Kujifungua sawa na kujisaidia?

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,942
3,047
Taarifa hii naona mtuhumiwa hajasema kweli. SOMA


Kichanga chaokolewa baada ya kutumbukia chooni, chaitwa Bahati
Na Festo Polea

MTOTO mchanga, mwenye umri wa siku saba hadi jana usiku wakati gazeti hili linaenda mitamboni, hakika anastahili kuitwa jina la Bahati, kwani bila bahati angepatwa na mauti baada ya mama yake kumzaa na kumwachia atumbukie chooni akidhaniwa ni haja kubwa.


Kisa hiki cha kushangaza kimetokea jijini Dar es Salaam, baada ya mama wa kichanga huyo, Aziza Said (21) mkazi eneo la Mbuyuni, Kata ya Tandale, kudaiwa kujifungua mtoto huyo saa 11:45 alfajiri ndani ya choo cha jirani na kutoroka akikiacha mtoto huyo akilia ndani ya shimo la choo.


Kichanga Bahati hivi sasa yupo katika mikononi mwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala wakati mama yake anashikiliwa na polisi, Kituo cha Urafiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jamal Rwambow, amethibitisha.


Bahati ya kuwepo hai kwa kichanga Bahati, inatokana na juhudi za Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbuyuni, Zinduna Kimbonaga, ambaye anaeleza kuwa baada ya kuptwa na uchungu, Aziza alikwenda chooni na kumzaa mtoto huyo na kuwa baada ya kumzaa alimuacha akitumbukia chooni na kukimbia.


Mama wa kichanga amekiri baada ya kukamatwa na kubanwa, kuwa wakati akijisadia, alihisi kitu kimetoka na kutumbukia kwenye shimo la choo.


"Watu walipofika katika eneo hilo, walisikia sauti kutoka ndani ya shimo la choo na kufikiri kuwa ni paka ametumbukia chooni kutokana na sauti kufanana na paka," alisema Kimbonaga.


Alisema baada ya kushuhudia hali hiyo, walipiga simu polisi, bila mafanikio na kwamba, kutokana na hali hiyo, akawatuma vijana wake kwenda polisi kutoa taarifa kwa njia ya mdomo.


Kimbonaga alisema vijana hao, kituoni hapo, walikutana na askari ambaye aliwaelekeza wawasiliane na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana.


Alisema waliwasiliana na Kamishna Tibaigana ambaye naye aliwasiliana na kituo cha Urafiki na kuwaelekeza kufuatilia tukio hilo. Hata hivyo, askari hawakufika katika eneo hilo.


Kimbonaga alisema baada ya jitihada hizo kugonga mwamba, waliwasiliana na Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji ambao walifika na kutaka kumuokoa kwa kutumia kamba.


Hata hivyo, alisema wananchi walipinga suala hilo kwa kuhofia kwamba, kichanga huyo asingeweza kutoka katika shimo hilo la choo akiwa hai.


"Wananchi walitishia kama kichanga huyo angetolewa akiwa amekufa basi wangelichoma gari la Zima Moto," alisema Kimbonaga.


Alisema baada ya zoezi hilo kushindikana, wananchi walivunja sehemu ya juu ya choo hicho na kijana mmoja akaingia katika shimo hilo bila ya kuwa na mavazi maalum ya kujikinga na kufanikiwa kumtoa mtoto huyo aliyekuwa anaelea juu ya kinyesi, huku akiwa katika kondo la uzazi lililokuwa halijakatwa.


Kimbonaga alisema baadaye, kichanga huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Jijini Dar es Salaam na siku mbili baadaye, Kimbonaga alianza juhudi za kumtafuta mtuhumiwa kwa kuuliza mwanamke aliyekuwa mjamzito.


Juhudi hizo zilizaa matunda baada ya Aziza kubainika kuwa ndiye aliyekuwa na dalili zote za ujauzito katika eneo hilo ambaye baada ya kutenda kitendo hicho, alikimbilia kujificha katika kijiji cha Chamazi, wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam wanakoishi wazazi wake.


Baadaye Kimbonaga aliomba msaada katika kituo cha polisi Urafiki ambako alipewa askari wawili waliomkamata msichana huyo akiwa kisimani.


Awali, baada ya kukamatwa, Aziza alikana kuhusika na kitendo hicho, hali ambayo ilizua utata na kuwafanya askari hao kulazimika kumpeleka katika zahanati kijijini hapo kwa uchunguzi zaidi na kuthibitika kuwa alihusika na kitendo hicho.


Baada ya ukweli kudhihiri katika zahanati hiyo, msichana huyo alikiri kuhusika na kitu hicho na kujitetea kuwa alitenda hayo kwa bahati mbaya.


Habari zinasema kuwa mume wa msichana huyo, Shabani Athumani, ameripotiwa kumfukuza nyumbani mkewe baada ya kusikia kuwa amehusika na kitendo hicho.


?Mke wangu ndiye amefanya hivyo! Sidhani. Mimi nilikuwa mmoja katika harakati za kuokoa kiumbe kile, kumbe ni kiumbe changu kweli! Aziza amefanya unyama huu kweli! Aliniambia ana mimba ya miezi mitano, kumbe ilishafika miezi ya kujifungua! Sasa kwanini alinidanganya, kaficha nini hapo?!? alilalama Shabani, huku machozi yakimtoka kwa uchungu.


Shabani aliliambia Mwananchi kuwa walipatana na mkewe ambaye ana watoto wadogo wawili wa miaka mitatu na mwingine mwaka mmoja kuwa watumie uzazi wa mpango ili kuzuia mimba na wote kwa pamoja waliafikiana na kukubaliana kutumia njia hiyo.


Hata hivyo, alisema kadri siku zilivyokwenda, mkewe alionekana kuwa na mabadiliko ya kama mtu mwenye ujauzito na kwamba, siku zote alipojaribu kumuuliza, alikataa kuwa na ujauzito.


?Muda ulipozidi kuyoyoma, mimba ilizidi kukua. Ndipo nilipombana na akakubali kuwa ana mimba na kuniambia kuwa alikosea wakati wa kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Nikakubaliana naye na kuendelea kuilea mimba aliyoniambia kuwa ni ya miezi mitano. Kumbe ilikuwa imeshafika miezi tisa tena ya kujifungua,? alisema Shabani.


Alisema siku ya tukio alishiriki kikamilifu kuokoa mtoto aliyetupwa chooni bila wasiwasi huku akijua kuwa mkewe alikuwa na mimba ya miezi mitano, hivyo, hawezi kuwa ni mhusika wa kitendo kile.


Kamanda Rwambow alipoulizwa, alikiri kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 14, mwaka huu baada ya Aziza kujifungua mtoto chooni, kisha kuanguka katika tundu la kujisaidia na baada ya mama huyo kujifungua alitoweka na kutiwa mbaroni siku mbili baadaye.


"Ni kweli tukio hilo liliripotiwa wiki iliyopita na jalada limefunguliwa. Kwa sasa polisi inafanya uchunguzi kuona kama mama huyo alijifungua kwa bahati mbaya au alifanya makusudi,"alisema Kamanda Rwambow.


Hata hivyo, baada ya Mwenyekiti huyo wa Serikali ya Mtaa kukubaliana na baba wa mtoto huyo kumchukua mtoto wao na kurudi naye nyumbani ili kuendelea kumlea Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala ametaka apelekwe Ustawi wa Jamii kwa ajili ya matunzo.


Mvutano huo umetokea wakati mwenyekiti huyo akitaka kumchukua mtoto aliyemuokota, huku akionyesha karatasi ya ripoti kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Urafiki/Ubungo iliyokuwa na namba URP/RB/10275, huku Mganga Mkuu akikataa kumuacha mtoto huyo mikononi mwa mwenykiti huyo.
 
huyo mwanamke mwongo wa kutupwa watu kama hawa ndo wakaozee segerea....utatupaje mtoto?na ka ulikua humtaki kwanini uli....... ovyo ovyoooo??
 
mume kachezewa akiri hapo............alafu akiri zake ziko kiBushoke Bushoke.........!
We huwezi ukaambiwa mkeo ana mimba ya miezi mitano alafu anajifungua mtoto kisha anamtupa chooni ......we una kadhania kwamba mtoto wako!
Mtoto huyo ni wababa mwengine .... alafu yy (mkeo) hana mpanga nae walikua wanajiachia tu.... sasa bahati mbay ndio nanilihiii.. ikaingia takuaambiaje wewe wakati anajua wewe unajua kwamba anatumia vidonge vya uzazi...!!? sindi akuaongopee alafu ana opt kutupa kiumbe ndani ya toilet.
Lakini ww badi unakazania wako,basi poa "ok then wako ila nilijifungua bahati mbaya wakati naenda kujisaidia....." nafikiri hii ni parfect excuse,isn'nt it!?
Wewe unakubari kwavile unampenda mkeo na maaisha yanaendelea.............AU MNASEMAJE????
 
ha hah aaaa haaaa aiseee wewe sanda wajua kufikiria.....
ila hapo pa kujifungua kwa kwenda chooni kibahati mbaya....hapana bado hatukubaliani....
 
1. Mtoto alivyo mzuri kama malaika- yaani kumtupa chooni ili kumuua ni dhambi sana- heri tu angemzaa akamwacha barabarani wasamaria wema wamchukue wamtunze!

2. Kuzaa na kujisaidia- kwa kweli mimi mwanaume sijui- hebu Mamalao au Mwafrikawakike mtupe mwanga!
 
Taarifa hii naona mtuhumiwa hajasema kweli. SOMA

...Alisema baada ya kushuhudia hali hiyo, walipiga simu polisi, bila mafanikio na kwamba, kutokana na hali hiyo, akawatuma vijana wake kwenda polisi kutoa taarifa kwa njia ya mdomo.

Kwa nini simu ya Polisi isipatikane? kuna emergency number? je wananchi wanaijua? Mungu hakutaka tu kukichukua kiumbe hiki, it should have never been allowed to take all this long for someone to do something to save the life of this poor little baby.

Kimbonaga alisema vijana hao, kituoni hapo, walikutana na askari ambaye aliwaelekeza wawasiliane na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana.

This is ridiculous! huu ndio utaratibu uliopo?yaani kumtoa mtoto alietumbukia chooni hadi uwasiliane na Kamishna wa polisi?mind you watu wamepiga simu hampokei..(sorry-haipatikani?), wametembea all the way hadi kituoni lakini baaaaado??! na kwanini basi kama hizo ndio taratibu huyo askari mwenyewe asimpigie simu mkuu wake kuelezea hiyo incident? Sack him now!


Alisema waliwasiliana na Kamishna Tibaigana ambaye naye aliwasiliana na kituo cha Urafiki na kuwaelekeza kufuatilia tukio hilo. Hata hivyo, askari hawakufika katika eneo hilo.

Eti hawa ndio tunawategemea walinde usalama wetu na mali zetu! Hii ni emergency, you are talking about saving a human being life,ilitakiwa iwe priority hata ikibidi wafunge kituo kwa muda ili waende huko kwenye tukio.Kuna suala la insubordination pia hapa, wamekaidi amri ya mkuu wao.

Kimbonaga alisema baada ya jitihada hizo kugonga mwamba, waliwasiliana na Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji ambao walifika na kutaka kumuokoa kwa kutumia kamba.

Mimi nafikiri toka mwanzo hawa wananchi walitakiwa wawasiliane na hawa mabwana lakini siwalaumu kwa kuwa sidhani kama information za nini kinapaswa kufanyika kwenye matukio kama haya zinapatikana popote.

Kazi kwelikweli..........
 
Back
Top Bottom