Kuitwa dhaifu na kuitwa fisadi, kipi afadhali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuitwa dhaifu na kuitwa fisadi, kipi afadhali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Jun 21, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Tarehe 15 Septemba 2007, aliyekuwa Mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo , CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alitoa orodha ya mafisadi (list of shame) katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke. Pamoja na orodha hiyo kumhusisha Raisi wa Jamhuri Tanzania Col. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, hapakuwepo na kelele kama hizi tunazozishuhudia, kulikoni? Je kuitwa fisadi na kuitwa dhaifu, kipi afadhali?
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  hawa ndio zzm wanatuambia nchi yetu inaheshimika sana kwa amani.Huwa wanachelewa sana update reference zao, na mtaalamu wa kubadili naye akibadili anakuja na outdated stuff.pengine ndio unawapa kwa mara ya kwanza na wataanza bishana na wewe.Hivyo ndivyo watu wanavyoingia nchini na kujigawia kila kitu wakiambiwa wanakuja juu,halafu baadaye wanaamka, wengine wakiwa wanapiga mahesabu
   
 3. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,218
  Likes Received: 10,583
  Trophy Points: 280
  Dhaifu ni soo.... siyo siri
  Umagine mkeo anakwambia wewe ni dhaifu utajisikiaje?
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahi kukiri hadharani kuwa mafisadi, hasa wale waliohusika na wizi wa EPA hawakamatiki, na baadaye alidai kuwa wakikamatwa wanaweza kuyumbisha nchi na uchumi wake. Maneno haya yanathibitisha kuwa mafisadi, kama watu, wana nguvu kuliko taasisi zote za Serikali zinazohusika na masuala ya uhalifu katika Taifa.

  Kwa maneno mengine hapa Waziri Mkuu anatamka wazi kabisa kuwa serikali ni dhaifu na haiwezi kufua dafu mbele ya wahalifu na wahujumu. Spika wa wakati huo, Samwel Sitta naye aliwahi kudai kuwa serikali inaonesha udhaifu mkubwa katika kuwashughulikia mafisadi na hivyo kumtaka Raisi Kikwete apate ujasiri na kuchukua hatua stahiki.

  Mzee Peter Kisumo naye aliwahi kuitahadharisha CCM kwa kuonesha udhaifu mkubwa katika kuwashughulikia wanakichafua chama na kumtaka Mwenyekiti awe jasiri kukinusuru chama anachokiongoza. Viongozi mbali mbali ndani ya chama tawala na serikalini kilio chao kimekuwa hicho hicho, udhaifu wa waliopewa madaraka ya kuviongoza vyombo hivyo.

  Bila shaka yoyote kama wasemavyo wahenga...the buck stops with the topmost leader ambaye madudu yote haya yanafanyika under his watch. Hapa hatumwongelei mtu yeyote yule mwingine, hapana, tunamwongelea Raisi, Kiongozi Mkuu wa serikali, Kiongozi Mkuu wa chama tawala an Amiri Jeshi Mkuu, Col. Jakaya Mrisho Kikwete, period!
   
Loading...