Kujifungua kwa Operation imekuwa too much nowdays, why? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujifungua kwa Operation imekuwa too much nowdays, why?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Paul S.S, Jun 11, 2012.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kufuatia uzoefu wangu kupitia ndugu jamaa na marafiki, na pia maneno yanayosemwa sana mitaani ni kwamba hivi sasa asilimia ya wanawake kujifungua kwa upasuaji imekuwa kubwa sana tofauti na zamani

  Na kwa uchunguzi wangu mdogo kujifungua huku kwa operation kunatokea zaidi hapa DSM na mikoa mikubwa kama Arusha, Mwanza na Mbeya.
  Na kana kwamba haitoshi upasuaji huo hutokea zaidi hospitali za binafsi au hospitali za rufaa kwenye huduma fast track kama Muhimbili

  kwanini imekuwa hivi
  Je ni nyakati zimebadilika aina ya vyakula,madawa na mazingira yanafanya akina mama wanashindwa kujifungua kawaida?

  Je ni njia ya kupunguza uzazi kwa watu kuzaliana kwa kasi? (inaaminika operation mwisho watoto watatu,na once operation always operation)

  Je ni mbinu ya hospitali kujiongezea kipato(inaaminika operation is very expensive na inalipa zaidi,na Drs wanalipwa zaidi kwa kila upasuaji iwe private au gvt huduma ya fast track)

  Je ni mambo ya kisasa, akina mama wanataka wenyewe upasuaji kwa kuhofia uchungu na ''kupanua njia''

  Naomba mawazo yenu wadau................mnalionaje hili hasa akina mama
   
 2. awp

  awp JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  wadada wengi hawapendi kuzaa kwa kawaida, ku-exprerince ule uchungu naturally, secondly wanahisi wakiza kawaida maumbile yatabadilika kumbe hicho kitu hakipo kabisa. mi nina uzoefu wa kawaida na operation bado k yangu nng'aaa!
  la tatu mahospitali pia ni biashara kwani operation siku hizi inafika hadi laki saba.
   
 3. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kuhusiana na hali hiyo,ila wapo wanaotaka kufanyiwa upasuaji wenyewe na wengine ni matatizo .Ila nina ndugu yangu yeye kuanzia day one alivyopata ujauzito alisema mimi sitaki kuzaa kwa njia ya kawaida na kweli alienda hopital zote kuulizia procedures za kuzaa kwa operation na baadaye akapata hospital iliyomruhusu kufanya upasuaji pindi mimba itakapofika week 38 .Nikajiuliza hee kumbe ndio hivyo hee!Tunatakiwa tuwaelimishe dada/mama wenzangu kwa hili kama alivyosema Prof.Massawe kwenye utafiti wake kuhusu madhara ya upasuaji.
   
 4. UPOPO

  UPOPO JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 1,371
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  Mimi mwenyewe watoto wangu nimejifungua kawaida na bado kuko bomba kabisa.Wajue Mungu alisema mtazaa kwa uchungu na sio mateso(kisu).
   
 5. P

  Paul S.S Verified User

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  How did u know kuko bomba...................joking lol
  Huyo ndugu yako hakusema ni kwanini haswa anataka upasuaji na sio kawaida
   
 6. M

  Mzalendowetu Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kuna dada mmoja alichagua kujifungua kwa operesheni ili mtoto wake aazimishe siku yake ya kuzaliwa kila tarehe 7 July. Yeye alikuwa katika wiki yake ya mwisho kabla ya kujifungua.
   
 7. Loly

  Loly JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  nakweli kuzaa kwa opereshi
  ni mateso makali sana, ila kawaida ni uchungu tuu
  mara puchuuu mtoto keshatoka unasahau unaendelea kula bata, ila kupigwa kisu kisa unaogopa uchungu?
  Lamda kama kuna tatizo ila kama hakuna bora mtu apush thats normal way.


  0
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wengi wao wamewahi kufanya mapenzi kinyume na maumbile, hivyo wanaogopa AIBU kutoka kwa Dr., na Manesi. Manesi inapotokea, kwanza humtukana mama na baadaye baba kwamba ana tabia mbaya kwa mkewe. Sasa hapo ndiyi kimbembe kama wewe baba hukuwahi kushiriki huo uchafu huo na mkeo,labda aliwahi kushiriki kabla hujamuoa au alichakachukua huko nyuma mkiwa ndani ya ndoa. Sasa ili kuepuka AIBU na hatari ya ndoa kuvunjika wengi wa dada zetu wanapendelea Kisu badala ya njia ya kawaida. Ikiwa kule nyuma kulisha tibuliwa, then HAJA KUBWA hutoka bila brake wakati anajikamua kumtoa Mtoto.

  Jaribu kuongea na madaktari watakuambia ukweli huu.
   
 9. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,283
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Go try labor pains to tell if c-section option is kinda luxury.
   
 10. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kweli? hata kama tumbo lipo tupu??eh
   
 11. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mimi nilishawahi kuona video ya jinsi mtoto anavyozaliwa...nakuhakikishia mkuu pauls hata wewe ungekuwa na 'K' unakitamani hicho kisu ...ni soo...Wakishikwa na uchungu wengine huwa wanapiga kelele kwamba hawatapata tena mimba lakini wakijifungua pamoja na mateso yote wanawaza kupata katoto kengine...Nadhani kuna fumbo kubwa sana Mungu ameliweka kwenye kubeba mimba na kujifungua kwa mateso kwa akina mama na nadhani ni vizuri mtu akajifungua kwa njia ya kawaida unless awe na matatizo
   
 12. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hizi ni sababu za wanawake kujifungua kwa Upasuaji  KUMEKUWA na ongezeko la wanawake wajawazito ambao wamekuwa wakijifungua kwa upasuaji, hali hii inaonekana kuongezeka siku hadi siku. Zipo sababu nyingi ambzo zimekuwa zikichangia mojawapo ni wanawake kuhofia kuharibika kwa viungo vyao vya uzazi na kusababisha kuharibu mahusiano na waume zao. Katika makala haya mwandishi FREDERICK KATULANDA amefanya mahojiano na Dk. Andrew Kilonzo Mwanza Hospitali ambaye ni bingwa wa magonjwa ya wanawake.
  Mwananchi: Kumekuwa na ongezeko la wanawake wajawazito kujifungua kwa opasuaji na imeleezwa kuwa kati ya wajawazito 7 hadi 10 ambao wamekuwa wakijifungulia Hospitali kati yao watatu ama watano wamekuwa wakijifungua kwa upasuaji, hali ikoje katika Hospitali yako?

  Dk. Kilonzo: Kwanza ni lazima tuwe waangalifu kwamba takwimu hiyo ni kwa kituo gani, takwimu hizi ni kweli lakini huwezi kuzipata katika vituo vingi bali zaidi ni katika Hospitali zile ambazo zinapokea rufaa ya kama Bugando ambayo inapokea wajawazito hawa kutoka vituo vidogo wenye matatizo ya kujifungua. Wanawapata wagonjwa wengi kwa sababu wamekuja kwa matatizo.
  Lakini kwa hospitali zingine ukienda kama Hospitali ya wilaya huwezi kuona hili, sasa kwa hospitali kama yangu hapa kwa vile ni maalum, hapa matababu tunayotoa ni ya Specialist Care (Huduma ya Daktari Bingwa) hivyo tumekuwa tukipoka wale wenye matatizo pia.
  Wagonjwa wengi hapa wamekuwa wakiona na Specialist na usimamizi wakati wa kujifungua na wakati wa ujauzito pia wanaonwa pia na kwa sababu hivyo kumeshajengeka mazoea kuwa hapa wakija wanapata huduma ya Daktari Binngwa (specialist care). Wagonjwa ambao hawaendi kwenye vituo vya afya vya serikali (Public Services) wanakuja hapa, wanajua kuwa wakifika watahudumiwa na Daktari bingwa, hivyo hiki pia ni kituo ambacho kinapokea wagonjwa wengi wenye matatizo ya uzazi, ingawa sina takwimu za hivi karibuni lakini tatizo hilo lipo ni kati ya silimia 25 hadi 30 wanapata kujifungua kwa upasuaji.
  Vilevile utakuta kwamba hapa kwetu tuna ‘very high rate' ya kuona wagonjwa wenye matatizo ambao tayari wameshazaa kwa upasuaji siku za nyuma na wale ambao walipoteza watoto wakati wakijifungua.
  Mwananchi: Basi kutokana na maelezo yako, inaonekana kuwa kuna ongezeko la wanaojifungua kwa upasuaji, hebu tusaidie unadhahi inatokana na nini, pengine labda ni mazingira, maumbile au kitu gani kinasababisha wajifunge kwa njia hiyo?
  Dk. Kilonzo: Tukiangalia kwa ujumla ongezeko la wagonjwa ambao wanajifungua kwa upasuaji, Kwa ujumla hata kama siyo vituo vya afya au hospitali kama zetu na zile za rufaa, mie kama Specialist wa wanawake naweza kusema zipo sababu muhimu ambazo ninaweza kuziweka kwenye makundi matatu.
  Sababu ya kwanza; Ni kuongezeka kwa usimamizi wakati wa huduma za afya ya uzazi hasa wakati wa uchungu na kujifungua, kumekuwa na ongezeko la ubora katika kusimamia wakina mama wakati wa uchungu na kujifungua. Hili nalo limeenda sambamba pamoja na usimamizi mzuri wakati wa ujauzito katika kliniki zetu, imesaidia kutambua matatizo kutambua wakinamama ambao wanauwezekano wa kupata mtoto.
  Katika Klinini zao wanapokwenda usimamizi umekuwa mzuri zaidi, watu wametambua matatizo wakati wa uchungu, usimamizi unapoongezeka matatizo yanatatulika mapema na kama nilivyosema kujifungua kwa kwa kufanyiwa upasuaji (silzelie refection) ni moja wapo ya vifaa tiba (tools) tulizonazo katika kuongeza na kuborosha matokeo ya ujauzito, uchungu na kujifungua mtoto salama.
  Mwananchi: Umesema kuwa kujifungua kwa kufanyiwa upasuji ni moja kati ya vifaa tiba vya kuwezesha kuboresha matokeo ya ujauzito, uchungu na kujifungua salama, pengine ungetueleza ni kwa sababu gani unafanyika?
  Dk. Kilonzo: Upasuaji unafanika kwa sababu mbili tu moja ni kuhakikisha mtoto anazaliwa kwa usalama, na pili upasuaji unafanyika ikiwa afya ya mama inaonekana itahatarishwa ikiwa ataendelea kujifungua kwa njia ya kawaida, sasa hizo sababu ni mbili, lakini ongezeko utalikuta zaidi kwa sababu ya kutaka kuhakikisha mtoto anazaliwa katika hali nzuri na ya usalama.
  Hili ndilo limeleta ongezeko kubwa kwa siku za hivi karibuni, yaani indication umakini kwa ajili ya mtoto kupatikana. Zamani watu walikazania zaidi kuangalia afya ya mama, yaani mama alikuwa anajifungua kawaida lakini anajifungua mtoto akiwa katika hali gani lakini sasa kumekuwa na mkazo zaidi katika kujali hali ya mtoto, anakuwa katika hali gani, hivyo hili ndilo limeleta ongezeko.
  Na hili nalo limekuja kutokana na kuwepo kwa msisitizo wa kupata mtoto, sababu yake ni kuwa jamii yenyewe ama wanandoa wamehamasika kuwa wanapokuwa na ujauzito lengo lao ni kupata mtoto. Ndicho wanacholenga, hakuna tena kwa sasa anayesema tumepoteza mtoto ilikuwa amri ya Mungu… au ilikuwa bahati mbaya ahaaa! Kwa sasa ikitokea hivyo mtoto amepotea basi wanasema lazima kulikuwa na sababu na ndiyo maana wamepoteza mtoto.
  Na ikitokea wanauliza kweli, sababu iko wapi, je ni uzembe wa usimamizi wa vituo vyetu ama watoa huduma? Hii ni kwa sababu wazazi ama wanandoa wenyewe wako Confined na hali ya mtoto ndiyo maana wanapeleka shinikizo kwa hawa watoa huduma kuhakikisha matokeo ya ujauzito yanakwenda vizuri.
  Unapokuwa na shinikizo, hili shinikizo la kutaka mtoto, matokeo mazuri, hili shinikizo la kutokubali bahati mbaya na hili shinikizo la kutokubali mpango wa Mungu, inapokuja kwa watoa huduma ndiyo utakuta wanahakikisha usalama unakuwepo kwa mtoto na mama. Na zaidi ninasema ni usalama kwa mtoto.
  Unapokuja kwenye vituo binafsi, huku shinikizo ni kubwa zaidi, lipo kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kuliko kwenye Hospitali serikali. Bado katika hospitali za serikali kuna mwamko wa kupata matokeo mazuri lakini kwenye hospitali binafsi ni kuna mwamko mkubwa zaidi kwa vile katika hospitali hizi kuna suala la kufanua investigation, na watu kutaka kuhoji kwa nini matokeo yamekuwa mabaya, je, kulikuwa na uzembe au vipi?
  Kuna matukio mengi watu wamekwenda kutaka majibu haya hata katika vyombo vye sheria mahakamani, sasa katika huduma za hospitali binafsi watu wanataka kupata matokeo mazuri. Hii ni sababu moja ama ya kwanza.
  Sababu yingine ya pili; Hii ya kitalaam yaani tumeanza kuona wazazi watarajiwa (Mke na Mume) wanaomba wenyewe, wanaomba wenyewe kabisa, sasa hapa kuna mambo mengi hapa yanayojiingiza.
  Mwananchi: Dk. Inaelezwa kuwa kuna (wanawake) wanaoomba wajifungue kwa upasuaji kwa sababu kujifungua kwa njia ya kawaida wao wanaamini kuwa kunawaharibia maumbile yao ya asili ya sehemu za siri na kumpunguzia starehe mume wakati wa tendo la ndoa, unadhani hii nayo ni sababu ya hawa wanaomba?
  Dk. Kilonzo: Hili nalo tutaliona, lakini kwanza tuangalie kundi zima la wanaoomba kuzaa kwa kufanyiwa upasuaji. Watu wanaoomba kujifungua kwa upasuaji moja ya sababu ni kwamba wanaimani kuwa matokeo yatakuwa mazuri ikiwa mtoto atazaliwa kwa mama kufanyiwa upasuaji. Wanaona kama ni short cut ya kupata matokeo mazuri na ukiangalia katika kundi hili utagundua kuwa wengi ni wale waliowahi huko nyuma kupata matatizo, mimba ya kwanza ilitoka, uchungu uliichukua muda mrefu….. hatua hazikuchukuliwa zikachelewa na nini…. akapoteza mtoto, sasa mimba hii anaona kwamba ni kwa nini tungoje…! Anakuja anaomba Daktari mimi naomba nizae hivi.
  Anaomba afanyiwe upasuaji, kumbe ni kwa sababu ni kwa sababu ya matokeo ya nyuma hayakuwa mazuri ama kwa sababu yalishindwa kutatuliwa au kwa kweli ilibidi yatokee au pengine wameona kwa ndugu zao ama majirani zao ambao wamewaona, basi kumeanza kujengeka hiyo imani kwamba ukifanyiwa uapasuaji matokeo matokeo yanakuwa ya uhakika zaidi.
  Na sisi tumetumia njia hiyo hata siku za nyuma pale tunapoona mama mjamzito anamatatizo hatutaki kuachia kila kitu kiende kwenye nature (njia ya kawaida) kwani nature siyo perfect (yenye uhakika), ukiacha kila kisu kwa nature wakati mwingine inaku-surprise.
  Sisi tulitumia hii wakati mwingine kwa kufanya kitu ambacho kinaitwa Plan to deriver yaani kujifungua ambacho kimepangwa kabisa, tunapanga huyu mama azalishwe siku fulani anazalishwa kwa upasuaji, kila mtu anakuwa amejiandaa vizuri na hii inasaidia, ni kwa kweli inasaidia kuhakikisha kila kitu kinaenda. Lakini sasa hapa naomba ieleweke siyo kwamba ninahimiza watu waombe kujifungua kwa upasuaji, hapana ninajaribu kuelezea sababu au mazingira ambayo yanapelekea watu kufikiria kuwa akifanyiwa upasuaji watapata matokeo mazuri.
  Vilevile hili nalo limetokana na matatizo ya huko nyuma ya sehemu kubwa ya uangalizi wa huko nyuma katika vituo vyetu, hawa watu wengi ni wale ambao hawakupata uangalizi mzuri. Ukiwaangalia hawana matatizo makubwa, basi tu walikosa uangalizi mzuri wakapoteza watoto na safari hii wanakujia wanataka wazae kwa upasuaji ili kuhakikisha wanapata mtoto.
  Lakini kuna kundi lingine la wakina mama wanaoomba kuzaa kwa kufanyiwa upasuaji, wanaomba tu kuzaa kwa upasuaji, na hawa tunawaona na moja wapo ya sababu ni usimamizi wetu yaani namna tunavyo hudumia, vijana wengi wa sasa hivi, wa kileo na makuzi na malezi ambayo tunayafahamu kwa jamii yetu, wengi wanakuwa na woga mkubwa wa kupita katika njia ya uchungu wakati wa kujifungua.
  Kwa hiyo suala la uchungu kuna kundi la akina mama (wazazi watarajiwa) wamepata woga mkubwa wakupita katika uchungu wakati wa kujifungua, nah ii ni ka sababu upande wetu sisi watoa huduma tunaweza kuishughulikia lakini hapajakuwa na msisitozo mkubwa katika kupunguza ama kuondoa maumivu wakati wa uchungu.
  Hili nalo linatuhitaji sisi wanataaluma kulichukua, unajua tumekuwa tukishuhgulika na mambo makubwa makubwa kama unavyojua nchi yetu tumekuwa tukihangaika na vifo vya akina mama, vifo vya watoto wachanga, haya ya uchungu ukianza kuyazungumzia mahari ambako tunazungumzia vifo vya watoto 500 au 600 kwa kila wajawazito 100,000 wakati wenzetu wanaongelea vifo 10, mkianza kuongelea comfort wakati wa kujifungua inaonekana kama wakati wake haujafika. Kwamba tutatueni haya ya vifo kwanza tukimaliza ndipo tuangalie na hili.
  Lakini hili nalo ni tatizo, lakini tunashindwa kutokana ama na uweo wetu kuyashika yote, ni tatizo, lakini nadhani umefika wakati sasa wa hili nalo liangaliwe kwamba wakati wakina mama wanajifungua wanapata comfort, tuliangalie suala hili kwa vile kizazi hiki tulichonacho wengi hawawezi kustahimili maumivu yote ya uchungu.
  Wakina dada wengi wanakuja kwangu na kuuliza je mnafanyi nini kwa ajili ya maumivu ya uchungu, wengine wanaondoka kwenda nje kujifungua kwa kuogopa uchungu au wengi wanaona ni afadhari kujifungua ka upasuaji kwa kuogopa vilevile uchungu kwani maumivu yake ni ya muda mfupi akitoka pale basi safi. Kwa hiyo nayo ni sababu ambayo inasababisha kujifungua kwa upasuaji.
  Sasa kuna sababu za kundi hili la tatu; Wanaoomba kuzaa kwa upasuaji kwa vile hawataki kuzaa kwa njia ya kawaida, basi tu wanaona kitendo cha mtoto kupia katika sehemu zake za kawaida wanaona kwamba kutawaondolea hali fulani hivi katika maumbile yao.
  Kwenye kundi hili si wengi lakini wapo, wote hawa wanaoomba wanayo imani ukizaa kawaida shemu za uzazi zitaharibika, nalo linamisingi yake kwa sababu kwenye hii minsingi utakuta kwamba usimamizi wakati wa uchungu huko nyuma katika vituo vyetu hawakuwa wakihakikisha watu wanashonwa vizuri baada ya kujifungua haikuwa ikienda kwa umakini sana.
  Programu hizi za sasa hivi ndizo zimeanza kusisitiza kuhakikisha kwamba wakina mama wapochanika wakiumia sehemu zao hizo wakati wa kujifungua wanatoa zile stadi za kuweza kushonwa vizuri ama kuweza reaper vizuri kuweza kurudi katika hali yake ya kawaida.
  Watu wengi wamekuwa hawafanyiwi reaper vizuri, nah ii imepelekea hali kama hii ambayo tunaizungumza, kwa hiyo kuna wanaokuja kwa sababu hizo na wale ambao wanafikiri kwamba wanataka kuzaaa mtoto mmoja au wawili kwa nini apate shida zote kupitisha mtoto kwenye njia ya kawaida. Hili nalo ni kundi ambalo tunaliona.
  Kwa hiyo hili ongezeko la kujifungua kwa upasuaji tumelizungumza katika maeneo haya matatu ambayo tunaweza kusema yanachangia kwa sehemu kubwa.
  Lakini nilisahau kueleza sababu hii nyingine hapo juu inayosababisha wajifungue kwa upasuaji, tayari tunao wazazi wengi ambao walishajifungua kwa upasuaji huko nyuma, hawa ambao wamejifungua kwa upasuaji ni moja wapo ya kundi ambalo linaongeza idadi ya wanaojifungua kwa upasuaji, huku nyuma ameshazaa kwa upasuaji kwa hiyo hayuko tayari kupoteza.
  Mwananchi: Lakini kuna wanaoleleza kuwa sababu ya maumbie yetu yanazidi kubadilika, watu wanapungua kimo cha urefu, wanawake wanaozaliwa wengi wanakuwa wafupi, kwa maana hiyo ni kuwa nyonga zao haziruhusu mtoto kupita wakati wa kujifungua kama warefu, hili lina ukweli gani?
  Dk. Kilonzo: Hapana sikubaliani sana na sababu hiyo, maumbile ni sawa tu na siku zote tunajua kwamba maumbile ya akina mama yanaweza kuhusiana na uwezo wa kujifungua either kwa urahisi, kwa mfano wakina mama wafupi wanao uwezekano wa kuwa na nyonga finyu na kusababisha shida wakati wa kujifungua, lakini hizo tunaweza kusema zilikuwa ni sababu za wajawazito kujifungua kwa upasuaji ni sababu za akina mama na siiyo za mtoto hazijaongezeka hizo.
  Kwa sehemu kubwa afya za Watanzania kwa sasa zimeimarika tunapata wengi ambao wanakuwa na maumbie makubwa, warefu wanafikia urefu mzuri hili siyo sababu, afya za akina mama zimaimarika na hata ukiona vjana ambao wamefikia umri wa kubalehe wanamaumbile makubwa kuliko wale wa miaka mingi ya nyuma. Hilo siwezi kufikiri kama sababu nyingi nimeeleza hapo na sababu kubwa kuliko zote ni kuboreka kwa umamimizi wa huduma.
  Mwananchi: Lakini kuna hili ambalo upande wa wateja wazazi nalo wanasema kwamba kujifungua kwa upasuaji kunawaingizia fedha ninyi watoa huduma, kwa hiyo madai yao ni kuwa mtu akifanyiwa upasuaji analipa sh. 1.5 milioni, mnatumia kama sehemu ya kujiongezea mapato, pengi unalizungumziaje hili?
  Dk. Kilonzo: Yaah..! Hili linazungumzwa sana mara nyingi na watu wanapenda kuzungumzia hili suala la Financial Benefit kwamba ukizaa kwa upasuaji wanafikiri kituo fulani kinapata fedha haraka kwamba ni mradi wa watu, mimi niko kwenye Hospitali binafsi nalisikia likizungumzwa pia.
  Lakini kusema ukweli ni kwamba; Moja, unapofanya upasuaji watu wanapaswa kuelewa kuwa ni gharama kwa kituo kuweza kufanya upasuaji, watu wanafikiri upasuaji unaleta faida kubwa lakini zinaingiza gharama kwani uwekezaji wa kuweza kufanya upasuaji ni kubwa. Kwa uzoefu wangu mimi hapa kituo changu hiki cha Mwanza Hospitali ninapata faida kubwa mama akijifungua kawaida kuliko faida inayopatikana mgonjwa akijifungua kwa upasuaji.
  Wagonjwa hawawezi kuelewa hilo, lakini Impute ya mjamzito aliyejifungua kawaida ni ndogo sana, tunachohitaji ni kuhakikisha tunakuwa na vyombo salama na vifaa vya kuweza kumsimamia, Muuguzi Mkunga ambaye amepata mafunzo vizuri anaweza kumsimamia na kumsaidia ajifungue kawaida, lakini ukianza kufanya upasuaji utatumia muuguzi, daktari bingwa afanye upasuaji, daktari wa usingizi, vifaa vya upasuaji na nini.
  Sasa impute ukileta daktari wa usingizi anataka hela hii, wa upasuaji hela, vifaa vyenyewe vinavyotumika tu kwa upasuaji vinahitaji hela, na maarifa tu (skill) zinazotumika, risk kwa mpasuaji ya kupata maambukizo ya HIV, kushitakiwa matokeo yakiwa mabaya, Mgojwa akae siku tatu, yaani siku tatu unaye mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji unasubiri uangalie anaendeleaje.
  Ukiangalia vyote hivyo ni hedeck kuliko mama akijifungua kawaida, huyu akifika napigiwa simu naambiwa Dokta kuna mama amekuja hapa kila kitu kinaendelea vizuri basi baada ya saa mbili naambiwa amejifungua kawaida, gharama yetu ni ile ile ya kujifungua.
  Watu hawaelewi kwamba gharama tunayotoza kwa kujifungua ni ile ile tunayotoza kwa mama kwa anayejifungua kwa upasuaji na kawaida, tofauti inakuja kwenye matumizi, lakini ile tuliyomtoza ambayo hospitali ikiipata ni ile ile sasa tukipata mjamzito anataka kujifungua bila ya hedeck na kukaa siku tatu, siku tatu unae mgonjwa wa upasuaji unamgoja uangalie kamba anaponaje….! Mimi sikubali hoja hiyo kabisa, ingawaje inawezekana kuwa watu wanafanya hivyo, lakini ni gharama, ni gharama ya yule Daktari.
  Kuna watu anatumia hii kumchaji zaidi yule mgonjwa, lakini kwa vituo, sisi kaka kituo tunapata faida kubwa zaidi kwa mgonjwa anayekuja kujifungua kawaida ambazo zinahitaji investment chache na matokeo yake ni kubwa zaidi. Kwa hiyo hili hatulitumii kama mradi, hata kidogo na mara nyingi kwetu siwezi kusemea vituo vyote, kabla ya upasuajia hapa kwetu wazazi na wahusika wanapata ushahuri nasaha vizuri katika kila hatua mbapa ile itakayompelekea kwenda kufanyiwa upasuaji.
  Hakuna mgonjwa anayepelekwa kwenye upasuaji bila ya yeye kuelewa kinachoendelea ni nini. Kitu kikubwa ambacho tumekibaini kwa hili ningependa niliseme wanaolalamika sana juu ya upasuaji ni watu wan je ambao hawahusiki lakini wale ambao wapo ndani wakati wakati wa tukio wengi wao wanaona kabia kwamba kulikuwa na sababu nzuri na za msingi.
  Mwananchi: Pengine sasa kwa kumalizia, umekuwa Dkatari bingwa wa magonjwa ya akina mama, unadhani nini ambacho ni tatizo unakumbana nalo katika kazi zako nab ado halijafikiwa ama kufanyiwa kazi zaidi katika huduma hii ya mama na mtoto?
  Dk. Kilonzo: Kuna mambo mengi ambayo yamekuwa yakishughulikiwa, haya ambayo tumekuwa tukiyaongea ya afya ya uzazi, masuala ya uzazi salama yameshuhgulikiwa sana kwa sababu za kutosha tu kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto na akina mama, raslimali nyingi ya kwetu na za kimataifa zimetumika na nadhani ni matumizi mazuri, lakini kuna maeneo mengi yameacha nayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa upande wangu kwa vile pia ni changamoto kwani kitaifa bado hatujayawekea mkazo.
  Nina amini ni suala zima la matatizo ya wazazi kushindwa kupata watoto (Ugumba), ninataka kusema watu wenye ugumba wanaoshindwa kupata watoto, hii ni sehemu ambayo kwa kweli bado inaleta changamoto kubwa katika huduma zetu hapa nchini kwa sababu bado halijawekewa msisitizo wa kutosha kwa hiyo maendeleo makuba yaliyopatikana katika nchi zingine zile zilizoendelea na zinazoendelea hayajaweza kufika huku kwetu kwa sababu ni kama nilivyoeleza tunayo mengi tulichukua kuanza kuyashughulikia kwanza.
  Wakati tunaapojiweka vyema ni wakati mzuri wa kuanza kuangalia na haya ambayo kwenye huduma za umma hayajaweza kupewa kipaumbele, hili ni sehemu kubwa ambayo tunachangamoto hapo, kuhakikisha watanzania wanafaidika na a nchi katika eneo zima la utoaji.
   
 13. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mada nzuri,hili ni tatizo na linapaswa kupewa kipaumbele kujadiliwa,limekithiri mno,hali inatisha!
   
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  nakubaliana nawewe kabisa mimi nimezaa mara 3, na kuko supa. infact kuzaa kwa kawaida kumekuwa na risk sana has ukizingatia mabinti wengi ni waoga, hawana mazoezi na magonjwa pia. ukiwa mjamzito wakati uchungu unaanza kama utazaa kawaida hata kama mtoto anacheza kumpata mtoto akiwa mzima ni probability siku hizi, lakin ikiwa ni kwa upasuaji nai 100%.

  binafsi sifagilii upasuaji kwani hatma yake ni makovu tumboni yasiyopendeza ila kama umezaa kawaida tumbo liko safi hakuna mikunjo ya mishono.
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye blue,,,,acha bwana,,,kitu mnato eeenh,hongera mamaaa,,,,
  kwenye red ni kweli upasuaji unaendana na biashara,,,,,hilo lipo sana private,lakin na vyakula vya dada zetu navyo ni sababu,,,,baadhi hulahula hovyo na kujikuta watoto wana miili mikubwa,,,,wadada wengine nao hawali sana na hukosa nguvu
   
 16. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  Aaaha mimi nimetoka jifungua miez 2 iliyopita niliwahi kwenda hosp moja pale kinondoni kucheck kabebii kamekaaje
  amini usiamini docta kabla hata kuniangalia kaniambia eti ni vizuri nijifungue kwa upasuaji
  sikuamini masikio yangu pale alipokuwa akinishawishi kwa dhati kabisa kuwa hiyo hospitali yao ni nzuri sana kwa shughuli za kualisha kwa upasuaji .nkamdanganya narudi ngoja nikajadiliane na baba wa mtoto
  akanipa namba yasimu eti kanamba na bei watanipunguzia
  loh
  nimejifungua salama salmini pale kcmc ,na sasa nipo fit kama ingelikuwa upasuaji mpaka sasa ningekuwa mbovu.maskini mdogo wangu angel yeye alifanyiwa upasuaji mimba ikiwa na umri wa miez nane na wii moja,wanaendelea vizuri
   
 17. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kujifungua kwa kawaida mara nyingine kumekuwa na complications nyingi zinazopelekea hatari kwa mama au mtoto wakati wa kujifungua. Nafikiri ni kukosekana kwa maandalizi ya kutosha kwa upande wa mama mjamzito na mtoto aliyeko tumboni....especially inapotokea mtoto ni mkubwa au amekaa vibaya. Hii nimeshuhudia zaidi ya mara moja mama anashauriwa ajifungue kwa njia ya kawaida lakini anasisitiza operation mwishowe anajifungua mtoto akiwa na kilo 4 ambapo ingekuwa ni ngumu sana kujifungua kawaida.

  Mimi mwenyewe mke wangu aliambiwa ajifungue kwa njia ya kawaida lakini tulikataa. Siku zilipokaribia tulifanya check up kwa Dr mwingine na kupima ultra sound ikaonyesha umbilical cord imejiviringa shingoni mwa mtoto ambayo ingemnyonga kama mama angejifungua kwa njia ya kawaida...tukaishia kwa operation kama tulivyotaka na mtoto akazaliwa akiwa na afya njema.
   
 18. Siri Sirini

  Siri Sirini JF-Expert Member

  #18
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 547
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Me nilikuwa naogopa sana kuzaa kwa kawaida, ila nikasema nitajuaje mtoto anavyouma, dah, ila ndo hvyo nilipata kisu, mana nyonga zangu hazitanuki, na nina watoto 3 wote kwa operation.
  Ila kuna wasichana wengine wanapenda operation, kuna rafiki yangu alikuwa mjamzito, alikuwa ananiuliza kuhusu operation kama ina uma, nikamwambia ndio inauma ili kumwogopesha, akasema hataki kuzaa kwa njia ya kawaida, nikamwambia kawaida ndo njia nzuri na uchungu unauckia vizuri, ila akaja kula kisu, mana mimba ilipitiliza na mtoto alikuwa mkubwa sana, nadhani alifurahi sana.
  Hv hamna dawa ya kuondoa haya makovu ya mshono?
   
 19. F

  Froida JF-Expert Member

  #19
  Jun 12, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kuna wale wa cosmetic ambao labda hawazidi asilimia moja wengi na matatizo ya sekta ya afya
  Wakunga ,,na madaktari bingwa wachache kwenye maeneo husika mama anapokuwa labaour anatakiwa kila baada ya saa moja apimwe njia kama inapanuka kwa centimita angalau moja lakini kama hakuna wapima haitajulikana kama mama anaendelea vizuri na njia gani zichukuliwe ili asaidiwe
  umbali wa maeneo ya vituo vya afya na ukosefu wa usafiri kama mama amesafirishwa ili apatiwe huduma ya kitaalamu anachelewa kwa kitu kidogo
  ukosefu wa vifaa vya msingi gloves,mikasi ya kuvunjia chupa,dawa za kuongeza uchungu n.k huu upungufu unaongeza pia uwingi wa akina mama kuelekea kwenye kufanyiwa operesheni
  wengi kutokupata huduma ya klinik kabla ya kufunguliwa pia inachelewesha mama tatizo lake kutambulika mapema ikiwepo dalili za kifafa cha uzazi ( pre-eclamsia)
  kwa kweli sekta hii inahitaji bajeti ya kutosha sana
   
 20. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kuzaa kawaida raha sana. Uchungu unauma mpaka macho yanageuka kuwa kengeza, unaita ndugu, jamaa na marafiki wote unawamalilza mwisho wake unasukuma mtoto kwa raha.
   
Loading...