Kujitoa kwenye uchaguzi dakika za mwisho

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,404
9,233
Bila shaka wengi tumeshasikia baadhi ya maeneo ya nchi wagombea wanavyojitoa dakika za mwisho bila kuwa na sababu za msingi. Hii inadhihilisha ni jinsi gani CCM umedhamilia kushinda kwa KUSHINDWA na kuamua kuwahonga wagombea wa upinzani ili wajitoe na kuonekana wamepita bila kupingwa. Hizi si dalili nzuri kwa upinzani na kwa hili nawalaumu wapinzani kwani kuna baadhi ya maeneo wagombea wameokoteza tu kwa waliokuwa wanachama wa CCM na kuwaweka wagombee bila kuandaliwa ipasavyo.
Hivi hakuna mahala ambapo tunaweza kuwashtaki hawa waliojitoa dakika za mwisho?
 
Nadhani ni fundisho vyama kuhakikisha wanasimamisha watu ambao ni patriots wa kweli!
 
Hawa wakipewa adhabu na wale waliomtegemea kuwawakilisha ki-silencer ndio muarubani. Lazima kuweka mazingira ya watu kuhofu usaliti.
 
Inakoelekea ni kipigo tu kwa wasaliti, hvi utamfanya nini kingine msaliti, we negotiate with them? UMMA UTAAMUA
 
Back
Top Bottom