Kujitoa muhanga ni pamoja na wabunge kupunguziwa mishahara na mafao yao

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Juzi nimemsikia mbunge wa ilala bwana Zungu akiipigia debe kodi ya uzalendo. Binafsi siiungi mkono kodi hiyo kwani wananchii tuna kodi nyingi sana tunalipa pamoja na uchumi wa wananchi kuwa ni duni.

Pendekezo langu kwa wabunge nawashauri kwa kuwa wao ni wawakilishi wa wananchi basi waanze wao kutuonyesha uzalendo kwa kukubali kupunguziwa mishahara yao na mafao kwa asilimia 15% tu ili fedha hizi ziwe zinaenda kwenye miradi ya maendeleo ya majimbo yao na baada ya miaka 5 yale mafao yao nayo yakatwe asilimia 20%ili nazo ziende kwenye majimbo yao kwani ndiyo yaliyowawezesha wao wabunge kuvuna mafao hakika huo utakuwa uzalendo wa kujitoa muhanga kwa wabunge wetu.
 
Naunga mkono,haiwezekani mtu kikao kimoja tuu anapokea mshahara wa mwalimu tena bila makato...yaani ndani ya mwezi mmoja wa vikao mtu anapokea mshahara 2a mtumishi mingine wa mwaka na nusu...wacha watuchukulie mademu zetu mtaani maana hakuna jins.
 
Wabunge 100% ni wa CCM, na tunavyojua CCM ina nia ya dhati kabisa kuwaletea wananchi maendeleo - sasa hili la kuwapunguzia wabunge mafano na mishahara yao limekuja muda muafaka.

Naunga mkono hoja !!
 
Yule mzee basi tu, nashauri sio tu wakatwe bali mishahara yao ipunguze hadi alau milioni 4.5 kwa mwezk ni nyingi sana haoo ndipo watajua maana ya maisha magumu na sio kwa kejeli wanazowafanyia watanzania
 
Wabunge 100% ni wa CCM, na tunavyojua CCM ina nia ya dhati kabisa kuwaletea wananchi maendeleo - sasa hili la kuwapunguzia wabunge mafano na mishahara yao limekuja muda muafaka.

Naunga mkono hoja !!
Bilashaka watatekeleza hili kwa ukamilifu😅😅
 
Nitawaona wabunge hawa wa ccm ni wazalendo kwa nchi yao kama watakubali k mishahara yao ikatwe kodi kama wafanyakazi wengine.

Tofauti na hapo tutaendelea kuwaona ni sawa na mafarisayo wanawabebesha watu mizigo mizito ambayo wao hawataki hata kuigusa kwa ncha ya vidole vyao.
 
uzalendo ungeanzia kwenye mishahara yao na posho zao sidhani kama wananchi wa kawaida wangelalama.
 
Walipoamua waitwe "waheshimwa" kabla ya kutajwa kwa majina yao na kuliepuka neno "ndugu" kama ilivyokuwa imezoeleka hapo awali, na kama ilivyo kwa wananchi wengine, walikuwa wanamaanisha wao ndiyo ni "walaji wa kodi" na wala sio "walipa kodi".
 
Sasa kama mbunge mwanamke anauliza WANAUME MPO? wafanyaje hao wanaume
 
Back
Top Bottom