Kujadili wagombea Uraisi 2015 wakati Raisi wa sas katushinda ni UPUNGUANI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujadili wagombea Uraisi 2015 wakati Raisi wa sas katushinda ni UPUNGUANI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Jan 20, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii mijadala inayoibuliwa huku ya mara Lowassa for 2015, Prof Mwandosya kugombea 2015, Membe anafaa 2015 mara Sitta na mbio za uraisi 2015 ni upunguani!

  Tunaongelea 2015 wakati 2011 inatushinda. Hao tunaowasema wamekaa tu nchi inateketea tunawajadili eti watagombea 2015. Watagombea ili nini? Sasa hivi wanatusaidiaje? Dowans wanalipwa, IPTL, TRC, Loliondo, Wizi kwenye Halmashauri na mengineyo bado tunapoteza muda kuwafikiria. Kwani kukemea maovu mpaka 2015? Mafanikio yao ni nini sasa hivi? Eti ni wasafi!! Kwani JK kabla ya 2000 alikuwa na uchafu gani tunaoujua? Si aliitwa chaguo la Mungu?

  Saa nyingine tunacheka tamko la waislamu lakini na matendo yetu humu ndani hayapishani sana. Hatuweki vigezo vya kumpata Raisi bora atakayetutoa kwenye dhiki. Tunabaki kujadili watu ambao hatuoni msimamo wao kwenye matatizo yetu ya msingi! Wengine watasingizia collective responsibility, hii haikuzuii kufikiri. Haikuzuii kusimama kidete na kutetea maslahi ya watanzania. Kama waziri au kiongozi unaona unabanwa kutetea achia nafasi na tutakuamini.

  Hakuna sababu ya kupoteza muda kuwajadili watu wasio na msaada kwetu. Nakereka sana viongozi wote wako kimya kuhusu dhuluma inayoendelea. Sio wa upinzani sio wa CCM. Hakuna vitendo ni maneno tu. Dowans ni ya fulani, Dowans kampuni ya kitapeli, Mkataba na Richmond feki, huu sasa ni upuuzi! Ni sawa sawa mtu anakukumbusha jina lako!!

  Maneno huumba lakini siku wananchi waliochoka na porojo zetu watakapochagua msitu na kutokea huko ndio tutajua 2015 nani Raisi!
   
 2. A

  August JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  hili nilisha lielezea hapo nyuma lakini inawezekana kuna watu wa system au kutokuelewa kwa baadhi ya watu basi huleta hizi habari naona kupoza vuguvugu wa masuala ya sasa. lakini ni vizuri kukumbushana watu waache hii tabia.
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Ndio uhuru wa kuongea uo mkubwa! Ama hujui GIGO!!
   
 4. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inakera sana! Nashindwa kuelewa kwamba hao tunaosikia wanatajwa kwamba wanafaa mara hawafai sasa hivi wanafanya nini? Kwa nini wanatuacha tunadhulumiwa? Tunaibiwa? Tunatapeliwa? Kwa nini? Kuna ule msemo 'the silence of our friends hurts more than the noise of our enemy'. Kama wao wanatupenda na wanatufaa ni marafiki zetu, lakini ukimya wao unatuumiza kuliko kelele za mafisadi na wezi wengine! Kuwa kwao safi hakuwapi haki ya kuendelea kukaa kimya
   
 5. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Najua Mwanamageuko ila 2015 asikudanganye mtu sio karibu. Kwa shida tulizo nazo utafikiri ni mwisho wa karne. Tunaanza kumfikiria mtu mwingine wakati huyu tulie nae hatujamalizana nae! Na hao tunaowasema wako nae, tena karibu kuliko sisi. Ndio washauri wake. Anayoyafanya huyu wa sasa wanayaona pia naamini wanashiriki! Kama wanamshauri hawasikilizi mbona bado wako nae? Au ni maslahi?

  Kwa wenzetu mtu kabla ya kuwa mgombea unakuta msimamo wake kwnye mambo kama ushoga, abortion, kodi, mazingira etc unajulikana. Huku hamna hilo! Tunatumia usafi kama kigezo kikuu! Yeye anaweza kuwa 'msafi' marafiki zake mijizi! Halafu anawaendekeza! Uhuru wa kuongea tuutumie kuongea yanayoijenga nchi yetu! Tusiutumie kupiga story!
   
 6. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180

  Maneno huumba lakini siku wananchi waliochoka na porojo zetu watakapochagua msitu na kutokea huko ndio tutajua 2015 nani Raisi![/
  QUOTE]

  Hapo sasa umenena
   
 7. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  UJUE WATU WENGINE SIJUI WANA AKILI MGANDO, WAKATI HAYA MANGURUWE( meaning CCM by HAMAD RASHID) YAMESHINDWA KUTULETEA MAENDELEO WAO BADO WANAWAKUMBATIA,
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  a very tricky debate!
   
 9. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  kaaaaaaaaazi kweli kweli,lakini nadhani ni bora wanaoutaka urais wangetangaza nia mapema ili tupate muda wa kuwajadili kuliko sasahivi watu wanavyojadili uvumi
   
Loading...