Kujiunga na Jeshi kwa mujibu wa sheria

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
4,015
5,397
Wanajamvi,

Miaka ya nyuma ili upate ajira serikalini au upate kuendelea na masomo ya elimu ya juu,ilikuwa ni lazima uende jeshini kwa mwaka mmoja JKT ili kujitolea kulijenga taifa,kujifunza mbinu za medani na za kivita na kuhitimu kama askali wa akiba.

Katika kipindi cha mwaka mmoja, vijana wa kitanzania kutoka mikoa yote ya nchi yetu walikusanyika katika makambi yote ya JKT ili kujitolea katika ujenzi wa taifa.

Utaratibu huu mzuri ambao kwa sasa sina hakika kama unaendelea uliweza kwanza, kuondoa zile tabia za ubinafsi,dharau,ukabila,umwinyi na uvivu na badala yake kuwafundisha vijana nidhamu ya kazi utii na uzalendo na kuwa tayari kuzikabiri changamoto za maisha kwa ujasiri na weredi.

Naamini katika jukwaa hili wapo waliopitia hatua zote za utaratibu huu mimi nikiwa mmojawapo na ningependa kwa kupitia uzi huu tukumbushane yale tuliyopitia ili wale ambao hawakuwahi kupitia huko waweze kujifunza. Karibuni.
 

Attachments

  • YALIYOPTITA SI NDWELE.docx
    17.1 KB · Views: 62
Mimi nimejifunza kwamba naweza kufanya kila kazi, nimegundua kuwa mwanadamu ni dynamic, woga wa kila aina hauna nafasi kwangu.
JKT ni nzuri ila kwa siku hizi wacheki upya mifumo , kijana anapitia jkt anarudi mtaani anakosa mkopo , wazazi sometimes hawawezi kuwalipia wanao ada za chuo kijana anabaki dilemma huku kuchezea SMG, SRA, LMG, AK47 n.k anajua! What will happen?
 
Nyerere alikuwaga na akili sana,, sasa nashangaa eti siku hizi kuna mapumbavvvv pumbavvvv tu eti nayo yanafananishwa na Nyerere! Kama nilisikia jamaa limejiita J.K. Nyerere likaenda hata kuapa mahakamani eti libadilishe jina kabisa! Yaani jitu unaliona kabisa busara kichwani ni Bashite eti nalo linalazimisha lifananishwe na Nyerere!!
 
Back
Top Bottom