Kujengea Watoto Utamaduni wa Kupenda Kusoma

Jielewe

Member
Jan 10, 2017
39
62
Kusoma si tabia nyepesi kuijenga katika mazingira ambayo masimulizi na mazungumzo ni vyanzo vikuu vya maarifa kuliko maandishi. Tumelelewa katika utamaduni usiosisitiza sana umuhimu wa kusoma. Lakini, hata hivyo, hatuwezi kukwepa kusoma katika ulimwengu huu unaotulazimisha kuyasaka maarifa kwa njia ya maandishi.

Kadhalika, mafanikio ya mtoto kitaaluma yana uhusiano wa moja kwa moja na utamaduni wa kujisomea. Mtoto asiyependa kusoma anajiweka katika hatari ya kuwa na mafanikio dhaifu kielemu kwa sababu, katika mfumo wa elimu, kusoma si uamuzi binafsi.

Kwa hivyo, ikiwa tunatamani watoto wetu wafanikiwe kielimu sambamba na kujenga utamaduni wa kujisomea bila kushurutishwa, tunao wajibu mkubwa wa kuwajengea utamaduni huo tangu wangali wadogo.

Katika makala ifuatayo tunaangalia mbinu nne rahisi zinazoweza kuwasaidia watoto wetu kupenda kusoma.
 
Back
Top Bottom