Papa Mopao
JF-Expert Member
- Oct 7, 2009
- 4,107
- 2,506
Mshahara kwa mwezi ni laki tatu, nia ya kujenga nyumba ipo moyoni kabisa, sasa kwa mtu kama huyu afanyeje ili ndoto yake ya kujenga nyumba itimie?
Jipe muda ndoto yako utaitimiza. Ushauri wangu, anzisha mradi wowote ili hiyo pesa izunguke kwanza.Mshahara kwa mwezi ni laki tatu, nia ya kujenga nyumba ipo moyoni kabisa, sasa kwa mtu kama huyu afanyeje ili ndoto yake ya kujenga nyumba itimie?
Mshahara kwa mwezi ni laki tatu, nia ya kujenga nyumba ipo moyoni kabisa, sasa kwa mtu kama huyu afanyeje ili ndoto yake ya kujenga nyumba itimie?
wasikukatishe tamaa unaweza kuwa unalipwa laki mbili ukajenga nyumba na yule anayelipwa milioni mbili akashindwa kujenga. cha msingi jitambue kipato chake ni kiasi gani na utambue kwa kipato hicho unaweza kujenga nyumba ya aina gani na maeneo gani. Njia rahisi kwa wenye kipato kidogo ni kujenga kwa awamu kwa mshahara wako kama hauna kiwanja ukiamua ndani ya mwaka mmoja unapata kiwanja, sio masaki wala mbezi beach ila utapata (lakini kama hauna matumizi makubwa katika mshahara wako) ukishapata kiwanja kuwa na ramani ya nyumba unayotaka kujenga alafu inua vyumba kama viwili na ukishahamia unajenga taratibu kadiri unavyoweza. ndani ya miaka miwili unaweza ukawa unaishi kwako tena pakiwa bora kuliko unapopanga ikiwa utakiwa makini kuchagua fundi na kumsimamia. ukisubiri kuinua kipato inawezekana usijenge kabisa na kujenga ni njia moja wapo ya kuinua kipato kwa kuepuka kodi ya nyumba
ndg ushauri wangu achana na hayo mawazo kwa sasa kipato chako ni kdg sana kuza kwanza kipato chako ndio ufikirie ujenzi
Jipe muda ndoto yako utaitimiza. Ushauri wangu, anzisha mradi wowote ili hiyo pesa izunguke kwanza.
If u succeed bridging the gap between expectations and reality, u'll b in a better position.
U obviously have big dreams (u name suggests) but not much in the cup..
Kama umeshapata plot, sehem ya kichanga, save money for a whille ifike 1m, nunua cement, kodisha mashine lipa mafundi ufyatue matofali.. And move on from there.
But still be real and think right.
ushauri wa bure, sio kila tunachokipenda ni lazma tukifanye kwa wakati huo ila mazingira yanaamua. Kuwa na subira ila bana matumizi na anza kubuni mradi wa kukuongezea kipato. Ukiwa na uhakika wa kupata elf 15 kwa siku nje ya mshahara wako unaweza jenga