa na siasa zile zile za ndani ya bunge,sasa tunataka vitendo.