Kujibizana na wakwe...kumewahi kukutokea ?

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,786
1,225
Ni hivi umeacha pesa Mkeo kajifungua tena ana siku 10 hivi. Mama mkwe yupo nyumbani kwako halafu wewe ukienda job huku nyuma ni darasa kwa binti yake, "haiwezekani akawa anakuachia pesa ndogo namna hii"...Jioni ukirudi unamsalimia M'mkwe hakujibu, siku ya pili anaamua kukupa live....hebu mruhusu mtoto wangu nikamuuguze kwangu...hebu niambie utakuwa na ujasiri wa kukaa kimya? @ BADILI TABIA. Baada ya wiki mbili Mama anadai fidia ya shilingi miliioni moja kwamba ametukanwa...
huyo mama amemgeuza mwanae mtaji
 
  • Thanks
Reactions: SG8

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,785
2,000
Nisome vizuri mpendwa, ukijibu calmly itamfanya akuogope na akae mbali na wewe. Confrontations ni mbaya sana. Kwani ungemgeukia mkeo na kumuuliza unataka kwenda na mamako akakutunze vizuri zaidi ya ninavyokutunza? Dawa yake umsikie atakavyojibu mbele ya mamake.

Mjinga hapo ni mkeo, angemkemea mama yake kuwa hujui hali yetu na hayakuhusu haya yasingetokea. Na isitoshe mkeo ni mgonjwa sawa, lakini huhitaji kuacha hela ya matumizi kwa mama mkwe wala mamako kama yupo. Mkeo haumwi akili, anahitaji kupumzika. Kutoka alipolala hashindwi kusema mkanunue mchicha na mifupa tuchemshe supu. Binafsi hakuna anaeweza kuhoji matumizi ya fedha nyumbani kwangu unless anachangia budget, na sihitaji kujieleza. Nikiachiwa elfu kumi, mama atasikia namuagiza dada akalete nyama nusu kilo, matunda ya buku etc. Hapo kuna mjadala tena?

Ndo maana naona umuhimu wa kulindana na kujenga himaya yenu isiyoingiliwa na yeyote. Huwezi kuishi kwa std ya nyumbani kwao mwenza wako! Na mwenza wako akijua hili maisha yanasonga.

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,462
0

Usikae kimya.Si kakuomba ruhusa akamuuguze mwanaye mwenyewe?
Mwambie " sawa mama mkwe, haina shida hata kidogo.Basi mcukue tu maana naona utakua umenisaidia kwa kweli.Asante sana kwa msaada."
Kama alikua anatafuta ugomvi na wewe, utakuwa umemmaliza kisayansi.
 
prianka

JF-Expert Member
Aug 29, 2012
684
195
me nawashauri kua wavumilivu na kuishi kulingana na tabia ya huyo mkweo kwa maana wengine unaweza kubishana nao ukaumiza kichwa chako
 
Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
Hakuna sababu ya kujibizana vibaya na mtu yeyote awe ndugu yako au ndugu wa mume/mke wako. Jenga tabia ya kujiamini na siku zote jitahidi kutenda yaliyo ya haki na inapotokea umetenda kinyume uwe mwepesi wa kuomba msamaha. Jitulize, jifunze kukaa kimya na kutafakari kabla hujajibu lolote, usikurupuke, tambua jambo na nyakati za hatari, mdomo wako uwe mzito kutamka usiyokuwa na uhakika nayo. Hii itakusaidia kuishi vizuri na kila mtu, popote.

Ogopa kujiandaa kwa magonvi, yaani usiwe mwepesi kuwaza kuwa eti mtu akija kwenye 18 zangu namlipua, hapana usijiandae kwa mabaya, siku zote waza yaliyo mema. Jifunze kuuepuka uovu. Katika dunia hii hakuna aliyekamilika, kuwa mwepesi kujishusha na kuzielewa tabia za wengine. Jitahidi kuzizuia hasira zako. Simamia msimamo wako usiyumbishwe.

Umenena vema happiness win
 
Last edited by a moderator:

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,929
2,000
Nisome vizuri mpendwa, ukijibu calmly itamfanya akuogope na akae mbali na wewe. Confrontations ni mbaya sana. Kwani ungemgeukia mkeo na kumuuliza unataka kwenda na mamako akakutunze vizuri zaidi ya ninavyokutunza? Dawa yake umsikie atakavyojibu mbele ya mamake.

Mjinga hapo ni mkeo, angemkemea mama yake kuwa hujui hali yetu na hayakuhusu haya yasingetokea. Na isitoshe mkeo ni mgonjwa sawa, lakini huhitaji kuacha hela ya matumizi kwa mama mkwe wala mamako kama yupo. Mkeo haumwi akili, anahitaji kupumzika. Kutoka alipolala hashindwi kusema mkanunue mchicha na mifupa tuchemshe supu. Binafsi hakuna anaeweza kuhoji matumizi ya fedha nyumbani kwangu unless anachangia budget, na sihitaji kujieleza. Nikiachiwa elfu kumi, mama atasikia namuagiza dada akalete nyama nusu kilo, matunda ya buku etc. Hapo kuna mjadala tena?

Ndo maana naona umuhimu wa kulindana na kujenga himaya yenu isiyoingiliwa na yeyote. Huwezi kuishi kwa std ya nyumbani kwao mwenza wako! Na mwenza wako akijua hili maisha yanasonga.
Of course nakuelewa unachojaribu kusema hapa....Hii ni story imemtokea rafiki yangu. For sure binafsi ilinikera kwa sana kwa sababu jamaa akiongea na mkewe wanaelewana vizuri...akienda kazini jioni anakuja kukuta mambo yale yale....Ni kweli kabisa anayepaswa kulaumiwa hapa ni Mke, anayeruhusu Mzazi wake aendeshe nyumba yake...Pointi yangu hapa ni kwamba tusifanye generalization kwamba Wazazi wetu wote wako perfect...kwa utafiti wangu mdogo tu (sio lazima uwe wa kweli) wazazi wa kike (hasa ambao ni single) ni tatizo sana. Jambo la muhimu ni ku keep distance, muwe mnakutana kwenye matatizo tu basi (where necessary lakini)
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,929
2,000
Usikae kimya.Si kakuomba ruhusa akamuuguze mwanaye mwenyewe?
Mwambie " sawa mama mkwe, haina shida hata kidogo.Basi mcukue tu maana naona utakua umenisaidia kwa kweli.Asante sana kwa msaada."
Kama alikua anatafuta ugomvi na wewe, utakuwa umemmaliza kisayansi.
Imagine familia zetu za Kiafrika, Mama yako Mzazi pia amekuja kuuguza mgonjwa aliyejifungua halafu Mama Mkwe anaomba akakusaidie kuuguza utakubali na kumwambia mama yako arudi kijijini kwake alikotoka au utasema na yeye aambatane na mgonjwa?
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,785
2,000
Nakubaliana na wewe. Kwanza mie sioni sababu ya mama mzazi.kuja kuhudumia.mzazi. Kama inalazimika aje basi 2 weeks ndo maximum. Kwani anashindwa kuhudumia mkewe for the first week? Kuna housegal na utaratibu wenu wa maisha, mzazi anashindwa kuambia dada chemsha nyama unipe supu?

na kama hali inajirudia, dawa ya huyo mama unamuambia aondoke na mwanae, na humpi fedha. Kama mwanamke ana akili hataondoka na atajua mwenzie kakasirika. Ukikasirika huongei maneno mengi, saa zingine mama mkwe unamkata jicho tu anajua kavuka mstari. Mie hata unisimulie.mama mkwe kanisema, simuulizi ng'ooo, nikikutana nae namchekea hadi ajishuku mwenyewe kama najua ama sijui.
Of course nakuelewa unachojaribu kusema hapa....Hii ni story imemtokea rafiki yangu. For sure binafsi ilinikera kwa sana kwa sababu jamaa akiongea na mkewe wanaelewana vizuri...akienda kazini jioni anakuja kukuta mambo yale yale....Ni kweli kabisa anayepaswa kulaumiwa hapa ni Mke, anayeruhusu Mzazi wake aendeshe nyumba yake...Pointi yangu hapa ni kwamba tusifanye generalization kwamba Wazazi wetu wote wako perfect...kwa utafiti wangu mdogo tu (sio lazima uwe wa kweli) wazazi wa kike (hasa ambao ni single) ni tatizo sana. Jambo la muhimu ni ku keep distance, muwe mnakutana kwenye matatizo tu basi (where necessary lakini)
 
  • Thanks
Reactions: SG8

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,348
2,000
Maisha ya kisasa kuishi na watu ni ngumu sana,,kila kitu lawama, na ki africa kuishi familia moja as baba , mama, watoto wenyewe ni ngumu sana,, sasa hapo mama mzaz wa mume yupo, na wa mke nae yupo si kunaweza gombanisha wazaz,,

Mungu anisimamie wife akizaa nikae nae home tu na msaidiz wa kaz, as kwetu au kwao ataenda 2 weeks za mwanzon tu mimba ya kwanza.. Akapate direction ya anatakiwa aweje after that anarud geto kwa kamanda maisha yanasonga.. Kuishi na ndugu ni kazi sana especially wa kike
 
Fixed Point

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
11,310
1,225
sijawahi kujibizana nao ila kama mara 2 hivi nimewahi kuwakalisha kitako na kuwaambia yangu ya moyoni......wakaniomba msamaha, tunaendelea kama kawaida
 
KUN

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
380
225
mimi huwa nakaa nao mbali sana ili kuepusha migongano km hiyo, nimeweka utaratibu wa kuwa nawapigia simu mara 1 tu kwa mwezi kuonana ndo usiseme japokuwa wote tupo mjini hapa.
 
Double K

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
907
225
hakuna sababu ya kujibizana vibaya na mtu yeyote awe ndugu yako au ndugu wa mume/mke wako. Jenga tabia ya kujiamini na siku zote jitahidi kutenda yaliyo ya haki na inapotokea umetenda kinyume uwe mwepesi wa kuomba msamaha. Jitulize, jifunze kukaa kimya na kutafakari kabla hujajibu lolote, usikurupuke, tambua jambo na nyakati za hatari, mdomo wako uwe mzito kutamka usiyokuwa na uhakika nayo. Hii itakusaidia kuishi vizuri na kila mtu, popote.

Ogopa kujiandaa kwa magonvi, yaani usiwe mwepesi kuwaza kuwa eti mtu akija kwenye 18 zangu namlipua, hapana usijiandae kwa mabaya, siku zote waza yaliyo mema. Jifunze kuuepuka uovu. Katika dunia hii hakuna aliyekamilika, kuwa mwepesi kujishusha na kuzielewa tabia za wengine. Jitahidi kuzizuia hasira zako. Simamia msimamo wako usiyumbishwe.

yote yanawezekana kama haukai nao nyumba moja ila kukaa nao nyumba moja ipo siku mtajibizana haswa maana wazazi wengine wanadandia mambo hayawahusu. Wanataka muishi kama yeye alivyoishi na mumewe, inabidi kwanza atambue hiyo inakua ni ndoa nyingine kabisa na ina sheria zake.
 
Dina

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
3,146
2,000
Kujibizana na wakwe ni utovu wa adabu kwa kiwango cha juu na hakuna sababu yoyote itakayohalalisha.

Mkwe ni mzazi wa mwenzio.Ukimjibu vibaya ujue mwenye mzazi wake ataumia sana rohoni.
Unachopaswa kufanya pale mkwe kakuboa kupita maelezo ni kumwachia mwenye mzazi wake achukue uamuzi.
Wewe usimjibu mzazi wa mwenzio, mjibu mzazi wako mwenyewe ikibidi.

Nakubaliana nawe, japo nina maswali ya nyongeza. Tunafanyaje pale ambapo mwenye mzazi naye hasemi kitu, ukumbuke naye ana mtazamo kuwa mzazi wake hakosei.

Sijaelewa kipande cha mwisho, mzazi wangu namjibuje wakati hapa nina-deal na mzazi wa mwenzangu?
 
  • Thanks
Reactions: SG8

happiness win

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,462
0
yote yanawezekana kama haukai nao nyumba moja ila kukaa nao nyumba moja ipo siku mtajibizana haswa maana wazazi wengine wanadandia mambo hayawahusu. Wanataka muishi kama yeye alivyoishi na mumewe, inabidi kwanza atambue hiyo inakua ni ndoa nyingine kabisa na ina sheria zake.

Hapana. Ukikaa nao nyumba moja ni rahisi sana kuwaepuka maana utakuwa umewasoma na kujua tabia zao, hii itakusaidia kujipangia misimamo yako ya uhakika na itakufanya ujiamini zaidi na itakufanya usijibizane nao hata waseme nini maana penye ujinga utadharau na utasimama kwenye ukweli bila kelele nao wataishia kuguna tu maana una usimamo na huna majibizano nao!
 
WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,462
0
Imagine familia zetu za Kiafrika, Mama yako Mzazi pia amekuja kuuguza mgonjwa aliyejifungua halafu Mama Mkwe anaomba akakusaidie kuuguza utakubali na kumwambia mama yako arudi kijijini kwake alikotoka au utasema na yeye aambatane na mgonjwa?
Usipoangalia vizuri utageuka mwamuzi wa "sakata" la mama mkwe na mama mzazi.
Always avoid hawa wamama wasikutanie kwako. Utaambulia laana.
 
  • Thanks
Reactions: SG8

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom