Kujenga jengo la Bank (BoT) sio sawa na Kujenga banda la kufugia kuku

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Kujenga jengo la Benki ni gharama na sio kitu rahisi, Ingekuwa kitu rahisi basi hata Mimi nyumba yangu ningewapangisha Bank.

Tuachane na Bank za Biashara kwenye hii mada, Tujadili kuhusu Benk kuu ingawa hata Bank nyingi za biashara zinashindwa kufungua matawi kutokana na gharama za ulinzi wa vifaa vya kisasa, Ingekuwa Bank ni nyumba tu basi Kila Bank ingefungua tawi kila kona ya nchi.

Gharama za vifaa vya usalama vyenye kutoa tahadhari wakati wa moto, uvamizi au milipuko ni gharama kubwa.

Basement inatumia gharama kubwa zaidi hasa kwa BoT mfano BoT ya Dar es Salaam.

Kesi za akina Liyumba ziliishia wapi? Ilikuwa kelele tu za wanasiasa Wanaojua kuhesabu tofali na mabati, wanafikiri BoT ni lile jengo la nje yaani tofali na vioo.

Nchi zilizoendelea Jengo sio kitu hata kwenye Banda la nyuki Unafanya kazi, Wao wanaangalia usalama na vifaa vya kujilinda na hao nyuki.

Jengo la BoT Dar es Salaam, Ukiliangalia kwa kuangalia idadi ya tofali na vioo utasema pesa zimepigwa, Lakini ukifika ndani na vifaa vilivyofungwa vya kisasa utasema gharama ni sahihi.

Nimeshangaa kuhoji Jengo la BoT Mwanza kwa kuangalia idadi ya tofali na vioo badala ya kuangalia teknolojia inayotumika kujenga na kuhifadhi pesa.

Pesa sio kama mawe unaweza ukaziweka tu ndani, Pesa zinavunda, zinaharibika, Hivyo lazima vifaa vya kisasa vifungwe kunyonya hewa toka vyumba vya kuhifadhia pesa BOT na kuitoa nje.

Kama sio vifaa vya kisasa basi pale BoT Dar nje tungejaza vifaru, Drones na kila aina ya polisi kwa ajili ya kulinda Jengo na Pesa.

Teknolojia ya kisasa ndio iliyopunguza idadi ya walinzi na vifaru kuzunguka jengo.

Ni vyema wanasiasa wakaacha unafiki na watueleze kwa kina pesa zinahifadhiwa kama matofali hapo BoT?

Hizo strong room za pesa ni sawa na chumba cha kulala, Hapa na ongelea BoT.
 
Hivi vifaa vya usalama ni kutoka kwa beberu huyu huyu aliyekuwa anatupiganisha vita vya kiuchumi?

Kwani yale mahubiri ya kizalendo yaliishia wapi?
 
Hivi vifaa vya usalama ni kutoka kwa beberu huyu huyu aliyekuwa anatupiganisha vita vya kiuchumi?

Kwani yale mahubiri ya kizalendo yaliishia wapi?
Vifaa vinatoka kwa Mabeberu mpaka software zinatoka kwa Mabeberu

Software za Bank Equinox system, Flexcube system, Finacle system. zote zinatengenezwa na Mabeberu

Wahindi wa India ni mabeberu au sio mabeberu?

Lakini ili kupunguza gharama anakuwepo beberu mmoja akiwasaidia wazawa kufunga system za mabenk
 
Vifaa vinatoka kwa Mabeberu mpaka software zinatoka kwa Mabeberu

Software za Bank Equinox system, Fkexcube system, Finacle system. zote zinatengenezwa na Mabeberu...
Tuliingizwa chaka sana kuaminishwa kumchukia beberu.

Hata mhindi kwa tafsiri iliyokuwapo alikuwa ni beberu.

Kumbe beberu ni mwuungwana sana tuna mhitaji sana hata kwa usalama wetu na pesa zetu.

Udumu sana ewe beberu ambaye pamoja na kukuzodoa kumbe ni umburula wetu tu.
 
Back
Top Bottom