Kujadili Katiba Mpya bila ya kujadili Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujadili Katiba Mpya bila ya kujadili Muungano

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MAMMAMIA, Apr 25, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Siku alipokuwa akitangaza majina ya wajumbe wa tume ya katiba, Kikwete alisema kuwa "Wananchi wajadili katiba, wasijadili Muungano" na akasisitiza kuwa watakaojadili Muungano watachukuliwa hatua kali.

  Naye Waziri Mkuu juzi katika hotuba yake alipokuwa akizungumzia suala la mchakato wa katiba mpya, alilisitiza hilo, kuwa ni suala la katiba na sio Muungano.

  Wasiwasi wangu, ikiwa nimeelewa dhamira ya maneno yao, tutawezaje kujadili katiba bila ya kujadili Katiba Mpya (ya Muungano) bila ya kujadili Muungano?. Ukiipitia katiba yetu kuanzia jina lake "KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA" hadi vipengele vyote vilivyomo ndani, vinahusu masuala ya Muungano, serikali, utendaji wake...iweje leo tuanaamiwa tujadili katiba tusijadili Muungano?

  Naomba michango na msaada wenu.
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Nchi ikiongozwa na vilaza mawazo yao yanakuwa kikilaza kilaza, wao wanapiga mkwara kwa kuwa wana jeshi na mabomun lakini wanasahau kuwa sisi tuna Mungu. Wakati ukifika kuuvunja muungano kamwe jeshi halitaweza kuzuia hamasa, wao walitakiwa kuruhusu mijadala huru ambayo ingeimarisha muungano kwa kujadili mahitaji ya watanganyika na wazanzibari ya wakati huu. Mabomu ya machozi yasiwadanganye kuwa ndio dawa ya kuimarisha muungano
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Walichokuwa wanaringia hawa wenzetu, ni imani tu kuwa Tanzania ni nchi ya amani, Watanzania ni wapole, bila ya kusahahu kuwa nyimbo hizo kwa sasa hazina msikilizaji. Upole wa Watanzania usiwape garantii kuwa hawatanyua sauti kudai haki zao kwa mujibu wa vizazi vyao.
   
Loading...