Kujenga ukuta Mererani haitaweza kutatua tatizo la utoroshaji wa madini

Kweli kabisa suala la ukuta lilikuwa suggested na team ya wataam baada ya madini ya Tanzanite kuusishwa na ugaidi watz tatizo lao kila mtu mjuaji
Ila mheshimiwa rais ameliwekea msisitizo anaonekana tofauti kabisa.

Watz tunajifanya wajuaji sana mkuu. Namtakia mheshimiwa rais asilegeze msimamo wake.
 
Uzuri inajulikana, Kwa Tanzania hakuna jambo utakaloanzisha lisipingwe, bora tu kukaza uliposhika OVA
Sawa kabisa uncle, ukuta lazima uwepo, kupunguza wizi wa kijinga, swala atakayeiba akipatikana, namhurumia...
 
Ushirikisheaji wa wananchi ndio njia rahisi na endelevu na pia itakayokuwa na tija kwa Taifa. Hii ya ukuta itaongeza smugling ya Tanzanite badala ya kupunguza huku ikiwaongezea wananchi mzigo.
 
Utajenga ukuta sawa utapata wapi waaminifu wa kuulinda huo ukuta mbele ya pesa,cha muhimu wanunuzi wakubwa wanaogopa mererani sababu ya jiografia yake kiusalama pia,ijengwe point maalumu yaani soko kubwa La ununuzi wa madini lenye facilities zote za kuwezesha mazingira rafiki Kwa wafanyabiashara na taasisi zote.Ukuta na ukali hauwezi shinda nguvu ya Pesa.
 
Napendekeza tujenge UKUTA nchi nzima ili kuwadhibiti wezi wa mali asili zetu - tuanchie gate moja tu la kuingilia na kutokea nchini. Tena hawa wazungu wakipita getini wasachiwe saana maana hawa ndiyo suspect numberi one.
 
Napendekeza tujenge UKUTA nchi nzima ili kuwadhibiti wezi wa mali asili zetu - tuanchie gate moja tu la kuingilia na kutokea nchini. Tena hawa wazungu wakipita getini wasachiwe saana maana hawa ndiyo suspect numberi one.
Ha ha ha!
Analogy kali, a.k.a Trump!
 
Km za mraba 87 wow thamani ya tanzanite inatokona Na mauzo ya nje hao wazungu wakisabotage soko? Na hizo tanzanite chini zimemebaki kiasi gani? Kufidia gharama Na kuleta faida au ndo kujenga kila Kona kujenga jamaa bado anadhani yupo wizara ya ujenzi au
 
View attachment 593349
Pamoja na nia njema ya Rais wetu kudhibiti Tanzanite katika machimbo huko Mirerani, hii ya kujenga ukuta kuzunguka eneo zima la Mirerani laweza kutotatua tatizo hata kwa chembe.

Tukumbuke tunaongelea wachimbaji, huko wanaitwa nyoka!

Sifa kubwa ya hawa wachimbaji wadogo ni kukosa any sort of order katika uchimbaji wa madini hayo.

Ugomvi mkubwa wa Tanzanite One na hawa achimbaji wadogo ni kwamba wakifika huko chini ya ardhi, its a lawless land down there.

Nyoka anafuata mkondo wa jiwe la Tanzanite kule linakoenda iwe juu, chini, mashariki au kusini.

Jiwe likienda hata nje ya mipaka mliyowekeana juu ya ardhi huko chini hakuna beacon ya kuonyesha hiyo mipaka.

Changamoto yangu hii hapa:
Je mtu tayari amejengewa ukuta, na ana mawe yake mfukoni, kwani kuchimba mtaro mwingine chini ya ardhi ili kutorosha atashindwa nini?

Hili ni swala mbalo huko Israeli waPalestina wanawasumbua sana waYahudi katika kuingiza silaha huko ukanda wa Gaza.

Si vibaya wizara ya madini ikalifikiria hili kwa makini.
Nia ya Ras ni njema, lakini methodology ya kutatua tatizo ina ukakasi.

Kibonzo source: The Guardian, leo 22/9/2017
You can not stop stealing instead control
 
Pingapinga naona mmeshavamia kama kawaida yenu. Ukuta utajengwa na vifaa vya ulinzi vitawekwa. Endeleeni kujidanganya muone kama mnaweza kushindana na Serikali inapoamua Jambo na kutilia mkazo. Mnafikiri kwa nini jukumu hilo wamepewa JWTZ na sio kandarasi za kawaida! MAJIZI ya rasilimali zetu Mtajuta kuifahamu serikali ya awamu hii.
 
Kujenga ukuta ni muhimu sana Madini yanayoibiwa kuptia juu na hao wamiliki wa Tanzanite One ni mengi sana kulinganisha na yanayoptshwa kwenye mitobozano under ground japo na wataalam wafkrie kuhusu kudhibiti njia za Under group
 
Najiuliza anavyovisemaga jukwaani huwa vinakuwa vimejadiliwa kwa kina na wasaidizi wake kweli?

Ila ngoja tujifunze kukaa kimya anapofanya kazi yake!
 
Ukutabutasaidia kudhibiti kuliko ilivyo sasa.. Hujui mzigo umetoka kiasi gani na umetolewa na nan
 
Misukule pingapinga naona mmeshavamia kama kawaida yenu. Ukuta utajengwa na vifaa vya ulinzi vitawekwa. Endeleeni kujidanganya muone kama mnaweza kushindana na Serikali inapoamua Jambo na kutilia mkazo. Mnafikiri kwa nini jukumu hilo wamepewa JWTZ na sio kandarasi za kawaida! MAJIZI ya rasilimali zetu Mtajuta kuifahamu serikali ya awamu hii.

Angalia sana mkuu, msukule unaweza kuwa wewe usiyejua kutumia akili ingawaje umejalia kuwa na kichwa kizuri.

Kichwa kisiwe cha kutunzia nywele na kuzichana kila asubuhi, kitumie kufikiri vile vile, na ukumbuke kuwa kichwa si pambo!

Tunatoa maoni mbadala ili uchumi na rasilmali zetu ziwatumikie watanzania vile vile na si wageni.

Nyie msio na uwezo wa kuafakari mawazo mbadala, kuboresha hali iliyopo ni bora mkapige deki vyoo ingalau mtumike vizuri.
 
Back
Top Bottom