Kujilinda na vibaka ama wavamizi bila ya kuwa na silaha

mjusilizard

JF-Expert Member
Nov 7, 2019
918
1,576
Vipi wakuu?

Kuna jamaa yangu alivamiwa beach na vibaka watatu wenye visu, hakuwa na ujuzi ila nafikiri nao walikuwa mateja tu hawakujua kutumia silaha, aliwaweza kwa street fight tu za kuzaliwa, alimmwagia mchanga mmoja usoni akapiga vibaya mno.

Ila siku nyingine anaweza kutana na wababe, si unajua hapa bongo. Je, ni mbinu gani za kujihami na hawa vibaka au watu wanaokuvamia pasipo nawe kuwa na silaha? Mbinu gani za kueliminate the challenge/ defencing katika hali kama hii ya jamaa yangu?
 
mimi nilikua na laki tatu mfuko wa nyuma, alafu mfuko wa mbele nilikua na sh.200 tu.
Nikapita chocho flani kajamaa kamoja kakajifanya kanakojoa, nilivyompita tu akatokea mwingine kwa mbele machale yakanicheza.

Yule wa mbele akaniambia "braza tupe hata pesa tukavute mafegi" (nadhani alifikiri nitakataa kumpa hela ya fegi ili wapate sababu ya kunikaba).

Kwa haraka sana nikaingiza mkono mfukoni nikatoa sh.200 nikampa akaipokea akabaki ameduwaa; Yule mwenzake akaanza kupiga kelele kumlaumu kwa nini ameniacha nipite ila jamaa hakumjibu chochote na mimi nikawa tayari nimeshamaliza kuvuka hicho kichochoro salama salmini.

Mbinu kubwa ni kujiamini tu.
 
mimi nilikua na laki tatu mfuko wa nyuma, alafu mfuko wa mbele nilikua na sh.200 tu.
Nikapita chocho flani kajamaa kamoja kakajifanya kanakojoa nilivyompita tu akatokea mwingine kwa mbele machale yakanicheza,
Yule wa mbele akaniambia "braza tupe hata pesa tukavute mafegi" (nadhani alizani nitakataa kumpa ili wapate sababu ya kunikaba)
Kwa haraka sana nikaingiza mkono mfukoni nikatoa sh.200 nikampa akaipokea akabaki ameduwaa; Yule mwenzake akaanza kupiga kelele kumlaumu kwa nini ameniacha nipite ila jamaa hakumjibu chochote na mimi nikawa tayari nimeshamaliza kuvuka hicho kichochoro salama salmini.

Mbinu kubwa ni kujiamini tu.
daah safiii, nimeelewa.
 
mfano mimi niliwahi kukutana na vibaka kama saba hivi wakanisimamisha ilikuwa kama saa saba usiku. Nilisimama haraka sana na kuanza kuwasilikiliza wanavyopiga mikwara mbuzi mwisho nikauliza "mambo haya mnayaweza au ndo mnajifunza isije kufika mahali mkakataana", wakati huo nilikuwa natembeza macho pande zote kumtafuta mbabe zaidi ili element of supply ianzie kwake. wakaishia kucheka tu na kusema haina noma bro.
 
daah, asante kwa mbinu kaka, barikiwa!!!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom