Kujadili urais miaka mitatu kabla ya uchaguzi ni dalili za kuchoshwa na rais aliyepo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujadili urais miaka mitatu kabla ya uchaguzi ni dalili za kuchoshwa na rais aliyepo...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jul 26, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  mijadala ya kujadili rais ajae mara baada ya rais kikwete kumaliza awamu yake ya pili ilianza mapema mara baada yakumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,mijadala hii inaonyesha wazi kwamba wananchi hawana hamu tena na rais aliyepo sasa na kama wangekuwa wanaridhishwa na utendaji wa rais wa sasa sidhan kama mijadala hii ingeanza mapema kiasi hiki,ni fursa ya pekee sasa kwa rais kikwete kuyaona hayo na kujiuliza kwa nini mijadala hii ianze mapema kiasi hiki na kisha kujitathmini na kuona kama bado anatosha kuendelea kuwaongoza watz, kwa mawazo yangu ya harakaharaka naona wananchi wamechoshwa na rais kikwete ndio maana mijadala ya urais haiishi kila kukicha.
  NAWASILISHA!!!
   
 2. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,361
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja mia kwa mia.... then nagonga meza kuonyesha msisitizo.
   
 3. k

  kaudagaa Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  naunga mkono hoja..kawaaibisha watu wa pwani na wana uchumi wa mwaka wake kwa kuprove failure, huwezi kutumia mifuko ya hifadhi ya jamii kutimiza ahadi zako za kisiasa instead of finding another source of tax
   
 4. B

  Bob G JF Bronze Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huyo Jk ndie alie sababisha yote haya kwasababu ya udhaifu wake sasa hivi hata watu wasiona akili wanaona wanaweza kuwa Rais, Cheo cha Urais kimekosa value kwa sababu ya utendaji wa ovyo wa Jk na siasa za kifisadi za ccm zimeanza kuenea kama ukimwi hata kwenye vyama Tarajiwa, makundi, chuki, majungu, uzushi, uongo,uchu wa madaraka sasa imekuwa ni kitu kisichoonewa haya tena
   
 5. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli tumechoka na kikwete. Kuanzia pale alipoachiwa nchi mpaka leo mambo yanazidi kwenda pabaya umaskini unaongezeka, rushwa, udini, ukabila, ufisadi, elimu, afya, nishati, chakula mambo kibao hali mbaya. Huyu aliingia madarakani sio kwa ajili ya wananchi bali ufahari wa kuwa yeye amekuwa rais, pia kwa manufaa ya familia yake na marafiki. Tumechoka kwakweli. Tunamuaombea hata dua mbaya. Mungu asikie kilio chetu
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndo maana mi nasema rais asiwe tu anapewa miaka 10 ya nini? Si ajabu kikwete alishachokwa toka 2010 ila kwa kumpa heshma akaachiwa aendelee.. Siamini kwenye siasa ambayo rais lazima a serve 2 terms..everyone wants change sio ccm sio upinzani.. Ccm wenyewe wanataka mabadiliko washajua hakuna law n order tena with this JK guy still in power
   
 7. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenena, kwa kifupi jamaa ameshindwa sana.Halafu hiyo user name yako imenikumbusha riwaya moja zamani sana,safi sana.
   
 8. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli, Nteko Vano Maputo. Nina rafiki yangu alikuwa anaipenda sana hiyo riwaya. Kila ukikaa nae anakusimulia hiyo tu. Kwakeli Jk fate haiko nae tena.
   
 9. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,798
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  nyie ni madereva wa magari ya kampeni? mpo idle mnataka kila siku kuwepo na uchaguzi,
   
 10. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa kwa sababu kama angekuwa ni mzuri watu wangekuwa wanapigania angalau katiba imruhusu a serve 3rd term, lakini hata hii 2nd term watu wamemchoka ile mbaya.
   
 11. l

  lawyer christina Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutamkumbuka JK coz aliyofanya ni mengi na hakuna presidenti yeyote NCHINI waliomtangulia akathubutu kufanya hao.......hv sasa tunajadili Katiba mpya.....vp baba Ben alihubutu hil? Mzee ruksa Je? Baba WA TAIFA ndio alikua mtemi haswaaaaaaa! Jaribu kumfanyia ndivyo siyo uone mziki wake......zamani watu WALIKUA wanapitea tu....Sio sasahv eti ishu ya Ulimboka kila MTU anajua ni Usalama wamemshughulikia hadi Mhusika nimemuona juzi kwenye gazeti la Kubenea.
  Kuna mengi ya kumfagilia Jk.
  Viva Kikwete.........ila punguza tripu, kwani naamini toka mwaka 2005 ulipoanza ruti zako hizo ungekua unahusisha mTz RAIA WA Kawaida labda wa3 kila Tripu basi hadi Leo ingekua nusu ya wapiga kura wako washakwea pipa! Lazima passport I zaidi ya 7 ushajaza wewe Prezident wetu. Kwa Hilo punguza Mkuu WA kaya hali tete uswahilini.
   
 12. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  He he he he eee eti chaguo la Mungu. Kufuru hizi jamani.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hakuna mwananchi anayejadili urais wa 2015 bali wenye nia ya urais 2015 ndo wanajitangaza aidha kwa tamaa zao au kuweza kuchukua tahadhari mapema kutoka na vikwazo ambavyo wakichelewa watakumbana navyo toka kwa miungu watu wa kutoka katika vyama vyao.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sana tu JK rais wa watu. yeye watu walimhitaji wao wanajihitaji wenyewe ili iweje?
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ni makundi ndani ya vyama husika ndiyo yanfanya wenye nia ya urais kujitangaza mapema ili kuvunja nguvu za makundi ya vyama vyao.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Umeona watu wengine bwana. Mijadala ya urais ndani ya Chama tawala utasikia makundi yanawatafuna, lakini mijadala hiyo hivyo ndani ndani vyama vya upinzani anapigwa mawe JK kwa nini yasiwe makundi ndani ya vyama hivyo?

  Au ndo mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu? Hivi wote wanaompinga ZITTO siyo makundi yanayojidai kumuunga mkono SLAA na MBOWE?

  JK bado ni mtu safi, mchapakazi, asiyependa majungu. Piganeni vikumbo lakini mwisho wa siku kitaeleweka kuwa makundi, uchu wa madaraka na kuabudu miungu watu ndani ya vyama vya upinzani ni chanzo cha wajanja kama akina ZITTO kuona mbali na kuanza mapema ili kuvunja hizo nguvu za Umafia.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Pendera fuata upepo, yaani ungekuwa bungeni ungekuwa miongoni mwa mwa wanaosinzia na kukurupuka kugonga meza wakitoka usingizini bila kujua meza zinagongwa kwa sababu gani.
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hawa ni vijana wavivu wamemaliza chuo hawatafuti kazi, wao wamegeuzwa wanamikutano na maandamano yasiyokuwa na mwisho. Wanachoambulia ni kugeuzwa wauaji wa akina Mkumbo na Mnyika.
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Siku zote mazuri ndo yanaigwa. Akina ZITTO lazima wanaridhika na utendaji wa JK na ndiyo maana wanataka kufuata nyayo zake. Habari ya udikteta, umafia wa akina MBOWE na SLAA ndani ya CDM sasa umeshagundulika na kina ZITTO.
  Ni kweli anachojaribu kukwepa Jembe Zitto ni Majungu, chuki , udini na ukabila ndani ya CDM mambo ambayo yamejidhihirisha kutoka kwa akina Mchungaji MSIGWA ya ubaguzi wa wazi wazi.
   
 20. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  Wamefikia hatua hii baada ya kuona upepo unavyokwenda kama sisi wanainchi tusingeonyesha hali ya kukata tamaa wasingaliweza kutangaza adhma yao awali hivi
   
Loading...