Kujaribu kupambana na Lissu ni kujaribu kupambana na Mungu mwenyewe

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
382
1,000
Kwa jinsi Tundu Lissu alivyopona katika tukio lile la kushambuliwa tena kwa Bunduki kubwa na kumiminiwa zaidi ya risasi therathini, ni hakika hayupo peke ake kuna mkono wa Mungu mwenyewe.

Tukio la Tundu Lissu ni moja ya kazi za Mungu akihusika yeye mwenyewe moja kwa moja kama ilivyokua katika visa kadhaa katika Biblia na ama katitka Qur'an tukufu.

Katika kisa kimoja ambapo Mungu mwenyewe anahusika ni kisa cha Shedrach, Meshach na Abedinego walipotupwa kwenye Tanuru la Moto, moto ambao ulichochewa mara saba zaidi ya moto wa gesi tunaoufahamu. Cha kushangaza Mfarume Nebukadineza aliona watu Wanne ndani ya tanuru. Je huyu Mtu wa nne ndani ya Tanuru alikua nani kama sio kazi ya Mungu yeye mwenyewe akihusika moja kwa moja. Kwa undani wa kisa hiki soma kitabu cha Daniel katika Biblia Takatifu.

Kazi nyingine ambapo Mungu mwenyewe anahusika moja kwa moja ni katika kisa kingine katika Biblia Takatifu, ambapo sasa Daniel mtu wa Mungu anatupiwa katika Shimo la Simba wenye njaa kali sana. INASHANGAZA Asubuhi ilipofika Mtu wa Mungu Daniel alikua salama salimini kwani Mungu aliwafunga midomo ya wale Simba wenye njaa na uchu kwa mkono wake yeye mwenyewe direct. Kisa hiki pia kinapatikana katika Biblia kupitia kitabu cha Daniel.

Sasa kisa kingine kipya kabisa ambapo Mungu anahusika yeye mwenyewe ni katika kisa cha Mh Tundu Lissu Mtu wa Mungu.Ambapo sasa Risasi kwa maana ya Bullet zaidi ya therathini zinamiminwa kutoka katika mdomo wa Bunduki kubwa za Kivita tena zikitumiwa na Professional Snipers ambao kiuharisia wagehitaji Risasi Moja tu (just one Bullet) kumaliza Mchezo but Mungu mwenyewe Live alishusha Mkono na Kuokoa Maisha ya huyu Mtu wa Mungu Tundu Lissu.

ONYO/TAHADHARI
Kama ilivyokua kwa wale Watu watatu Shedrack,Meshack na Abedinego ambapo hawakuliwa na Moto yaani hata Unywele mmoja vichwani mwao. Lakini Ule Moto Ukawala wale Maaskari Wote waliowabeba hawa Watatu Watu wa Mungu. Ndivyo Mabaya yatakavyowatokea Watu wote Waliohusika na tukio la Tundu Lissu Mtu wa Mungu kupigwa Risasi. Na Mabaya yatawatokea Watu woote wanao jaribu kupambana na Mtu huyu wa Mungu kwani kuna Mkono wa Mungu yeye mwenyewe kwa huyu Mtu wa Mungu Tundu Lissu.

Na pia kama ilivyokua kwa Mtu wa Mungu Daniel kwa kushinda jaribio la kuliwa na Simba na hatimaye wale Watu waliomchongea kwa Mfarume wao ndo Walio Uwawa kwa kuliwa na wale simba na hata Mfupa mmoja usibaki. Ndivyo itakavyotokea kwa Wote waliomchonge kwa Mkuu Mtu wa Mungu Lissu na kupelekea jaribio la kummua.

Hili ni onyo kwa yeyote yule anaye jaribu kupambana na Mtu wa Mungu Lissu kwani kwa kufanya hivyo ni kujaribu Kupambana na Mkono wa Mungu Mwenyewe Live.
 

TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Wanasubiri wagongwe na Punda wengine na Nyati ndio ziwakae sawa.

Yule Jamaa wa NZEGA aligonga Twiga mpaka leo humsikii tena akiongea ongea upumbavu..
Angegonga wa upinzani kesi ya kuuwa nyara asingeikwepa hasa angekuwa Mbowe.
 

TIBIM

JF-Expert Member
Dec 1, 2017
8,026
2,000
Kupona kwa TL ni muujiza wa Mungu,ili wahusika wapate kutubu wapone waziache njia zao mbaya wamtazame Mungu.Tunapoambiwa tutembelee tusafishe makaburi lengo kuu huwa tuujue ukuu wa Mungu kwamba maisha si chochote si lolote, ni heri kupata Furaha ya moyo, kuliko kuvipata vyote.
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,094
2,000
Kama kawaida ya wapinga maendeleo na vibaraka wa ubeberu wakishindwa hoja wanageukia dini/mungu kufanya ghiliba kwa kua wanajua bado watu wengi wanaamini miujiza. Tundu lissu ni hatari yafaa wananchi kumuepuka kama ukoma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom