Kujaza uwanja mashabiki wa Yanga walizoea kulipiwa na Yusuf Manji

Wameletewa ushahidi kwamba sio CAF tu bali hata ligi ya nyumbani. Wanabaki tuachieni timu yetu. Mnapoizungumzia Simba kwani timu yenu?Makwasukwasu baridii. Wakibanwa kidogo tu ulimi nje.
Mtani kwani unateseka? 🏃‍♀️🏃‍♀️
 
Sidhani kama ni kujifanya kuwa na huruma. Mara zote huwa mjajinasibu kuwa Wananchi mna washabiki wengi nchini kuliko Simba. Lakini hizi statistics zinatia shaka hoja hiyo. Jazeni mlinde hoja, vinginevyo nahisi si hivyo, maybe Simba wapo wengi zaidi nchini, kwa kuwa haiwezekani iwe kwa bahati mbaya kila mara
Huenda nikawa sijui hii kitu Mkuu! Kwani kipimo cha mashabiki kuwa wengi kwenye timu kinapimwa kwa kuingia Uwanjani?
 
Yani Yanga wamekosa ubunifu kabsa, Timu ya wananchi ndo nini sasa?
Hata KMC ambao ndo timu ya wananchi hawajiiti hivi.
Sasa nyie Yanga mnajiita timu ya wananchi, ni wananchi wa wapi? Wa Tanzania?
Na kama ni timu ya wananchi wa Tanzania je, mnafikiri mnaweza mkaifanya Yanga iwe brand ya kimataifa?
Nani mwananchi wa nchi nyingne atakubali kuipenda Yanga ambayo ni timu ya wananchi wa Tanzania?
Kuweni wabunifu, Jipambanueni ninyi ni akina nani?
Wenzenu simba saizi wanajiita ni timu ya watu. Tayri wameshawapiga bao.
Kujiita timu ya watu manake haina mipaka hadi Africa nzima ni watu, dunia nzima ni watu.
Yanga acheni ujanja janja fanyeni kujibrand Sio kuweka vi slogani vyenu vya kipumbavu.
Timu inategemea wanachama afu mnajiita timu ya wananchi, na KMC inayotegemea kodi ya mwananchi ijiitaje sasa?
Manchester City inaitwa The Citizens...Timu ya watu maana yake Mo na familia yake
 
Huenda nikawa sijui hii kitu Mkuu! Kwani kipimo cha mashabiki kuwa wengi kwenye timu kinapimwa kwa kuingia Uwanjani?
Hapana kinapimwa na uhudhuriaji wao kwenye vibanda umiza. Timu zinagawana mia 9 baada ya mechi halafu unauliza kama timu hizi zina mashabiki?Hata kwenye timu za,wenzetu tickets allocation zinagaiwa kutokana na mashabiki timu inaingiza uwanjani.
 
ONGEA NA DATA ,SIO KASHATA ZA KIJIWE CHA KAHAWA MKUU
Kwani siku hizi mzee Kilomoni siyo mshikaji wenu tena?
Screenshot_2019-06-17-17-57-25.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mna tabu nyie!!! Yaani tusiojaza uwanja tumetulia nyie ndio munahangaika. Mutusaidie basi kuwa munaujaza.

Na pia niwakumbushe kwenye mechi za Ligi kuu muwe munajaa huko uwanjani sio kelele tu wakati kujaza kwenu Uwanja tunakujua fika ni kwa baadhi ya mechi na mechi.
Sasa nyie hata mechi kubwa ya kimataifa hamjai.
Kweli unaweza ukawa mwananchi lakini usiwe mzalendo.
Simba, This is the next level.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Huenda nikawa sijui hii kitu Mkuu! Kwani kipimo cha mashabiki kuwa wengi kwenye timu kinapimwa kwa kuingia Uwanjani?
Ni mojawapo ya kigezo kikuu.
Sasa unasemaje mshabiki wa timu afu Kwenye matukio hupatkani.
Hivi nyie Yanga wote ni ccm. Mana hata uhalisia mnaukataa.
Hii bongo ni timu gani iliongoza kwa wachezaji wake kugoma kwa sababu ya stahiki zao zaidi ya Yanga.
Mkiingia uwanjani mtaisaidia timu kulipa wapiganaji wenu.
" unaweza ukawa mwananchi usiwe mzalendo"
 
Wadau nadhani mtakumbuka kuwa Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji alikuwa na utaratibu wa kuwalipia Kadi na Viingilio Mashabiki wa Yanga.Tabia hiyo imezoeleka ka Mashabiki wa Yanga.Sasa hivi Yusuf Manji hayupo hivyo hakuna wa kuwalipia Mashabiki hao ndio maana Wanashindwa kwenda Uwanjani.Namshauri Mwenyekiti wa Yanga arudishe Utaratibu wa Yusuf Manji wa kuwalipia Mashabiki ili waujaze Uwanja.
Kwahiyo ni kweli Yanga walikuwa wanajaza uwanja.

MTU kusema ss ndo tunajaza uwanja ni uduwanzi kufikiri hakujawahi tokea hapa TZ
 
Back
Top Bottom