Kujitoa EU: Wanasiasa wa Uingereza walivyowadanganya wananchi wao

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kama kawaida ya wanasiasa huwadanganya wananchi kwa maneno matamu wakati wa kampeni, halafu kampeni zikiisha yale yale waliyoyasema na kuyakampenia wanaanza kuyakana na kugeuka!

Uingereza ni mfano mzuri ile kampu ya Brexit au kundi ambalo lilikuwa linakampenia kujitoa Uanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) uliwaahidi Waingereza mambo kibao ambao wananchi walivutiwa nayo wakajitikoeza kwa nguvu kuwapa kura sasa kura wameipata Uingereza inatakiwa iondoke EU wanasiasa wale wale wanakuja kukana yale ambayo waliwaahidi wananchi wao, inanikumbusha chadema na ufisadi wa Lowasa, alikuwa fisadi mpaka siku alivyohamia chadema baada ya hapo ikawa Lowasa siyo fisadi bali tatizo ni mfumo, lkn Mungu anatupenda WatanZania akatupa hekima na tukaona huu udanganyifu na utapeli na kuwapotezea hawa mafiozo chadema/ukawa!

Ndiyo maana nampenda raisi Magufuli, kwa maana anasema na kutenda, na siyo blah blah kama wanasiasa wengine, hakika Raisi Magufuli ndiyo Raisi bora World over nina imani Waingereza wangependa kuwa na raisi kama Magufuli wetu, aliyotuahiddi kwenye kampeni ndiyo anayoyafanya!

3,w=650,c=0.bild.jpg
 
Magufuli katokea wapi tena na Mambo ya Brexit ?

Ngoja na mimi nichanganye mengine naona ishakuwa mazoea ya Watanzania... tumekuwa kama Waarabu baya lolote likitokea huwasingizia Waisrael kuwa ndio wamehusika...
 
Kama kawaida ya wanasiasa huwadanganya wananchi kwa maneno matamu wakati wa kampeni, halafu kampeni zikiisha yale yale waliyoyasema na kuyakampenia wanaanza kuyakana na kugeuka!

Uingereza ni mfano mzuri ile kampu ya Brexit au kundi ambalo lilikuwa linakampenia kujitoa Uanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) uliwaahidi Waingereza mambo kibao ambao wananchi walivutiwa nayo wakajitikoeza kwa nguvu kuwapa kura sasa kura wameipata Uingereza inatakiwa iondoke EU wanasiasa wale wale wanakuja kukana yale ambayo waliwaahidi wananchi wao, inanikumbusha chadema na ufisadi wa Lowasa, alikuwa fisadi mpaka siku alivyohamia chadema baada ya hapo ikawa Lowasa siyo fisadi bali tatizo ni mfumo, lkn Mungu anatupenda WatanZania akatupa hekima na tukaona huu udanganyifu na utapeli na kuwapoteza hawa mafiozo chadema/ukawa!

Ndiyo maana nampenda raisi Magufuli, kwa maana anasema na kutenda, na siyo blah blah kama wanasiasa wengine, hakika Raisi Magufuli ndiyo Raisi bora World over nina imani Waingereza wangependa kuwa na raisi kama Magufuli wetu, aliyotuahiddi kwenye kampeni ndiyo anayoyafanya!

3,w=650,c=0.bild.jpg
Hahahahahahah hamkutegemea !Ndo ivo deal done no kuchakachua.Huwezi kulinganisha siasa za huko na huku never!!!
 
Kwa hiyo unadhani na Waingereza nao wanadanganywa kwa Tshirt na kofia?

Katika mifano yooote ukaona mmoja tu wa UKAWA, ila umesahau kuwa mwenzenu mmoja aliyekuwa Mwanaharakati wakati wa Katiba Mpya aliwahi kusema kuwa DC na RC ni mzigo wa bure kwa mwananchi, leo hii ni DC.

Mimi sioni kama una kichwa cha kuchambua siasa ya nje. Propaganda za kisomi sio level yako. Wewe kaa hapa hapa uhubiri sukari kushuka bei next year
 
hakika Raisi Magufuli ndiyo Raisi bora World over nina imani Waingereza wangependa kuwa na raisi kama Magufuli wetu, aliyotuahiddi kwenye kampeni ndiyo anayoyafanya!
kweli kazi ipo.............British ''Republic'' has never had such thoughts.
 
kweli kazi ipo.............British ''Republic'' has never had such thoughts.

Ni kwa sababu tu hawamfahamu Raisi Magufuli lkn leo hii ukienda ukawaambia Waingereza aina ya Raisi tuliye naye ambaye anafanya yale yaliyaahidi nina uhakika zaidi 70% wangependa wawe na Raisi kama Magufuli wetu!
 
Ni kwa sababu tu hawamfahamu Raisi Magufuli lkn leo hii ukienda ukiwaambia Waingereza aina ya Raisi tuliye naye ambaye anafanya yale yaliyaahidi nina uhakika zaidi 70% wangependa wawe na Raisi kama Magufuli wetu!
kwanini umefikiri Waingereza wangependa kuwa na ''rais'' kama Magufuli...?Kwa nini Rais na si Kiongozi?...
 
Kama lengo lako lilikuwa ni kuongelea ukawa swala la uingereza linaingiaje hapa. Tatizo la watanzania ni kujenga hoja na akaitetea hoja hiyo kwa kuipa maneno ya afya. Na ndiyo maana tunazidiwa maarifa na wenzetu wa nchi jirani. Hii ingekuwa interview tayari umefeli.
 
kwanini umefikiri Waingereza wangependa kuwa na ''rais'' kama Magufuli...?Kwa nini Rais na si Kiongozi?...

Vyovyote vile unavyopenda kuliita hilo, neno lkn ukiwaonyesha mambo anayoyafanya Magufuli wetu yaani kuongoza kama alivyoahidi kwenye Kampeni, ni dhahiri wangependa kuwa naye, hiyo ni human nature!
 
kwanini umefikiri Waingereza wangependa kuwa na ''rais'' kama Magufuli...?Kwa nini Rais na si Kiongozi?...

Fanya flashback ya posts za jamaa kwanza kabla hujapoteza muda kujibizana naye.

Yuko kwenye Payroll ya chama kwa hii kazi.
 
Tatizo lako nahisi unafikiri kwamba Wazungu ni Superhuman kumbe usichokijua nao ni ****** tu kama wananchi wengine na wanadanganywa na kutumiwa kwa manufaa ya Wanasiasa kama watoto wadogo, tofauti ni kwamba tu wao wameanza kudanganywa muda mrefu sana karne hadi karne tangu enzi za middle ages huko na sasa uongo wa wanasiasa wao umebadilika kulingana muda na mazingira yao, lkn mwisho wa siku uongo ni ule ule tu, na mfano hai huwo niliokupa, upande wa Brexit waliwaahidi Waingereza kwamba wakipiga kura ya HAPANA basi Uingereza inajitoa mara moja, wamefanya hivyo sasa wanawageuka na hawataki kujitoa tena haraka bali wanataka majadiliano na EU na yale yote waliyoyaahidi wanasema kuayafanya mara moja sasa wanasema yanazungumzika, kwa mfano waliahidi fedha ambazo Uingereza inachangia kapu la EU wataipeleka kwenye afya leo hii wanapinga ...

Suala la superhuman hilo lako. Nilichokukumbusha ni kuwa hawakai wakajadili kwa mtindo huo unaohanikiza hapa. Unajifanya kunijibu nusu, kwani nusu ya pili ya comment yangu hukuiona?

Wewe achaga kujitoa fahamu. Waingereza wanataka demokrasia ndio iwaongoze, sio habari za kiintelijensia. Kwao wana uhuru wa kuandamana, wanafanya makongamano na nafikiri umeona jinsi wanavyoamua kwa kura ya maoni.

Hivi we kwa akili yako, ingeitishwa kura ya maoni tuchague SUKARI IUZWE 2000 AU 3000, TUNGECHAGUA 3000?
 
Fanya flashback ya posts za jamaa kwanza kabla hujapoteza muda kujibizana naye.

Yuko kwenye Payroll ya chama kwa hii kazi.
Hilo nalifahamu fika mkuu..ila kitendo cha kuendelea kusisitiza Uingereza ingependa kuwa na ''Rais'' kama Magufuli inakupa picha tosha huyu ni mtu wa namna gani..
 
Hilo nalifahamu fika mkuu..ila kitendo cha kuendelea kusisitiza Uingereza ingependa kuwa na ''Rais'' kama Magufuli inakupa picha tosha huyu ni mtu wa namna gani..

Ha ha ha, hawa jamaa ni shida, akishalipwa ni lazima aandike kutetea hata kama ni uozo. Wanaandika hata vitu wasivyoviamini hata wao wenyewe, ila kwa sababu ni lazima mkono uende kinywani inabidi tu kuandika.
 
daaah mi nikadhani umeleta mada nzuuuuuri na mapya toka uingereza kumbe unania kuelezea history ya siasa za kibongo tena la mda uliopita.
 
Vyovyote vile unavyopenda kuliita hilo, neno lkn ukiwaonyesha mambo anayoyafanya Magufuli wetu yaani kuongoza kama alivyoahidi kwenye Kampeni, ni dhahiri wangependa kuwa naye, hiyo ni human nature!
Ina maana Uingereza haina Balozi hapa nchini wa kureport Yanayoendelea kiasi cha wao kutamani kuwa na ''Rais'' kama Magufuli....???
''Ukiwaonesha''.kwani ni jukumu la nani kuwaonesha kama hata wao hawaoni?
 
Ha ha ha, hawa jamaa ni shida, akishalipwa ni lazima aandike kutetea hata kama ni uozo. Wanaandika hata vitu wasivyoviamini hata wao wenyewe, ila kwa sababu ni lazima mkono uende kinywani inabidi tu kuandika.
uandishi wake ni mzuri.........................................................................................katika bolding na font size
 
Ina maana Uingereza haina Balozi hapa nchini wa kureport Yanayoendelea kiasi cha wao kutamani kuwa na ''Rais'' kama Magufuli....???
''Ukiwaonesha''.kwani ni jukumu la nani kuwaonesha kama hata wao hawaoni?

Unachangaya mambo, ninavyoongelea Waingereza naongelea wananchi wa kawaida wa nchi hiyo na siyo maelite ambao wanaongoza, sasa huyo Balozi si ni sehemu ya maelite hawezi kuwaambia ukweli huko...
 
Back
Top Bottom