Kujenga miundombinu na kuruhusu wamachinga wasibughudhiwe ndio kusema kunafuta madoa ya utawala wa hayati Magufuli?

Nchi zote unazoona zimesimama duniani zimemwga damu hasa kuwandoa wasaliti Rwanda leo mnapenda kuitolea mfano ila fuatilia historian take miaka 10 nyuma. utajua kwamba hakuna mamlaka takatifu.
Una akili timamu au unalazimisha kujadili mada hii?
 
Naomba kuuliza itifaki inasemaje makamu wa raisi alivyoenda kumtembelea Lisu aliomba ruhusa kwa hayati Magu?
Hakwenda kiofisi. Alipitia tu dk.2 alipokuwa kwenye shughuli zake Nairobi.

Aliyefunga safari kwenda kumtembelea Lisu alikuwa ni Lazaro Nyalandu na mzee Mwinyi.
 
Halina ubishi hata kiduchu kwa miaka yote tangu mwaka 1995 hayati JPM amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha barabara za Tanzania zinaunganika. Na kweli sasa hivi nchi imepiga hatua kwa kuwa na miundo mbinu mizuri. Pia alipokuwa rais wa JMT aliwakingia kifua wamachinga wasiwekewe kiwingu na kufanya biashara kwa uhuru wao.

Lakini hii pekee ndio inakuwa sababu ya kusema hakuna madoa yaliyowekwa na uongozi wake au utawala wake?

Muamar Ghadafi alitengeneza taifa lililokuwa na miundo mbinu mizuri tena ya kisasa kuliko hata nchi za ulaya. Alihakikisha watu wanapata elimu bure,ndoa bure na chakula bure, lakini doa pekee lilimfanya mpaka akauliwa kwa fedheha ni ukatili dhidi ya binadamu, tena alioufanya kwenye gereza maarufu la Abu salim. Maana alikuwa hataki kukosolewa.

Ni kweli kabisa hayati JPM alikuwa mfuatiliaji na msimamizi mzuri ndio maana alifanikisha nchi ikawa na miundo mbinu mizuri, ndio kusema alitawala bila dosari?

Hiyo miundombinu yenyewe aliyojenga iko wapi wajamani? Au ni hii reli ambayo haijafikia hata 30% ya kukamilika kwake?
 
Angalau we unakiri Kuna mambo yamefanyika mengine hayo ni makosa ya kibinaadamu maana hamna binaadam aliyekamilka. Na hamna uongoz ambao watu hawajapotea kwa awamu zote
Magu amefanya makosa mengi kuliko mazuri,deni la taifa sasa ni 60 tri,yaani ni kubwa kuliko vitu vyote tulivyonavyo kama nchi
 
Hata Yesu hakukubaliwa na waisrael wote huo ndio utashi wa kibinaadamu hivyo hata JPM wapo wanao mkubali na wapo wasio mkubali hilo lazima liwepo kwa kuwa ndio hulka ya kibina adamu
Waliokuwa hawamkubali ni takribani 75%
 
Jibu hoja. nchi ipi takatifu au awmu ipi ni takatifu usikimbilie matus
Unataka kusema waliotekwa, kujeruhiwa, waliouliwa na kupotezwa walikuwa vitani? Amani haiji bila ncha ya upanga. Huu msemo hutumika kwa watu wanaopigana vita kujikomboa kwa watu madhalimu acha kupotosha watu.
 
Awamu ipi ilikuwa takatifu ambayo haijawai kutesa Wala kupoteza mtu Hilo ndo swali langu.
Halafu hata hao unasema wameteswa na kutekwa hebu waorodheshe tujue hata idadi yao. Si ajabu wasifke hata10 na bado hatuna ushahidi wa aliyewatesa au kuwateka, ni tuhuma tu.
 
Si ajabu wasifike 10...? Akili yako ilivyo ndogo unataka usikie habari za watu unaowajua au wanasiasa maarufu. Ndio maana ninakuhoji unazo akili? Kwa kwa kuwa awamu zote zilitesa na kupoteza watu ndio unaona ni swala la kawaida?
 
Angalau we unakiri Kuna mambo yamefanyika mengine hayo ni makosa ya kibinaadamu maana hamna binaadam aliyekamilka. Na hamna uongoz ambao watu hawajapotea kwa awamu zote

Basi waliopo magerezani wakatolewe kwani na wao wamefanya makosa ya kibinadamu. Unatetea viongozi madhalimu kwa kificho cha kutekeleza majukumu yao wanayolipwa mshahara!
 
Vibaraka wa Jiwe wamejitahidi kweli ku manipulate msiba ili ionekane Jiwe anapendwa sana , wamefanikiwa kiasi fulani ila uhalisia uko palepale wasiojulikana , watu kupotea , kutekwa , kufungwa kwenye viroba kufungulia watu kesi bandia za uhujumu uchumi , utakatishaji fedha , uonezi kufukuza watu kazi hovyo ,utumbuaji wa hovyo , ubomoleaji watu majumba ni baadhi ya sifa zake mbaya sana . Sasa swali hao walioenda kumuaga na kumzika ni wengi kuliko waliobaki ? Wasioenda ? Mataga ni empty set kwelikweli .
 
Hiyo miundombinu yenyewe aliyojenga iko wapi wajamani? Au ni hii reli ambayo haijafikia hata 30% ya kukamilika kwake?
Wanaunganisha lami zote kuanzia alipokuwa Waziri wa ujenzi enzi za Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kuwa zote hizo kajenga Magu.
Hawa wenzetu wanatushangaza maana kazi ni kujichukulia miradi yote eti kaijenga.Sifahamu hata hizo sifa za kujipa kwa miradi iliyotekelezwa kwa kodi zetu huwa ndiyo nini?
Nchi hazijengwi na tuliowapa madaraka Bali na wenye nchi yao.Ukiwa msimamizi haikupi uhalali wa kumiliki mradi na unalipwa mishahara na marupurupu yote kwa kazi hiyo.Tuwe wakweli,wanasiasa hupenda kujipa sifa si zao hata kidogo huku tukiwalipa kwa kutuongopea kila Mara.
Turekebishe tulipokosea kwa kukiri ukweli.
 
Nchi zote unazoona zimesimama duniani zimemwga damu hasa kuwandoa wasaliti Rwanda leo mnapenda kuitolea mfano ila fuatilia historian take miaka 10 nyuma. utajua kwamba hakuna mamlaka takatifu.
Sio kweli
 
Vibaraka wa Jiwe wamejitahidi kweli ku manipulate msiba ili ionekane Jiwe anapendwa sana , wamefanikiwa kiasi fulani ila uhalisia uko palepale wasiojulikana , watu kupotea , kutekwa , kufungwa kwenye viroba kufungulia watu kesi bandia za uhujumu uchumi , utakatishaji fedha , uonezi kufukuza watu kazi hovyo ,utumbuaji wa hovyo , ubomoleaji watu majumba ni baadhi ya sifa zake mbaya sana . Sasa swali hao walioenda kumuaga na kumzika ni wengi kuliko waliobaki ? Wasioenda ? Mataga ni empty set kwelikweli .
Alipofanya uswahiba na wale majirani wakamfundisha tabia hizo mbaya
 
Presha ya maandamano ya Mange Kimambi ililazimisha serikali ya Magufuli ichukue hatua fulanifulani kupunguza hasira za wananchi. Mojawapo ya hatua ilizochukua ni pamoja na kutolibugudhi kundi la wamachinga, maana hilo ndo kundi ambalo kama message ingewafikia halafu maisha yakawa magumu kwao basi wangeingia mtaani
 
Back
Top Bottom