kujenga uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kujenga uchumi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nmkenda, Mar 6, 2006.

 1. n

  nmkenda Member

  #1
  Mar 6, 2006
  Joined: Mar 6, 2006
  Messages: 11
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Eti mwenzenu mimi sioni kama tunaweza kujenga uchumi imara bila kuwa wazalishaji. Biashara sioni kama ni muhimili wa jishikilia.
  Mimi nikiangalia nchi nilizochagua (sijui zingine) zimepanda kwa kusimamia vizuri rasilimali zake. Baada ya hapo biashara inakuja tu bila kupenda.
  Mfano China ni mkakati mkubwa sana wa kilimo, viwanda vikubwa na migodi.
  Urusi wali identify resources zao kama madini nk.
  Marekani Waarabu, South Afirica etc.

  Kwa kweli tusipokuwa wakweli kwa nafsi zetu tutaumbuliwa hadharani vibaya sana kama huu mradi wa TANESCO ambao hata hauvutii kujadili.

  Wafanya biashara watakuja tu, serikali iweke mkazo kwenye uzalishaji.
  Resources zetu ni ardhi kwa kilimo madini na mifugo pia utalii.
  viwanda vitokane na hayo na visimamiwe na waadilifu wakijua hapo ndio pa kujengea nchi au pa kuiulia.
  Ningependekeza jina la nchi yetu lijulikane kwa umaarufu wa hayo yote. Kila moja na uzito wa kutosha.
  Mfano wasiwepo watu wasio na uwezo katika hizo sekta, kwa sasa panatakiwa uwajibikaji wa haraka na ufanisi wa hali ya juu kujitoa shimoni zilipo na kuanza kupanda.
  Chonde chonde wanasiasa sikilizeni wataalamu,
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Mar 6, 2006
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,433
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Heshima yako NMKENDA,
  Kusema kweli hili swala zito sana!...nakubaliana na wewe kwa mapana kama alivyochangia ndugu yetu Poloz huko kwenye siasa. Kusema kweli nashindwa kabisa kuelewa elimu ya kitabu yaani economics inahusishwa vipi na mazingira yetu.
  Mfano wako hapo juu tosha kabisa kutufahamisha kwamba, wasomi wetu sijui niseme viongozi maanake TZ viongozi wenyewe ndio haohao wasomi wanaotoa maamuzi ya ujenzi wa taifa hili. Kiutawala tu tayari tumekwisha changanya mchuzi na ndio maana viongozi wetu wana kiburi hawaambiliki.
  Ni kweli kabisa maneno yako ukiangalia tunakokwenda kiuchumi inaonyesha wazi bishara imepewa kipaumbele mbele ya Uzalishaji.. sasa sijui hiyo biashara ni ya kudumu ama tunaweka mkazo pale kwenye mirathi tuliyoachiwa na Mungu....mali asili tu.
  Ebu tazama toka uhuru, miundombinu kama reli ya kati na hiyo ya kaskazini imeshukashuka chini mwaka hadi mwaka haina ukarabati. na ukitazama kwa undani utakuta pato la mashirika haya yameshuka mwaka hadi kwaka na sababu kubwa ni ukosefu wa bidhaa!... yaani uzalishaji umepungua. Cha ajabu ni kwamba kila mwaka hata kama hizo statistics zinaonyesha kupungua kwa uzalishaji bado serikali yetu imefunga mkanda ktk sera ambazo zinazidi kupotosha kabisa malengo. Hatuwezi kufikia kujitegemea ikiwa Watanzania hatutaweza kuzalisha wenyewe mazao, mali ghafi za viwanda na hata finished product nchini. Na wala sijui nani wa kulaumu kwani wakulima na wenye viwanda pia madai yao nchi yetu haina maji wala umeme kuendesha shughuli zao. hawana budi kufunga virago na kutafuta riziki sehemu nyinginezo zisizotegemea maji wala umeme kwa wingi....
  Hivi kweli tutafika?
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,124
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  ...wind energy ndio itatuondolea matatizo yetu ya umeme sio vinginevyo..Germany sasa wamefikia 110,000 MW from wind energy,Tanzania nchi nzima hata hatuhitaji 1000MW na approx. cost za kujenga 100MW hazifiki hata 100m$,huku Richmond na IPTL tuliwapa 100's of millions kwa umeme ambao unatucost milele...Wind technology imemprove sana miaka ya karibuni,jamani we need that kama kuna mhusika humu afanye kazi yake...information zote zipo kwenye internet,hope tutaweza kuwa exporter wakubwa wa UMEME na viwanda vyetu tukaweza kuzalisha kwa bei rahisi,kwa ufupi tutawasha engine yetu ya maendeleo maana umeme ni kila kitu(ENERGY)
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,856
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Koba,
  1. Wind poa- naunga mnoko!
  2. Serikali yenyewe itengenge fungu la pesa pia kuwasaidi wawekezaji wazawa wakubwa kufungua viwanda vikubwa. Au watoe guarantee-manake vingi vilivyopo sii vya wazawa! sisi ni vibarua tu! Mimi bado sijaona juhudi ya makusudi -ZA wana Black Empowerment Scheme! Sisi hapa tunaongea tu kuwaleta wawekezaji wa nje!
  3. At the same time kuimarisha miundo mbinu
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,526
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  Hali yako muheshimiwa NMKENDA,tatizo ni kwamba nani atamfunga paka kengele ikiwa viongozi wote wa bongo ni wababaishaji??
   
 6. Philip Dominick

  Philip Dominick JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2013
  Joined: May 26, 2013
  Messages: 1,026
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  nasikia mabasha washanunua tiket kwa ajil ya show
   
Loading...