Kujitoa ufahamu ni mbinu pekee inayomsaidia mtu kupata cheo kwenye Serikali za Kiafrika

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Kwanza nianze kwa kueleza maana ya msamihati huu ambao unatumika sasa katika nchi inayotumia lugha ya kiswahili kwa ufasaha mkubwa, KUJITOA UFAHAMU...msamihati huu una maanisha, UNAFIKI. Kati ya mambo aliyoyachukia Bwana Yesu ni UNAFIKI. Mnafiki ni mtu anayevaa sura ya bandia huku akificha sura yake halisi, maana yake ni mtu anayejifanya asivyo.

a person who pretends to have virtues, moral or religious beliefs,principles, etc. that he or she does not actually possess, especially a person whose actions belie stated beliefs.

a person who feigns some desirable or publicly approved attitude,especially one whose private life, opinions, or statements belie his or her public statements.

a person who puts on a false appearance of virtue or religion
a person who acts in contradiction to his or her stated beliefs or feelings


Sitaki niwapotezee muda, niende kwenye mada yangu. Njia pekee ya kuweza kupata cheo katika serikali za nchi zetu za Kiafrika ni kujitoa ufahamu au kuwa mnafiki. Siwezi kuanzia kwenye nchi zingine naanzia katika nchi yangu Tanzania. Huu ndio ukweli usiopingika usipojitoa ufahamu kamwe huwezi kuteuliwa kwenye awamu hii ya tano.

1-Huku ndio kujitoa ufahamu kusikokuwa na kiwango, hivi tangia uhuru ni chama gani kimeongoza nchi yetu?
Je mafisadi wote wanaotajwa nchini wametokana na utawala wa chama gani? mikataba yote mibovu inayolalamikiwa imesainiwa na serekali ipi?
kama siyo kujitoa ufahamu kuna sababu ya kuwalalamikia wapinzani kuwa wanawapokea mafisadi?
hivi serikali inashindwaje kuwakamata hao mafisadi waliokimbilia upinzani?
Kama siyo kujitoa ufahamu unawezaje kuwachukia wapinzani ambao hawakuzalisha mafisadi na kuwapenda ccm waliozalisha hao mafisadi?
Hivi kama siyo kujitoa ufahamu unawezaje kukichukia kioo kinachokuonyesha kama makeup imekaa vizuri na kumkumbatia anayekupaka uchafu?
Uovu wote unaolalamikiwa na utawala wa awamu ya tano umezalishwa na serikali ya ccm na wakiwemo hao wanaolalamika. Kama siyo kujitoa ufahamu unawezaje kuwalazimisha wapinzani wabaki na agenda moja tu ya ufisadi, huku ukizuia mikutano ya hadhara ambao ni uwanja wa kuwaambiwa wananchi uovu wa serikali?
Kama siyo kujitoa ufahamu unawezaje kuwataka wapinzani wawe wanaimbia pambio za kupongeza wakati wanaona nchi inaelekea pabaya?

Kaka yangu N muda simrefu utarudishwa kwenye ulaji maana njia pekee ni kukubali kuwa mnafiki wa kukubaliana na kusifia hata lile jambo unaloona halifahi. kidogo kidogo umeanza

Kwa kuwa watu bado wamejitoa ufahamu wanasifia sana serikali ya awamu ya tano, ila ufahamu ukirudi kama Zimbabwe utashangaa hao ndio wataanza kusema tumechoka. Mnakumbuka vijana wa Zanu ambao walikuwa wanamkingia kifua Mugabe ila ufahamu uliporudi walijazana barabarani na mabango ya kumtaka Mugabe aondoke.

Pale Uganda wapo ambao wamejitoa ufahamu kwa kumshabikia Mzee wao na kutaka katiba ibadilishwe ili ukomo wa miaka uondolewa ufahamu ukirudi watakuwa wa kwanza kubeba mabango.

Pale DRC Congo wapo waliojitoa ufahamu na kumsaidia Kabila kwa hali na mali ila ufahamu ukirudi watamwita kabila majina yote ya kashfa.

Ili uweze kupata cheo kwenye serikali nyingi za kiafrika ni kujitoa ufahamu na kuwa mnafiki wa kusifia na kukubali kila kinachofanywa na watawala wa nchi husika.

Hapa tulipofikia na umaskini wote huu umesababishwa na serikali ya ccm msijitoe ufahamu kutetea. Kwa nini ccm mkituomba radhi watanzania mtapungukiwa nini? kwa nini mnataka kuamishia lawama kwa wapinzani?
 
Kujitoa ufahamu ili mradi mkono uende kinywani! Unakuta profesa mzima anajitoa ufahamu na kukubaliana na kauli za hovyo! Mifano toeni wenyewe maana Kwa bongo iko chungu mzima!
 
Kujitoa ufahamu ili mradi mkono uende kinywani! Unakuta profesa mzima anajitoa ufahamu na kukubaliana na kauli za hovyo! Mifano toeni wenyewe maana Kwa bongo iko chungu mzima![/QUO

Hahaha Mkuuu sisi wote tumejitoa ufahamu kila kitu twasifia!!!!
 
Back
Top Bottom