Kujenga highway Arusha-Musoma ni kuzuia great migration? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujenga highway Arusha-Musoma ni kuzuia great migration?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by S.M.P2503, Jun 14, 2010.

 1. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wana jamii, niombe radhi kama kuna kati yenu hapa amekishwa post baada ya kuona hii article toka kwa majirani zetu wakenya wanaodai kwamba barabara ya Arusha- Musoma ikijengwa itazuia great migration ya wanyama kwenda Kenya na hivyo watakosa soko la watalii, wanyama watauwawa yaani mass extinction na uharibifu wa mazingira Wa hali ya juu...

  Binafsi sikubaliani na article ya huyo mkenya maana kuna technolojia nyingi tu zinaweza kutumika ili kuwafanya wanyama waendelee na great migration yao.. hivyo kama majirani zetu wanaona wanaathirika , kwanini wasitoe alternative solution kama ya kujenga underground road/highway au tube toka hapo Arusha -Musoma ili wao wasiendee kulalamika.

  Wanafikiri kwamba kwa kufanya kampeni ili barabara isijengwe basi watashinda kama walifanikiwa kuzuia uuzwaji wa pembe za ndovu... article yeneye ni hii hapa chini isomeni toka  Tanzania Request Alternative Route

  For Highway Through Serengeti National Park

  Coastweek-- We are all sensitized to the human wildlife impact and its challenges being faced everyday in our country.

  Every year we loose hundreds of our precious wildlife to drought, disease, economic growth and effects of climate change.

  As Kenyans, we have at least recognized the importance of our wildlife heritage and are now beginning to do something about it.


  The rejection of opening up trade in Ivory stockpiles, restoration of the Mau and the likes of Nairobi Green Line tree planting initiative to conserve our Nairobi National Park is a perfect example of what we accomplished this year.


  But what if you found out that our Great Migration of the Masai Mara will end in 2012?


  Yes! In just two short years, not twenty or fifty, only two!


  How is this possible you ask?


  Because of a highway.


  A highway cutting right through the Serengeti National Park which will edge towards our borders next to the Masai Mara.


  Tanzania is at this very moment preparing a feasibility study to be completed in December this year for the construction of the new Arusha-Musoma highway by 2012.


  The proposed new road will start at Mto Wa Mbu which is at the base of the Manyara Escarpment, continuing along Engaruka, further passing Lake Natron , following into the Loliondo Sanctuary, and directly through the Serengeti literally splitting the park apart before reaching Musoma.


  This road is smack in the middle of the great migration path which comes into Masai Mara.


  Although this highway will be of considerable economic importance to Tanzania and it will improve their human migration, the opportunity cost however to wildlife and to us in Kenya will be ruinous.


  The effect on our tourism would be colossal if the migration was slightly tainted or even destroyed.


  Kenya ’s tourism within the Mara and beyond will be seriously affected as inflows of tourism dollars will be diverted towards other international destinations that have parks or beaches.


  Local investment and thou-sands of jobs in the hospitality, tourism and corresponding industries will be lost.

  The Masai Mara and Serengeti are unquestionably the most profiled parks on this continent and only because of the largest animal migration on our planet.

  Thousands of Wildebeest, Zebras and other herbivores cross over from Tanzania into Kenya and return back, as they search for fresher greener pastures, to breed and to deliver new offspring.


  This routine which is driven by instinct and has been followed for centuries will now have a highway directly in its trail.


  Our Mara predators such as Lions, Cheetahs and Hyenas who have carefully timed the birth of their young to coincide with this migration and are desperately awaiting the arrival of the herbivores after a prolonged period of hunger, may be wiped out by starvation.


  The new highway could support hundreds of coaches, large trucks and other vehicles traversing each day.

  Imagine thousands of Wildebeest lined up on the side of this highway, all disoriented, scared and unable to cross the large tarmac into the Mara.

  Consequently forcing them to return into Tanzania .


  Imagine the wildlife massacres and human losses from the road accidents, the air pollution, noise pollution and increased levels of poaching.


  As a wildlife photographer, I am appalled, and the same sentiments are being expressed by our local safari guides and operators who also predict that this mass migration will now stay confined; into just a Tanzanian wildlife spectacle.


  There is already an inter-national outcry from environ-mentalists about the ecological impact and petitions are already flying all over the internet.


  Are we as Kenyans going to sit back? or are we also going to voice our concerns?


  I’m already trying to do my part.


  We and our government have a duty to reason with our COMESA neighbours.


  Tanzania , can you seek an alternative route which is outside the national park.


  If not, we should possibly bid farewell to the migration and say kwaheri to a world heritage site… the Masai Mara will die.


  Kasmani Shazaad
  , Mombasa .
  shazaadk@hotmail.com


  source:
  http://www.coastweek.com/3324-25.htm
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,059
  Trophy Points: 280
  ..nadhani juhudi zifanyike hiyo barabara isikatize ktk mbuga ya wanyama na kuathiri hiyo migration.

  ..bila hata shinikizo la Wakenya, wa-Tanzania tunapaswa kuitunza hiyo migration ya wanyama kwa vizazi vijavyo.

  ..pia kwa miaka mingi kumekuwepo na proposal ya kujenga reli ya Tanga-Arusha-Musoma.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jun 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa mawazo yao yako Tanzania kama vile hawana kwaoi. Kila linalotokea Tanzania wanalipigia kelele kama vile ni la kwao. Sijui ukifika muda huo wa jumuia mambo yatakuwaje.
   
 4. bona

  bona JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  I never heard some of our leader are thinking of that, i am Tanzanian but for sure this is the issue which does not need to be kenyan or tanzanian!

  There should be no tarmac road in national parks for whatever reason, infact personally i am furious with the government after it allow normal passenger buses goin to Musoma to pass across Serengeti as transit, this route should be the last alternative, all passengers should be passing to Mwanza via Singida and goin to Musoma!

  This plan should be condemned by all concerned individuals!
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Popote tu tupite maana sio wote wana uwezo wa kuwaona hao wanyama serengeti. Mbona highway inapita katikati ya Mikumi lakini wanyama bado wanaishi tu? reason ya hao wanyama kwenda kwa mtani wa jadi inajulikana sasa sijui kama highway itabadili hiyo reason? :roll:
   
 6. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kama unaijua vizuri Jiografia ya nchi yako Tanzania, nadhani wazo lako si sahihi kwa kipindi hiki kwani hakuna njia ya Arusha-Musoma ambayo itajengwa bila ya kupitia Hifadhini. Ni kutokana na ukweli huo, ndio maana feasibility study inayofanyika ni kukwepa kupitia Hifadhi ya Serengeti na hiyo ndio option pekee. Be ware please.
   
 7. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kwahiyo tusijenge barabara kwasababu ya wakenya... Kwahiyo tuhesabu kuwa barabara hiyo haitakuja kujengwa milele kwasababu hiyo mbuga itatunzwa milele...hivyo watz waishi kwenye barabara chafu na maendeleo duni kwasababu ya kuogopa kuwa hurt kenyans....

  Kwani tatizo lao liko wapi.. wenyewe si wanasema wanataka tuwe federation, sasa wanyama waende kwao au wabaki kwetu sisi sote si wamoja... huo umoja wanaohubiri mbona wanaanza kulialia kuukataa sasa?

  ...kwasababu kama wao wanaona sisi sote ni kitu kimoja kwenye federation inayokuja, watadhurika nini kama wanyama wakibaki huku kwetu...si huku kwetu utakuwa mkoa tu?

  ...toka lini wahehe wa Iringa wamelalamika barabara ya Mikumi na reli ya TAZARA kutokana na wanyama waliotoka kwenye Udzungwa Game Reserve?

  ...hawa wanacheza hawa...nitashangaa kama serikali itasitisha maendeleo yetu kwasababu ya hawa jamaa.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,059
  Trophy Points: 280
  ChiefmTz,Ubungoubungo,

  ..kwa maoni yangu eneo la hifadhi ya Serengeti halipaswi kuingiliwa na barabara kubwa ya lami.

  ..pia nimeangalia ramani mbalimbali ili kujielimisha na eneo husika nikaona kwamba unaweza kutoka Arusha, ukaingia Shinyanga, halafu ukaendelea kwenda mkoa wa Mara. kwa msingi huo, kama nia ipo, tunaweza kabisa kuepuka kuingilia hifadhi ya serengeti.

  NB:

  ..kuna mahali nimesoma kwamba TANAPA wamekuwa consulted, na wamekubaliana na eneo itakapopita barabara. sasa i hope TANAPA hawakuwa pressurised kubadili mtizamo wao wa awali.
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Lini tunaijenga hii barabara? au mpaka rais atoke Mugumu?
   
 10. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo ujenzi wa barabara kukatisha National Park kama vile ilivyo Mikumi ni mwiko?

  Na eneo hilo ndo litabaki hivyohivyo maisha yote....hii mbona ajabu...wanyama hao na barabara kipi chenye faida..tukipiga mahesabu hapo, ndo tutachagua chenye maana zaidi...
   
 11. N

  Nyamera Member

  #11
  Jun 14, 2010
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 15
 12. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Khe khe khe mimi namtaka Hugo Chavez wa Tanzania atakayeivunja Hii Jumuiya na kuwasulubisha mafisadi. Hapo ndipo utakapo gundua kwa nini Nyerere alifunga mpaka na Kenya miaka ile. Uchumi tunao tumeukalia hivi hawa wasomi wetu tena wengi tu walisomeshwa bure na serikali kupitia kodi zetu wanafikiria nini?
   
 13. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hawa jamaa wanatutukana sana kule kwenye facebook..sijui kwanini.
   
 14. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Nyerere hakukosea alipofimga mpaka. Matusi hawakuanza leo hata hapa JF si unaona wanavyoporomosha matusi, hiyo ni silka yao wala yasikupe tabu tatizo tulilonalo ni hawa maharamia walioshika serikali kazi yao kubwa ni kujikombakomba na kufikiria matatizo ya Tanzania yatatatuliwa na wageni. The solution is right here at home.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hawa wakenya siyo wenzetu kabisa, mimi nimekuwa nalifahamu hilo tangu mwaka 1977, ndiyo maana sikubaliani kabisa na huu upuuzi wa shirikisha. Juzi juzi hapa jamaa mmja kaandika kuwa Tanzania haina barabara ni chafu; tukitaka kujenga wanakuwa wa kwanza kupiga kelel tusijenge. Ngoja tuone kama serikali ya CCM itakubaliana nao, ni hapa ninapoanza kufikiria kuwa na kiongozi kama Lowasa ( minus tamaa ya mali).

  Wote mnaokubaliana na madai ya kenya mnakosea kwa sababu kadhaa, nitajaribu kusema chache hapa chini.

  (1) Sehemu kubwa ya mbuga ya Serengeti iko Tanzania, ni sehemu ndogo sana iliyoko upande wa Kenya ambako inaitwa Masai Mara. Kwa hiyo kufuatia mzunguko wa wanyama, ni wachache sana wanaokatisha mpaka baina ya nchi hizo. Wengi wao wanaishi Tanzania; hebu angalia ramani hii hapa.


  [​IMG]
  serengeti.JPG

  (2) Barabara kupita kwenye mbuga za wanyama siyo jambo la ajabu kabisa; kuna mbuga nyingi ambamo barabara zinapita na wala wanyama hawajawahi kuhama. Mifano ni kama ifuatavyo:

  a) Hapo Serengeti kuna barabara inayotoka Arusha kwende Mugumu kupitia humo humo Serengeti. Barabara hii ndiyo ambayo serikali inataka kuwekea lami; ni barabara ya siku nyingi sasa, na kwa miaka nenda rudi ilikuwa inatumiwa na maloli ya mzigo kusafirisha biadhaa katia ya Musoma na Arusha, Tanga na DSM. Kwa miaka yote hiyo barabara hiyo imekuwa inatumika huku ikitimua vumbi sana wakati wa kiangazi na wakati wa masika kujaa matope yanayoweza kukwamisha magari na kuhatarisha maisha ya abiria. Ubovu wa barabara hii ndio uliosababisha raia wa Tanzania wakawa wanaamua kupitia Kenya kutoka Arusha kwenda Musoma au Mwanza.

  (b) Vile vile kutoka Mto Wambu kuna barabara nyingine inayopita hapo hapo Serengeti kwenda hadi Lamadi; hii nayo ni kama ile inayokwenda Mugumu.

  (c) Barabara ya Bunda Musoma karibu na Lamadi ndiyo mpaka wa mbuga za Serengeti, lakini wanyama wale hutembea sehemu zote za barabara kwenda ziwani na kila ukiipta saa za jioni utakutana nao mbona hawajahama eneo lile.

  (d) Huko Kenya kwenyewe, ile highway inayotoka Mombasa kweda Nairobi inapita katikati ya mbuga za Tsavo. Vile vile ile reli inayotoka Mombasa nayo inapita hapo hapo Tsavo; na barabara inayotoka Moshi kwenda Taveta nayo inapita katikati ya mbuga ya Tsavo.. Mbona wanyama wa Tsavo hawajahama.

  [​IMG]
  Tsavo.JPG


  (e) Kwa upande wa kusini mwa Tanzania, reli ya Tazara inapita katikati ya mbuga za Selous wakati Barabara ya Southern Highway nayo inapita ndani ya mbuga za Mikumi na wala wanyama wale hawajadhurika.

  Hizi propaganada za kenya ndiyo changamoto kwetu watanzania kujiuliza tena kama kweli hili shirikisho lina maana yoyote kwetu. Nimesoma kelele wanazopiga kule facebook nikalinganisha na jinsi walivyotufanyia kwenye swala la uuzaji pembe za ndovu, na mgogoro wa maji ya mto nile nikaona hapa hakuna ushirika wowote; ni utapeli mtupu.
   
 16. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mbuga ya selous inapitiwa katikati kabis ana reli ya Tazara inayopita kila siku na mangongongo na treni za abiria, mbunga ya mikumi inapitiwa na barabara inayopitiwa na magari kila siku usiku na mchana lakini bado ipo, magari yenyewe yatakayokuwa yanapita huko mara ni mangapi jamani si yakuhesabu tu, mbona hawa jamaa wanatuoneaga sana ati...kipindi kile wamezuia machimbo ya magadi ziwa natron, tukakubali, sasaivi wanazuia hii tena...hawataki kabisa tuendelee kuwapita.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Are these people serious.. since when animals don't cross a road? hivi kule Mikumi wanyama huwa hawavuki barabara? what if when it get somewhere in the Serengeti the road is lifted on about 5 miles of pillars so the animals wapite chini yake? watakuwa bado na tatizo?
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu asante kwa kuniamsha........mimi nilishikwa kigugumizi baada ya kuona hii post hasa kutokana na majibi ya harakaharaka ya waTZ wenzetu(au ni imposters sijui wanisamehe).....ESIA ilifanywa na wataalamu wa wanyamapori ambapo makubaliano ni kuwa yale maeneo yeneye njia asili za wanyama pajengwe madaraja wanyama wapite chini.....huyu mwandishi wa Kenya amethibitisha mwenyewe kuwa wanyama hawa wan njia zao wenyewe ambazo wataalamu hawa wamwzitambua.....bara bara yenyewe inapita kwenye narrow patch of the Serengeti in the norht of it(Longido) amabapo ni hardly 200km....sasa sijui wao shida ni kukosa mapato au nini.....tulipoamua kujenga Aiport mugumu walipiga kelele kweli na sijui huo mradi upo ama vipi....maana na sisi tuanpenda jirani zetu kuliko tunavyojipenda wenyewe,against even the Bible for that matter...mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe(sisi tunampenda zaidi,yeye anatuchukia)
  Mimi maeneo hayo nimeyapita sana na nakumbuka majuzi walikuwa wanalazimisha tufungua border post moja yenye manufaa zaidi kwao na nawasifu TANAPA kwa kudindia hilo.
   
 19. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,520
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kwa sababu za kizalendo hebu msome Mkuu Kichuguu ambaye amefafanua kinagaubaga. Kwa masahihisho kidogo tu ni kwamba baada ya kufanyika study nyingi tu, ikaonekana kuwa kupitisha barabara kupitia Nabi Gate, itakuwa expensive na ingelazimisha kupitia kwenye babrabara ya sasa, japokuwa diversion yake pia itasababisha negative social and economic impacts kubwa kwa baadhi ya maeneo.

  Ni kutokana na sababu za gharama na kimazingira ikaonekana kuwa ni bora barabara hiyo ichepukie Loliondo kisha itokee Mkoa wa Mara ambapo urefu utapungua na hivyo kupunguza gharama za ujenzi.
   
 20. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kichuguu, imefika wakati tuangalie tunachohitaji kwa manufaa ya wana wa Taifa letu na si manufaa ya wengine at our expense. Kama Taifa lazima tuwe na uthubutu
   
Loading...