Kuitwa Kazini: Waliomba nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya waliofanya usaili Septemba 03, 2018

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
2,415
2,000
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya waliofanya usaili tarehe 03 Septemba, 2018 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili.

Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo Barabara ya Kivukoni, Jengo la Utumishi, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazijachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.

Aidha, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira.

Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.

View attachment Kuitwa kazini, Machi 14 2019.pdf
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom