Kujisafisha kwa Dk Hoseah kwasababisha kujipalia moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujisafisha kwa Dk Hoseah kwasababisha kujipalia moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 4, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Date::11/4/2009Kujisafisha kwa Dk Hoseah kwasababisha kujipalia moto

  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi  KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imesema hakuna azimio lolote katika taarifa yake kwenye mkutano wa 16 wa Bunge ambalo linaonyesha kumuweka kando na tuhuma za Richmond Mkurugenzi Mkuu wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah na kwamba, mbivu na mbichi zitajulikana kwenye taarifa ya serikali.


  Jumatatu wiki hii Dk Hoseah, akijibu swali la kwanini asijiuzulu ili kuonyesha uadilifu na uzalendo katika utumishi wa umma, alisema: "Siwezi kujitia kitanzi cha kamba eti ili nionekane mzalendo, sina mpango wa kujiuzulu".

  Hoseah alitoa msimamo huo huku akihoji kama watu wamesoma vizuri azimio namba 20 katika Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini ya mkutano wa 16 wa Bunge, ambayo ilionyesha hana kosa.


  Lakini, akizungumzia kinga hiyo anayoanza kuitumia Hoseah na baadhi ya wapambe wake mitaani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shellukindo alisema hakuna sehemu ambayo kamati imemsafisha bosi huyo wa Takukuru.


  "Hatujamsafisha popote, sisi tunamsubiri ndani ya ripoti ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio yetu, maana tunajua hadi sasa yeye ni mmoja wa watuhumiwa," alifafanua Shellukindo huku akionyesha kushangazwa na kauli hiyo ya Hoseah.


  Kumbukumbu hizo za Bunge (Hansard), ambazo Hoseah ameanza kuzitumia kuhusu Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini ya Agosti mosi, kujibu taarifa ya serikali iliyotolewa Julai 25.


  Kumbukumbu hizo zinasema: "Mheshimiwa Spika, Azimio Na. 20, Serikali iendeshe uchunguzi maalumu ili kubaini ukweli kama taarifa rasmi ya Takukuru iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine.


  "Na kama jalada halisi linalohusu kampuni ya Richmond lililokuwa BRELA liliharibiwa na kuwekwa jingine kwa lengo la kuficha ukweli. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa serikali: Kamati ya Vyombo vya Dola imekamilisha uchunguzi wake kuhusiana na suala hili.


  "Na imebainika kuwa, si kweli kuwa taarifa rasmi ya Takukuru iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa suala la Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine kwa lengo la kuficha ukweli.

  "Vile vile, taarifa ya kamati ya vyombo vya dola inaonyesha baada ya upelelezi na uchunguzi wa kina kufanyika wameridhika kuwa jalada halisi la Richmond lililokuwa BRELA halikuharibiwa na wala hakukuwa na jalada lingine lililowekwa kuficha ukweli wa jambo hili."


  "...Maoni ya Kamati; kamati inaridhika na taarifa hiyo."

  Hoseah akitumia azimio hilo, alisema alibahatika kusoma kwa makini taarifa zote za kamati kuanzia ya kwanza na hiyo ya pili na kuhoji : "Sasa nijiuzulu kwa kosa lipi, mnihukumu kwa haki si kwa hisia, siwezi kujitia kitanzi cha kamba ili eti nionekane mzalendo au unataka kuchukua nafasi yangu (alimuuliza mwandishi wa gazeti hili)?"


  Hata hivyo, Shellukindo akifafanua alisema Hoseah anaweza kuzungumza anachofikiri, lakini ukweli kama amesafishwa au la, utajulikana baada ya taarifa ya serikali kuwasilishwa ndani ya kamati kisha bungeni.

  "Kama anasema azimio hilo limesafisha basi asubiri kila kitu kitajulikana baada ya taarifa ya serikali, tunachojua hadi sasa yeye ni mtuhumiwa na tunamsubiri ndani ya kamati," alisisitiza Shellukindo.


  Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond na kumfanya Edward Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu Februari, 2008, alisema: "Hatuna muda wa kubishana na Hoseah, ila tunamsubiri ndani ya ripoti."

  Shellukindo alisema maazimio yako wazi na kusisitiza: "Sasa kama kuna sehemu tumemsafisha tutajua siku mbili hizi maana tutapata taarifa ya serikali".


  Alisema kamati itahitaji kujua watuhumiwa wote hata ikiwemo waliostaafu kama utaratibu uliotumika ulikuwa ni wenye mantiki gani.

  Katika mkutano wa 10 wa Bunge la Februari ilitoa maazimio 23 yaliyotakiwa kutekelezwa na serikali kuhusiana na kashfa ya Richmond.

  Kati ya maazimio hayo, Namba Tisa: Lilitaka Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru (Edward Hoseah) awajibishwe na mamlaka ya juu (rais), kutokana na taasisi hiyo kuisafisha Richmond.
  Utekelezaji: Tayari Hoseah ametakiwa kujieleza kwanini Takukuru iliisafisha Richmond, kwanini haikubaini kupuuzwa ushauri wa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) na kwanini haikubaini kasoro kama ilivyofanya kamati. Hoseah amekwishajitetea kwa Katibu Mkuu Kiongozi (Philemon Luhanjo), anasubiri hukumu.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ngoma mbichi usanii una mwisho na wadanyika ndiyo wana amka . Nasema 2010 ina mambo .So hapo lazima CCM waamue kutumia vyombo vya usalama zaidi ya hapo utasikia .
   
 3. l

  lukule2009 Senior Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hosea anantakiwa kuelewa kuwa sasa kinachoongelewa ni maazimio ya Bunge. Ripoti ilishasomwa naikaeleweka wabunge wakaweka maazimio baada ya kudigest ripoti .. kwa hiyo kwa sasa ni maazimio sio ripoti ..
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  Hosea ngangari, ni jeuri ya JK, wabunge watabaki wakipiga kelele za mlango.
   
Loading...