Kuitoa CCM madarakani ni ndoto sana, sema tu wanasiasa hawawezi kusema ukweli mbele za watu

hatibu juma

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
278
195
:A S angel::high5:UKWELI WA YOTE WANAUJUA SEMA KUNA MSEMO USEMEO USIJIVUNJE MOYO KWENYE MASHINDANOOOOO YEYOTE JARIBU TU //////LAKINI USEMI HUO --------- KUWADANGANYA WANANCHI
 
Mikael P Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,933
0
Acha kudanganyanya watu kama siyo unajidanganya. Pona ya ccm ni kusambaratika kwa UKAWA, vinginevyo 2015, watakuwa kama KANU vs NARC.
 
Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,869
2,000
Si ingekuwa hivyo mngetulia tu,sasa mbona mnalialia na UKAWA isitosho mpaka mnawatuma wavuta bange na mabango,pia matamko ya kizushi mkijifanya viongozi wa CDM.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,395
2,000
Wala si kazi zaidi ya mikakati sahihi make hata mkiamua kushinda kwa asilimia kubwa kwanzia vitongoji/mitaa,kata/sheia mpaka wabunge huo unatosha kuwa mwisho wa CCM ..hata kama raisi atabaki wa kwao tayari halmashauri na majimbo vikawa chini ya upinzani sioni tena wapi utaniambia kuitoa CCM ni kazi ngumu tena

Mwisho wa siku kila njama zao zitakuwa zinakwama hence no longer miradi feki/hewa,dili za kuchonga,wizi kwenye halmashauri n.k,na ukiniuliza mie ntakwambia CCM no Tz hata kama rais ni wao
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,938
2,000
Acha kudanganyanya watu kama siyo unajidanganya. Pona ya ccm ni kusambaratika kwa UKAWA, vinginevyo 2015, watakuwa kama KANU vs NARC.

Mkuu hii dhambi ya kuwaongopea vijana ilhali mkijua kuwa haiwezekani UKAWA kuitoa CCM madarakani itawatafuna.
Hebu tuambie mtafanya muujiza gani? Maana tukichukua matokeo ya NCCR, CUF , na CHADEMA mwaka 2010, Hayafikii hata nusu ya Kura za CCM. Kuna mbinu gani mbadala mtatumia?
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Acha kudanganyanya watu kama siyo unajidanganya. Pona ya ccm ni kusambaratika kwa UKAWA, vinginevyo 2015, watakuwa kama KANU vs NARC.
Kwani ukawa imesajiliwa wapi,je mda uliobaki unatosha kuisajili ukawa nyerere alisema acheni vyama vya upinzani vianze lakini vitakufa vyenyewe lakini upinzani wa ukweli utatoka ndani ya ccm.
 
Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,264
2,000
:A S angel::high5:UKWELI WA YOTE WANAUJUA SEMA KUNA MSEMO USEMEO USIJIVUNJE MOYO KWENYE MASHINDANOOOOO YEYOTE JARIBU TU //////LAKINI USEMI HUO --------- KUWADANGANYA WANANCHI

Ni kweli kama katiba iliyopo haitabadilika, tume ya uchaguzi ibaki kama ilivyo,police ccm, usalama wa taifa, rushwa hapo magamba hayabanduki. Timu pinzani itashindaje kama refa ni wao, wasadizi wa refa ni wao na kamisaa ni wao??
 
PICANOL

Member
Mar 19, 2014
57
70
:A S angel::high5:UKWELI WA YOTE WANAUJUA SEMA KUNA MSEMO USEMEO USIJIVUNJE MOYO KWENYE MASHINDANOOOOO YEYOTE JARIBU TU //////LAKINI USEMI HUO --------- KUWADANGANYA WANANCHI

Sasa kama kuwatoa ni ndoto acheni kutumi polisiccm kwenye siasa simameni wenyewe muone kama hayajawakuta ya J.Banda
 
ihs

Member
Jul 24, 2012
93
0
:A S angel::high5:UKWELI WA YOTE WANAUJUA SEMA KUNA MSEMO USEMEO USIJIVUNJE MOYO KWENYE MASHINDANOOOOO YEYOTE JARIBU TU //////LAKINI USEMI HUO --------- KUWADANGANYA WANANCHI

Siwezi kukushangaa, wakati wa enzi za ukoloni wakati ambapo wananchi 10 tu ndio walikuwa wasomi hapa Tanganyika, babu yako wa babu yako aliamini kama wewe tu!! kwamba sisi watanganyika hatuwezi kuwaondoa wakoloni, nzuri zaidi babu yako wa babu yako alikua na sababu nzuri na nyingi kuliko hata wewe leo hii, kwanzan kulikuwa hakuna wasomi, hakuna logistics za kusafiri na kuhamasisha, wananchi wengi walikuwa hawajui lugha, wengi walikuwa wajinga pengine kama wewe, wengi walikuwa na fikra za woga na resitance to change pengine kama wewe, na pia mawasiliano na technohama haikuwepo kabisa!!!! lakini je? wakoloni tuliwatoa??

sasa nini kinashindikana kuwatoa hawa wakoloni weusi?? ukiachilia mbali wananchi waoga na wasio na matumaini kama wewe, tunakosa nini tena??

Natamani nikuone kwa sura, pengine namweleza mzee wa miaka 85. Kama ni hivo, unisamehe
 
Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Ni kweli kama katiba iliyopo haitabadilika, tume ya uchaguzi ibaki kama ilivyo,police ccm, usalama wa taifa, rushwa hapo magamba hayabanduki. Timu pinzani itashindaje kama refa ni wao, wasadizi wa refa ni wao na kamisaa ni wao??

Na ndiyo maana Ole Sendeka akalia machozi na kusema "tukilegeza kamba tu, na kukubali haki itendeke, tunatolewa madarakani". Ebu kama CCM wanajiamini, waachie Uwanja wa kisiasa usawazishwe, halafu wakione cha moto kilichomtoa kanga manyoya!!!!!! CCM ni nyepesi kama karatasi bila haya yaliyotajwa hapa na Danny Jully.
 
karekwachuza

JF-Expert Member
Dec 23, 2013
1,001
1,500
Wewe naona uko usingizini,hivi hujui kuwa 2015 ndio mwisho wa ccm??hiki chama kitakuwa ni chama cha upinzani kama kilivyo TLP,kweli ccm ni janga la kitaifa
 
Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,737
2,000
CCM imekita mizizi iliyokomaa, na hii ni kutokana na UTUMISHI wake uliotukuka kwa wananchi. Hivi vyama vingine ni vya kilaghai.
 
ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,049
2,000
Acha kudanganyanya watu kama siyo unajidanganya. Pona ya ccm ni kusambaratika kwa UKAWA, vinginevyo 2015, watakuwa kama KANU vs NARC.

Uwepo wa ukawa unaipa ccm nguvu.
viongozi waandamizi wa " UKAWA" wanakauli KINZANA kwenye majukwaa ya siasa.
" Sisi hatushiriki uchaguzi"
"Sisi tutashiriki uchaguzi hadi tuing'oe CCM".
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Kuitoa ccm madarakani ni rahis sana! Tatizo wapinzani hawajajipanga kwa kuwaandaa wananchi kwa mabadiliko, mfano ccm ngome yao kuu iko vijijini ambako hakuna maji, elimu ya uraia, barabara nzuri, na hata huduma nzuri za kijamii! Vyama vya upinzani vingefanya ziara za mara kwa mara maeneo ya vijijini ili kuwafungua wananchi na kuwapa elimu ya uraia badala ya kuishia mijini tu! Ukawa bado hawajajipanga vya kutosha ili kuchukua nchi mwaka 2015!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom