Kuitwa Training TAESA

monta

JF-Expert Member
May 6, 2014
1,125
1,459
Wakuu miezi kadhaa iliyopita nilipeleka CV yangu na taarifa zangu za kitaaluma TAESA kama Taasisi ya serikali inayoshughulika na ajira yani (Tanzania Employment Services Agency).

Nimepigiwa simu niende nikareport kwa ajili ya Training ama Mafunzo,sasa je!kuitwa kwaajili ya mafunzo ina maana nafasi ya kazi tayari imepatikana wanataka kunipa direction jinsi ya kufanya ama kuna nafasi ya kujitolea wanataka wanifunze au nivipi yani.

Tafadhali mwenye kujua kuhusiana na hili naomba anitoe tongotongo anipe ABC's kabla sijareport kwa ajili ya hayo mafunzo.
 
Kuna baadhi ya watu walipata kazi kupitia TAESA japo wengine walianzia kama Interns,ila Sijajua Training wanayomfanyia mtu ofisini kwao ni ya nini
Intern unapangiwa sehemu mbalimbali, na mkataba wa intern kikawaida ni mwaka mmoja. So sehemu ambayo unafanyia intern wakikupenda wanakuchukua moja kwa moja ndio mana unaweza sema wamepata intern toka TaESA.

Kumbuka hawatoi ajira permanent, hiyo kazi ni ya Utumishi. Ila CV yako itakuwa inabustiwa kupitia wao. Kuna jamaa zangu kadhaa waliingia intern shirika flani TaESA akiwa ndo kawaweka. Utendaji wao wa kazi ulipelekea mmoja kupewa mkataba wa kudumu.

Intern hizo unapangiwa sehemu yoyote tu ile yenye uhitaji ila sio pale kwao. Mfano unaweza pelekwa TRA, TANESCO, NGOs mbalimbali. Mfano kuna mwaka flani nilienda omba intern Red Cross nkaambiwa wao wanachukua watu kutoka TaESA, so nkajisajili kwanza kule.
 
Hiyo training ni wanafundisha tu interview techniques na jinsi ya kuandika cv and cover letters basi usihisi ni kazi ushapata hapo ni unapigwa training kama kawaida then badae ndo wanaeza kukuita ufanye interview yao then utaingia kwenye system zao ikitokea kazi ya kada yako wanakupangia nafasi ya intern
 
Wakuu miezi kadhaa iliyopita nilipeleka CV yangu na taarifa zangu za kitaaluma TAESA kama Taasisi ya serikali inayoshughulika na ajira yani (Tanzania Employment Services Agency).Nimepigiwa simu niende nikareport kwa ajili ya Training ama Mafunzo,sasa je!kuitwa kwaajili ya mafunzo ina maana nafasi ya kazi tayari imepatikana wanataka kunipa direction jinsi ya kufanya ama kuna nafasi ya kujitolea wanataka wanifunze au nivipi yani.Tafadhali mwenye kujua kuhusiana na hili naomba anitoe tongotongo anipe ABC's kabla sijareport kwa ajili ya hayo mafunzo.
Kama ulishafanya interview basi ujue unaitwa kupewa mafunzo (orientation) kisha unapangiwa kituo chako cha internship.

Kama ndio umeitwa kwa mara ya kwanza baada ya kujisajiri basi utapewa mafunzo kwa ufupi namba ya kuandaa CV nzuri, namba ya kufanya interview na masuala kama hayo kukujenga kutafuta kazi kimafanikio. Baada ya hapo utapigiwa simu kujulishwa kuhusu tarehe ya kufanya interview.

Baada ya interview, ikitokea nafasi ya internship unayofit basi utaitwa kwa ajili ya orientation ambapo kubwa hasa huwa ni kuelekezwa ethics za kitumishi na baadaye utatajiwa kituo chako unachotakiwa kureport kwa ajili ya kuanza internship.

Ukifanikisha hatua hiyo utapewa contract ya posho ya laki na nusu kwa mwezi kwa ajili ya nauli na chakula, ukibahatika hiyo ofisi unayoenda ukawa unapewa top up hongera wakiwa makauzu ndo ujipange.

Pia usisahau kuwa na akaunti ya benki CRDB
 
Kama ulishafanya interview basi ujue unaitwa kupewa mafunzo (orientation) kisha unapangiwa kituo chako cha internship.
Kama ndio umeitwa kwa mara ya kwanza baada ya kujisajiri basi utapewa mafunzo kwa ufupi namba ya kuandaa CV nzuri, namba ya kufanya interview na masuala kama hayo kukujenga kutafuta kazi kimafanikio. Baada ya hapo utapigiwa simu kujulishwa kuhusu tarehe ya kufanya interview. Baada ya interview, ikitokea nafasi ya internship unayofit basi utaitwa kwa ajili ya orientation ambapo kubwa hasa huwa ni kuelekezwa ethics za kitumishi na baadaye utatajiwa kituo chako unachotakiwa kureport kwa ajili ya kuanza internship.

Nimekuelewa sana mkuu,Je!hayo yote yanaweza fanyika ndani ya mwezi mmoja?yani kufanyiwa Training- interview na kupangiwa kituo direct?
 
Kuna jamaa waliikuwa chini ya Taesa baadae wakapewa mkataba na waliikuwa wanalipwa 150,000/= kwa mwezi Ila Sasa wameajiriwa kwa hyo we komaa tu mkuu kuwa mvumilivu na uwe na nidhamu ya kazi utakapopangiwa mungu si athuman wanasema
 
Sawa mkuu,Asante kwa ushauri
 
Kama ulishafanya interview basi ujue unaitwa kupewa mafunzo (orientation) kisha unapangiwa kituo chako cha internship.
Kama ndio umeitwa kwa mara ya kwanza baada ya kujisajiri basi utapewa mafunzo kwa ufupi namba ya kuandaa CV nzuri, namba ya kufanya interview na masuala kama hayo kukujenga kutafuta kazi kimafanikio. Baada ya hapo utapigiwa simu kujulishwa kuhusu tarehe ya kufanya interview. Baada ya interview, ikitokea nafasi ya internship unayofit basi utaitwa kwa ajili ya orientation ambapo kubwa hasa huwa ni kuelekezwa ethics za kitumishi na baadaye utatajiwa kituo chako unachotakiwa kureport kwa ajili ya kuanza internship.
Ukifanikisha hatua hiyo utapewa contract ya posho ya laki na nusu kwa mwezi kwa ajili ya nauli na chakula, ukibahatika hiyo ofisi unayoenda ukawa unapewa top up hongera wakiwa makauzu ndo ujipange.
Pia usisahau kuwa na akaunti ya benki CRDB
Nilishajisajiri na hii ndio mara ya kwanza naitwa imepita miezi zaidi ya 6.
 
Nenda asee TAESA internship ama trainings zao wanalipwa pia inategemea na ofisi huko mnakopelekwa pia wanawalipa ukienda ka ofisi zao unaweza kata tamaa ila wanatoa sana mchongo na huko kwenye trainings unakolwenda utapata network na connection pia exposure jambo ambalo ni zuri kwa job seeker
 
Sawa mkuu,tayari nimehudhuria Training then next week kutakua na interview.Hivi baada ya Interview inachukua muda gani kupelekwa internship?pia academic certificates zinazohitajika kwenye interview inahusisha Transcript ya chuo?
 
Cheti cha chuo kinakua supported na Academic Transcript haina maana mbaya ukienda navyo,sijui utaratibu woa unachukua mida gani ila mvumilivu hula mbivu kama umekaa muda bila kazi hupungukiwi kitu ukiwa mvumilivu kwa muda so go for it. Atafutae hachoki huchoka akipata
 
cheti cha chuo kinakua supported na Academic Transcript haina maana mbaya ukienda navyo,sijui utaratibu woa unachukua mida gani ila mvumilivu hula mbivu kama umekaa muda bila kazi hupungukiwi kitu ukiwa mvumilivu kwa muda so go for it.
Atafutae hachoki huchoka akipata
Sawa mkuu asante nitachukua pia na transcript
 
Back
Top Bottom