Kuitwa kwenye usaili UDOM tarehe 15-16/10/2011

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Kwa wale walioomba nafasi mbali mbali za Kazi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mnaarifiwa kuwa kutakuwa na mtihani wa kuandika kwa tarehe tajwa hapo juu. Wale tu watakao faulu wataitwa kwa mahojiano (Oral Interview) Majina ya walioitwa ynapatikana kwenye tovuti ya Chuo (Japo sijaona kitu) na kwenye magazeti ya kesho tarehe 12/10/2011.

Kila la heri kwa wale TUTAKAOITWA, twendeni tukaonyeshane kazi!!!! Ukiona kajamaa kafupi na keusi tiii kakiwa na jezi imeandikwa Standard Chartered basi ujue ni ka Gerrard kametoroka mechi ya Man U kameenda kutafuta kazi huko Udom.

Source: TBC1
 
avatar20324_4.gif


Khaaa...(Gerrard)??)

Thanks Mkuu.
 
Kwa wale walioomba nafasi mbali mbali za Kazi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mnaarifiwa kuwa kutakuwa na mtihani wa kuandika kwa tarehe tajwa hapo juu. Wale tu watakao faulu wataitwa kwa mahojiano (Oral Interview) Majina ya walioitwa ynapatikana kwenye tovuti ya Chuo (Japo sijaona kitu) na kwenye magazeti ya kesho tarehe 12/10/2011.

Kila la heri kwa wale TUTAKAOITWA, twendeni tukaonyeshane kazi!!!! Ukiona kajamaa kafupi na keusi tiii kakiwa na jezi imeandikwa Standard Chartered basi ujue ni ka Gerrard kametoroka mechi ya Man U kameenda kutafuta kazi huko Udom.

Source: TBC1


mm nashangazwa na kitu kimoja. inakuwaje watu wanaambiwa wanatakiwa kwenye interview siku tatu kabla au ndo yaleyale (nafasi washachukua watu) ss tunaitwa kwenda kuwahalalishia ajira yao maana walipita bila ya hiyo interview.

sababu.
siyo watu wote walioitwaq kwenye hiyo interview wanatokea DODOMA hivyo watahiniwa watasafiri kutoka sehemu mbalimbali kwenda huko na watakuwa hawajapumzika wanaenda moja kwa moja kwenye interview. mfano mtu anatokea zanzibar au mikoa yakusini inamlazimu kesho asafir afike dar alale.ili ijumaa aelekee dodoma akishafika dodomakesho yake asubuhi anatakiwa kwenye hiyo interview akiwa anauchovu wa siku mbili kwa ajili ya safari kutoka alikotoka kuelekea DODOMA.
HII NI HATARI.
kwani mtu anaingia kwenye hiyo interview akiwa na uchovu matokeo yake anafeli hiyo interview.
HIVYO NADHANI
watu wameitwa ilimradi tu iyonekane kama muliitwa. LAKINI KUMBE TEYARI WAMESHAAJIRI. so wananafasi ya kujitetea kuwa ilifanyika interview ndiyo wakapatikana hao waliopo kazini hivi sasa.


TUMUOGEPE MUNGU TUSIPENDE KUWAHANGAISHA WATU SABABU TU WANASHIDA.
TUWE WAKWELI
 
Inabidi kupima mwenyewe na kufanya gambling yenye kukaribia 100%, ukiona haikaribii kwa nini uende labda kama wanarudisha nauli na sehemu ya kufikia kama nyumba ya kulala na misosi hapo ni sehemu ya kujifunza
 
msaada jamani atakaye yaona majina na gazeti atujuze hapa,ikiwezekana yawekwe hapa majina
 
Jamani nimepitia mtandao wa UDOM nimeona wamekweka tangazo la kuitwa kwenye Interview ila liko tooo general, nimewapigia baadhi ya watu ninaowafahamu hapo UDOM nao hawaelewi kwanini liko hivyo.

Yaani wanataka watu walio-apply waende kwa ajili ya written Interview bila hata kuwa-shortlisted, sijajua wanamaanisha nini hebu nisaidieni mwaya labda kwasababu mimi ni mwalimu wa kiswahili. View attachment interview ya Udom.pdf

Updates
wameweka majina sasa kwa wale wanaotakiwa kwenda huko UDOM naona asubuhi walikua na haraka kidogo, pls angalia kama jina lako limo, ingia kwene website yao au angalia maoni ya wadau katika thread hii au bofya hapa kwa category one
http://www.udom.ac.tz/DOCUMENTS/INTERVIEWEES.pdf
 
Pambaf zao wanataka kuwapotezea watu nauli na fedha za malazi bure. Wao wanajua wanahitaji watu watatu kwenye position moja kwa nini liende kundi la watu 100 kufanya mtihani? Huu ujinga unaniudhi sana kwa kuwa hauwatendei haki watu ambao wanahangaika kutafuta ajira at the same time hawana kipato. Fikiria si kila mtu atatoka Dodoma au Morogoro au Singida. Huenda kuna watu wameapply kutoka pembezoni mwa Tanzania ambao watahitajika kulipa kiasi kikubwa vcha fedha ili kufika Dodoma. We makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma hebu shirikiana na watu wako ili kuondoa huo utata na kuwasumbua watu bure. Kumbekeni kuwa watanzania wengi hivi sasa wamechoka plus miajali barabarani nk.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom