Kujitetea kwa mama Anna Abdallah akichangia bajeti ya kilimo na chakula

kupelwa

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
1,087
450
Nimeona kwenye runinga leo mapema asubuhi mama anna abdalah akichangia bajeti ya kilimo na hilchakula, kuwa anakiri kuwa mh. Mudhihiri na mkewe walilipwa posho ya kuhudhuria kikao cha bodi ya korosho , mudhihiri akiwa makamu mwenyekiti wa bodi , hito na mkewe kama msaidizi.

Je kukiri na kukubali alilipwa kama fadhila ya ulemavu, ili apate msaidizi, kanuni za fedha katika malipo ya wajumbe zinakubali wasaidizi nao walipwe kama wajumbe wa bodi?

Najua huyu mama alikwenda mbali zaidi kuwa hapashwi kulaumiwa na ubovu wa utendaji katika zao la korosho sababu ana mwaka mmoja tu.je mwaka mmoja na vikao vingi ambayo bado kuna ubovu anayo hoja ya kujitetea?
 
Hata mimi nimemshangaa kwani bila hata aibu anasema eti ni kweli mke wake kapewa posho kumwakilisha mume wake then anawalaumu walioletaj habari.uzee etaabu kwelikweli
 
Ni ukweli kabisa kwa hoja ya mudhihiri kuwa na msaidizi kwa hali aliyonayo. Kwamba ni mkewe cyo tatizo pia . Shida nani amlipe na kutoka fungu lipi?
 
Ni ukweli kabisa kwa hoja ya mudhihiri kuwa na msaidizi kwa hali aliyonayo. Kwamba ni mkewe cyo tatizo pia . Shida nani amlipe na kutoka fungu lipi?

Mie sikubaliani kabisa! Ulemavu Wa Mudhihiri si Wa kihivyo kama wale wenzio wasioona, wasioweza kutembea n.k. Yeye ni mkono mmoja, anaona vema na anatembea vema. Huyo msaidizi Wa kuingia hadi kwenye kikao na kulipwa sitting allowance Wa nini? Kama ni msaidizi atalipwa only nauli na perdiem ili kmsaidie chakula na malazi. Posho ya kikao ya nini? Wizi mtupu!
 
Yule mama ni mhuni pamoja na utu uzima wake.
Jerome Bwanausi amelipwa mara mbili kwa kikao kimoja. Sasa yeye anamtetea kwamba kuna kazi alikuwa amefanya kabla ya kikao.
Kwa kawaida wajumbe wa bodi wanalipwa kwa kuhudhuria vikao, si kwa kufanya kazi za bodi. Sasa kama bwanausi alilipwa kwa kufanya kazi nyengine, mkurugenzi na watendaji wengine wanafanya nini?
Ni kwanini hati moja ya malipo aandike J. Bwanausi na nyengine anaandika Jerome Bwanausi? Huu ni wizi wa dhahiri kabisa na kuutetea ni kukubali kuwa mwendawazimu!
 
yale yale ya Lowasa na Mke wake kwenye ziara ya kamati ya ulinzi na usalama nje ya nchi
 
huwa namuona Mudhihili mara nyingi kwenye Television ya Taifa akichangia mada mbali mbali bila kuwa na msaidizi au kwa sababu huko hamna posho? ndio maana aendi na msaidizi watanzania tuache kusapoti ufujaji kama huu
 
Tunahitaji sheria au mfumo utakuwa na sura ambazo ni combination ya (a)Sheria za kijeshi kidogo(b) Dictatorship kidogo (c) Ubepari kidogo (d) na zinazotoa adhabu moja kwa moja kwa wafujaji wa fedha za umma. Harafu naona hili neno la fedha za umma limezoeleka kiasi kwamba inaonekana kama hazina mwenyewe, sasa inabidi tuweke mwenyewe badala ya umma tuseme pesa za (i) Serikali (ii) Pesa za maendeleo ya kitu fulani zitajwe moja kwa mojwa siyo pesa za umma tu au kodi fulani tu ili mredi usipomaliza au kisipofanyika anayekuwa responsible anafilisiwa moja kwa moja na kifungo juu.
 
Hata mimi nimemshangaa kwani bila hata aibu anasema eti ni kweli mke wake kapewa posho kumwakilisha mume wake then anawalaumu walioletaj habari.uzee etaabu kwelikweli

wamezoea kufanya madudu na yakaendelea kuwa siri na wanashindwa kuelewa usiku umeisha ni asubuhu nyeupe waTz wamechoka na kufanywa misukule
 
Back
Top Bottom